warthog gun
JF-Expert Member
- Aug 9, 2018
- 1,466
- 1,260
Nyie vijitu vingine mlikuja duniani kwa bahati mbaya tu, huna point ya kuandika ni bora ukae kimya tu,shithole.Haya sasa anzeni kufanya hiyo mikutano ya hadhara hovyo hovyo hata kuanzia kesho asubuhi.
Ni kweli ndivyo mwongozo unavyosema.Kiukweli wapinzani wameonewa hatari, jukumu LA polis Ni kupewa taarifa sio kuomba kibali
Hayooo,, hayapendwi na wananchi yanalazimisha tu!Acha kupiga porojo nimeshakuambia anzeni hata kesho.
Hawa inzi wa kijani shida tupu ni makopo tu.Hivi Sheria inataka waombe vibali au watoe taarifa kwa jeshi la polisi?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mikutano ya hovyo kama ya Magu?Kuomba vibali pako pale pale. Msifikiri sasa ndio mikutano yenu hovyo hovyo ya hadhara kila siku imeruhusiwa.
Serikali ikiweka siku 7 tuu kuwa ndio muda wa kampeni zitatosha kwa vyama vyote kuwafikia wapiga kura?Mara tu baada ya kuapishwa kuwa Rais wa nchi hii, Rais Magufuli alivipiga marufuku vyama vya upinzani nchini kutofanya mikutano ya kisiasa hadi mwaka 2020, kwa madai kuwa uchaguzi umekwisha, kwa hiyo huo ni wakati wa kufanya kazi na siyo wakati wa kampeni.
Wakati akitangaza hivyo Rais Magufuli, alijua wazi kuwa anaisigina Katiba ya Jamhuri wa Muungano ya mwaka 1977, ibara ya 3(1) ambayo inatamka wazi kuwa "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itakuwa nchi ya kidemokrasia na yenye kufuata mfumo wa vyama vingi" mwisho wa kunukuu.
Jambo la ajabu ni kuwa Jeshi la Polisi nchini liliichukulia tamko hilo kuwa ni sheria na kuanza kuwakamata viongozi wote waliokuwa wameamua kukiuka kauli hiyo ya Rais, na kuwafungulia mashitaka ya kuleta uchochezi, ambayo ilikuwa ni uvunjaji wa dhahiri wa Katiba yetu ya nchi, kwani Jeshi hilo linajua wazi kuwa vyama hivyo vipo kwa mujibu wa Katiba ya nchi na kufanya mikutano ya kisiasa ni moja ya wajibu wao mkuu.
Wakati hayo yakifanyika kwa vyama vya upinzani wenyewe CCM, akiwemo yeye mwenyewe Rais, Katibu Mkuu wa Chama hicho. Dkt Bashiru Ally na Katibu Mwenezi wa Chama hicho, Humphrey Polepole, walizunguka nchi nzima wakifanya mikutano ya hadhara na ya ndani, wakifanya kampeni, bila kubughuziwa na Jeshi la Polisi.
Hata hivyo kama nilivyoeleza kwenye kichwa changu cha habari, kuwa mwaka 2020 ndiyo ushafika, kwa hiyo ni wito wangu kwa vyama vya upinzani kutumia fursa hii adimu, kwa kufanya mikutano ya kisiasa, ambayo itaratibiwa kisayansi zaidi, ili hatimaye ifikapo mwezi wa Oktoba mwaka huu wa 2020, wananchi tukafanye maamuzi kwenye sanduku la kura kwa kuking'oa chama hiki cha CCM ambacho kimedumu kukaa madarakani tokea tupate Uhuru wetu, kwa "mbeleko" ya vyombo vya dola vya Jeshi la Polisi na TISS, badala ya vyombo hivyo vya dola kuwa "neutral" kama vinavyotakiwa kuwa kwa mujibu wa Katiba, badala yake vimekuwa mstari wa mbele kuwalinda watawala wetu na kujigeuza kuwa vitengo vya CCM ili watawala hao wasing'olewe madarakani.
Absolutely true Mkuu warthog gunAlifikiri 2020 ni mbali na atakua ameshaua upinzani kumbe ndo kwanza vimeimalika kuliko wakati mwingine wowote uliopita.
Nakubaliana nawe Mkuu shungurui kuwa Rais alidhani kuwa mwaka 2020 hautafika!
Ndiyo maana nikasema kuwa siku hazigandi na mwaka 2020 ndiyo huo ushawadia, kwa hiyo hao Polisi watafute sababu nyingine za kuzuia mikutano ya kisiasa kwa kuwa mwaka aliosema Rais Magufuli wa kufanya mikutano ya kisiasa na kwa kuwa wanachukulia matamko yake kwenye majukwaa ya kisiasa kuwa sheria, sasa mwaka huo wa 2020 ndiyo huo ushafika
Hahahah!!!Upumbafff ukizidi unakua kituko!!!!Yaani ulivoandika nikama unayo mamlaka hiyo ya kuruhusu au kusemea.Wewe kwa binafsi yako huna cha kumwambia mtu,huna ubavu huo.At least ungejikomboa kwa kutotumia fake ID na fake avatar.Ati "nimeshakuambia"......khaaa ptuuuu!!!!!puke!!!!Acha kupiga porojo nimeshakuambia anzeni hata kesho.
Umesahau hapa JF ulisema hatamaliza mwaka? Achana na porojo za kitotoKwa nini unadhani "hawezi" kung'oka 2020? Walianguka mabingwa wa siasa kama Kaunda itakuwa huyu asiyeweza hata kujieleza?
Kutolewa 2020 kunategemea mazingira ya uchaguzi na kama wewe unadhani kuwa hatoki kwa sababu utatumika ulaghai na nguvu nawe umekubali huo ndio ujinga! Kwanini atumie njia hizo kisha ionekane ni halali?
Kwa kiongozi mwenye nia kama hiyo anahalalisha mapinduzi kwake kutokua uhaini tena, bali afanyacho ndio uhaini
Uthibitisho ni huu katika comment ya pili
Jamaa alidhani 2020 ni mbali na alidhani atakuwa katunyosha kumbe kanyoka yeye mwenyewe na mafrastrations juuKuomba vibali pako pale pale. Msifikiri sasa ndio mikutano yenu hovyo hovyo ya hadhara kila siku imeruhusiwa.
Fanya kazi mkuu upate hela acha wivu hapa hakuna mwanachadema mwenye kipto cha chini wala mwenye sifa yoyote ya umaskini.Pamoja na tafakuri yako, jaribu kuhangaikia mkate. Siasa za JF hazitakufikisha popote maana
View attachment 1313558
Mbona hujajibu swali na badala yake unatoa vitisho tu, hivi watu kama nyie huwa mnazaliwa wapi? Ccm wana mbinu sana, yawezekana hata wewe ulikuwa timamu ila wakakufanyia ndivyo sivyo mpaka umekuwa hiviHaya sasa anzeni kufanya hiyo mikutano ya hadhara hovyo hovyo hata kuanzia kesho asubuhi.