Uchaguzi 2020 Siku hazigandi, mwaka 2020 aliotangaza Rais Magufuli kuwa ndiyo mwaka wa kufanya mikutano ya kisiasa, kwa vyama vya upinzani, ndio huo ushafika

Uchaguzi 2020 Siku hazigandi, mwaka 2020 aliotangaza Rais Magufuli kuwa ndiyo mwaka wa kufanya mikutano ya kisiasa, kwa vyama vya upinzani, ndio huo ushafika

Alifikiri 2020 ni mbali na atakua ameshaua upinzani kumbe ndo kwanza vimeimalika kuliko wakati mwingine wowote uliopita.
 
Mara tu baada ya kuapishwa kuwa Rais wa nchi hii, Rais Magufuli alivipiga marufuku vyama vya upinzani nchini kutofanya mikutano ya kisiasa hadi mwaka 2020, kwa madai kuwa uchaguzi umekwisha, kwa hiyo huo ni wakati wa kufanya kazi na siyo wakati wa kampeni.

Wakati akitangaza hivyo Rais Magufuli, alijua wazi kuwa anaisigina Katiba ya Jamhuri wa Muungano ya mwaka 1977, ibara ya 3(1) ambayo inatamka wazi kuwa "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itakuwa nchi ya kidemokrasia na yenye kufuata mfumo wa vyama vingi" mwisho wa kunukuu.

Jambo la ajabu ni kuwa Jeshi la Polisi nchini liliichukulia tamko hilo kuwa ni sheria na kuanza kuwakamata viongozi wote waliokuwa wameamua kukiuka kauli hiyo ya Rais, na kuwafungulia mashitaka ya kuleta uchochezi, ambayo ilikuwa ni uvunjaji wa dhahiri wa Katiba yetu ya nchi, kwani Jeshi hilo linajua wazi kuwa vyama hivyo vipo kwa mujibu wa Katiba ya nchi na kufanya mikutano ya kisiasa ni moja ya wajibu wao mkuu.

Wakati hayo yakifanyika kwa vyama vya upinzani wenyewe CCM, akiwemo yeye mwenyewe Rais, Katibu Mkuu wa Chama hicho. Dkt Bashiru Ally na Katibu Mwenezi wa Chama hicho, Humphrey Polepole, walizunguka nchi nzima wakifanya mikutano ya hadhara na ya ndani, wakifanya kampeni, bila kubughuziwa na Jeshi la Polisi.

Hata hivyo kama nilivyoeleza kwenye kichwa changu cha habari, kuwa mwaka 2020 ndiyo ushafika, kwa hiyo ni wito wangu kwa vyama vya upinzani kutumia fursa hii adimu, kwa kufanya mikutano ya kisiasa, ambayo itaratibiwa kisayansi zaidi, ili hatimaye ifikapo mwezi wa Oktoba mwaka huu wa 2020, wananchi tukafanye maamuzi kwenye sanduku la kura kwa kuking'oa chama hiki cha CCM ambacho kimedumu kukaa madarakani tokea tupate Uhuru wetu, kwa "mbeleko" ya vyombo vya dola vya Jeshi la Polisi na TISS, badala ya vyombo hivyo vya dola kuwa "neutral" kama vinavyotakiwa kuwa kwa mujibu wa Katiba, badala yake vimekuwa mstari wa mbele kuwalinda watawala wetu na kujigeuza kuwa vitengo vya CCM ili watawala hao wasing'olewe madarakani.
Serikali ikiweka siku 7 tuu kuwa ndio muda wa kampeni zitatosha kwa vyama vyote kuwafikia wapiga kura?
 
Kuna mikutano ya hovyo kama ya Magu?
Hebu imagine wasaidizi wake "wanaagizwa" eti wadai kuwa msafara wa Rais unesimamishwa njiani ili aongee na wananchi!

Hivi mnadhani nyinyi makada wa CCM mtaendelea,kutuongopea hadi lini?
 
Alifikiri 2020 ni mbali na atakua ameshaua upinzani kumbe ndo kwanza vimeimalika kuliko wakati mwingine wowote uliopita.
Absolutely true Mkuu warthog gun

Huyu jamaa alikuwa amepigia hesabu ya kuua upinzani nchini kabla ya mwaka huu wa 2020 kwa njia zake ovu

Badala ya kufa upinzani, ndiyo kwanza umeimarika mara dufu!
 
Mods, tayari wamenyofoa comment yangu, waambieni hao tiss haisaidii maana tukikaa kimya hata mawe yatasema, hivyo tiss ni jukumu lao kuhakikisha mauaji, utekaji na wizi wa hela za wananchi unakoma na sio kutoa order kufuta topic au comments zinazoonyesha mazaifu ya jiwe, tena tiss mnastahili kubeba lawama zote, maana mngekuwa mnatimiza wajibu wenu vizuri huyu mtu asinge kuwa hapo alipo.
Nakubaliana nawe Mkuu shungurui kuwa Rais alidhani kuwa mwaka 2020 hautafika!

Ndiyo maana nikasema kuwa siku hazigandi na mwaka 2020 ndiyo huo ushawadia, kwa hiyo hao Polisi watafute sababu nyingine za kuzuia mikutano ya kisiasa kwa kuwa mwaka aliosema Rais Magufuli wa kufanya mikutano ya kisiasa na kwa kuwa wanachukulia matamko yake kwenye majukwaa ya kisiasa kuwa sheria, sasa mwaka huo wa 2020 ndiyo huo ushafika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka yaenda mbio ooh mama hatimaye 2020 imefika Jiwe hajafanya chochote cha maana kinachoonekana
 
Miaka yaenda mbio ooh mama hatimaye 2020 imefika Jiwe hajafanya chochote cha maana kinachoonekana
 
Jiwe linadanganywa kwamba wananchi wanalipenda,, lakini ukweli ni kwamba jiwe halipendwi hata ndani ya serikali yenyewe! Hivi mliona maandamano ilipovumishwa kwamba jiwe limedanja?
 
Acha kupiga porojo nimeshakuambia anzeni hata kesho.
Hahahah!!!Upumbafff ukizidi unakua kituko!!!!Yaani ulivoandika nikama unayo mamlaka hiyo ya kuruhusu au kusemea.Wewe kwa binafsi yako huna cha kumwambia mtu,huna ubavu huo.At least ungejikomboa kwa kutotumia fake ID na fake avatar.Ati "nimeshakuambia"......khaaa ptuuuu!!!!!puke!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini unadhani "hawezi" kung'oka 2020? Walianguka mabingwa wa siasa kama Kaunda itakuwa huyu asiyeweza hata kujieleza?
Kutolewa 2020 kunategemea mazingira ya uchaguzi na kama wewe unadhani kuwa hatoki kwa sababu utatumika ulaghai na nguvu nawe umekubali huo ndio ujinga! Kwanini atumie njia hizo kisha ionekane ni halali?
Kwa kiongozi mwenye nia kama hiyo anahalalisha mapinduzi kwake kutokua uhaini tena, bali afanyacho ndio uhaini
Umesahau hapa JF ulisema hatamaliza mwaka? Achana na porojo za kitoto
 
Hizo unazijua wewe.........

Mimi nina ID moja tu hapa JF nayo ni hii ya Mystery
Uthibitisho ni huu katika comment ya pili
 
Kuomba vibali pako pale pale. Msifikiri sasa ndio mikutano yenu hovyo hovyo ya hadhara kila siku imeruhusiwa.
Jamaa alidhani 2020 ni mbali na alidhani atakuwa katunyosha kumbe kanyoka yeye mwenyewe na mafrastrations juu
 
Back
Top Bottom