Uchaguzi 2020 Siku hazigandi, mwaka 2020 aliotangaza Rais Magufuli kuwa ndiyo mwaka wa kufanya mikutano ya kisiasa, kwa vyama vya upinzani, ndio huo ushafika

Uchaguzi 2020 Siku hazigandi, mwaka 2020 aliotangaza Rais Magufuli kuwa ndiyo mwaka wa kufanya mikutano ya kisiasa, kwa vyama vya upinzani, ndio huo ushafika

Mara tu baada ya kuapishwa kuwa Rais wa nchi hii, Rais Magufuli alivipiga marufuku vyama vya upinzani nchini kutofanya mikutano ya kisiasa hadi mwaka 2020, kwa madai kuwa uchaguzi umekwisha, kwa hiyo huo ni wakati wa kufanya kazi na siyo wakati wa kampeni.

Wakati akitangaza hivyo Rais Magufuli, alijua wazi kuwa anaisigina Katiba ya Jamhuri wa Muungano ya mwaka 1977, ibara ya 3(1) ambayo inatamka wazi kuwa "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itakuwa nchi ya kidemokrasia na yenye kufuata mfumo wa vyama vingi" mwisho wa kunukuu.

Jambo la ajabu ni kuwa Jeshi la Polisi nchini liliichukulia tamko hilo kuwa ni sheria na kuanza kuwakamata viongozi wote waliokuwa wameamua kukiuka kauli hiyo ya Rais, na kuwafungulia mashitaka ya kuleta uchochezi, ambayo ilikuwa ni uvunjaji wa dhahiri wa Katiba yetu ya nchi, kwani Jeshi hilo linajua wazi kuwa vyama hivyo vipo kwa mujibu wa Katiba ya nchi na kufanya mikutano ya kisiasa ni moja ya wajibu wao mkuu.

Wakati hayo yakifanyika kwa vyama vya upinzani wenyewe CCM, akiwemo yeye mwenyewe Rais, Katibu Mkuu wa Chama hicho. Dkt Bashiru Ally na Katibu Mwenezi wa Chama hicho, Humphrey Polepole, walizunguka nchi nzima wakifanya mikutano ya hadhara na ya ndani, wakifanya kampeni, bila kubughuziwa na Jeshi la Polisi.

Hata hivyo kama nilivyoeleza kwenye kichwa changu cha habari, kuwa mwaka 2020 ndiyo ushafika, kwa hiyo ni wito wangu kwa vyama vya upinzani kutumia fursa hii adimu, kwa kufanya mikutano ya kisiasa, ambayo itaratibiwa kisayansi zaidi, ili hatimaye ifikapo mwezi wa Oktoba mwaka huu wa 2020, wananchi tukafanye maamuzi kwenye sanduku la kura kwa kuking'oa chama hiki cha CCM ambacho kimedumu kukaa madarakani tokea tupate Uhuru wetu, kwa "mbeleko" ya vyombo vya dola vya Jeshi la Polisi na TISS, badala ya vyombo hivyo vya dola kuwa "neutral" kama vinavyotakiwa kuwa kwa mujibu wa Katiba, badala yake vimekuwa mstari wa mbele kuwalinda watawala wetu na kujigeuza kuwa vitengo vya CCM ili watawala hao wasing'olewe madarakani.
Hivyo wewe naomba nikuulize swali, unaelewa kweli lengo la binadam kuwa na maisha hapa duniani?

Binadam hajaumbwa ili kutwa kucha aje kupiga porojo za kisiasa. Siasa ni nini katika msingi wa maisha ya binadam?

Biologically ninavyo elewa mimi ni kwamba ili binadam aweze ku savive anahihitaji basically chakula. Mbali na chakula anahitaji maji na hewa na hasa oxygen ili aweze kuondoa kiu na kupata pumzi, kwani mwili wa binadam ili uwe na uwezo kuwa salama na kunawiri anahitaji catabolic processes ambazo zinatokea kwenye kila cell ya tissues zetu kwenye mwili.

Sasa ukija na mambo ya kila wakati kupiga siasa za porojo na longo longo nyingi, sidhani kama binadam huyo atakuwa na mda wa kuweza kuzalisha nafaka na kurahisisha upatikanaji wake na maji, vitu ambavyo ni muhimu kwa maisha yake, kwa kuweka miundo mbinu ya kurahisisha upatikanaji wa mahitaji muhimu hayo kwake.

Katiba sio msaafu wala biblia kiasi kwamba ukaiweka mbele kuliko uhai wa binadam. Binadam anahitaji maisha na maisha yanakuja kwa kupata mahitaji makuu matatu, chakula kutokana na nafaka, maji na hewa. Sijasikia na wala sijajifunza kwamba ili binadam aweze ku savive anahitaji siasa au katiba.

Ikumbukwe kwamba kwa vile Rais Kikwete na viongozi wengine katika kipindi cha kumaliza mhula wake wa awamu ya nne hii nchi aliiweka katika hali ambayo sio ya kueleweka kimfumo na maisha, ilikuwa ni sababu kubwa sana ambayo ilimfanya Rais Magufuli, kama jemedali wa nchi na kiongozi aliye pewa dhamana na watanzania kwa kulitambua hilo ilibidi tuchukue maamuzi magumu ili kuweka nchi iwe sawa na watu waweze kuishi kwa usalama na amani.

Hiyo ndiyo maana ya mtu kuwa kiongozi. Kiongozi hayuko kwa ajili ya kuyafanya maisha ya watu anao watawala au kuwaongoza yawe katika hali ya sintofahamu, la hasha, kiongozi yuko vile vile kwa ajili ya kuchukua maamuzi magumu inapo bidi ili kuhakikisha kuwa watu wanao mtegemea kuwa na maisha yenye amani na furaha.

Wewe mwenyewe kama mwana siasa au mfuatiliaji wa mambo ya siasa nafikiri utakuwa katika maisha yako umesha wahi kusoma kitendo ambacho Rais Roosevelt wa Marekani alikifanya baada ya kuona nchi yake iko katika hali ya kufanya mabadiliko ya kimfumo wa kisia kinguvu.

Rais Roosevelt ilibidi achukue maamuzi mazito ya kuwaita mabepari wote walio kuwepo nchini humo na kuwaeleza ukweli wa mambo ya maisha ya watu anao waongoza ulivyo. Na kwamba inabidi wafanye kitu ili kuondoa janga ambalo lilitarajiwa kutokea kama wasinge amua kuchukua hatua zozote zile ambazo ziliwawezesha kwa kiasi kikubwa kuzuia kutokea kwa mabadiliko hayo ya kimfumo wa kisiasa

Je, uamuzi huo aliouchukuwa Rais Rusewelt wa kuwalazimisha makapitalisti kufanya kitu ili kuepuka machafuko ya nchi kwa kuwa lazimisha matajiri hao kutoa kiasi fulani cha fedha walizo kuwa wamechuma ili kuwagawia wananchi wenye matatizo, ulikuwa umeandikwa katika katiba yao kuwa afanye hivyo? Jibu lake ni hapana, ila yeye kama kiongozi alijikuta yuko katika Situation ambayo ilimfanya lazima atafute mbinu ambayo itawawezesha watu anao waongoza wawe na maisha ya maelewano na matajiri. Vinginevyo kama machafuko yangetokea basi wote matajiri na masikini wangeweza kwa namna moja au nyingine wakapoteza aidha maisha yao au utajiri wao.

Kutokana na bandiko lako hili juu ya shutuma zako kwa Rais Magufuli za kitendo chake cha kuzuia maandamano ya vyama vya siasa kufanyika mpaka mwaka 2020, wakati wa kampeni ya uchaguzi, linaonyesha kiasi gani wewe ni immature katika kutambua mambo ambayo nchi yetu yalikuwa yanakabiliana nayo na kwamba uamuzi wa haraka ulitakiwa kuchukuliwa ili kuweza kuzuia kutokea kwa hatari ambayo ingeweza kutokea na kuathiri maisha ya wananchi kama Rais asinge chukua maamuzi mazito ya kuzuia maandamano hayo ya vyama vya kisiasa.

Wewe kama mwelewa wa katiba na siasa zinazo mwuhusu binadam kwa ujumla ulitakiwa kutambua hali ya sintofahamu ambayo wananchi walikuwa wanaiishi na migogoro ambayo ilikuwepo miongoni mwa wananchi hao. Kwa hiyo kufanya siasa kimazoea kwa vile katiba imeruhusu wananchi au vyama vya kisiasa kufanya maandamano hata kama mazingira ya wananchi ya kuishi pamoja kwa amani hayaruhusu na sio rafiki, sielewi kama inge kuwa ni busara, kwani hakuna ambaye angetabiri hali hivi sasa ingekuwaje.

Binadam mwenye akili pungufu na ambaye hana fikra nzuri za kuishi pamoja kwa amani na binadam wenzake utamtambua pale anapo shindwa kufahamu hali ya maisha ya binadam wenzake wanao mzunguka ikoje ili hali hiyo ya amani ikadumishwa. Sidhani kama mtazania mwenye akili timamu alitakiwa kuambiwa atazame hali ya maisha ya shida ya watu iliyo kuwepo na migogoro ya vyama vya kisiasa iliyo kuwepo pia miongoni mwetu ili aweze kutambua umuhimu wa hatua kuchukuliwa kuondoa au kupunguza shida na migogoro hiyo. Ni kichaa tu na mwendawazimu au mtu mwenye akili za kitoto angeweza kuwa katika hali ya kuto tambua matatizo hayo.

Kabla ya Rais Magufuli kuchukua madaraka nani atakataa kuwa hali ya maisha ilikuwa isiyo kubalika nchini? Rushwa ilikiwa imetapakaa kila sehemu na kila sekta, maofisini kulikuwa hakuna dsicipline, bandarini hovyo, hospitalini hovyo, kwenye biashara hovyo, kwenye uzalishaji wa mazao hovyo, elimu yetu hovyo, mahakamani na polisi hovyo, kwenye usafiri wa anga, majini na barabara hovyo, usalama hakuna, umoja wetu ulikuwa hatarini kuangamia, dhulma ilijaa na sidhani kama haki za binadam zilikuwa hazikiukwi. Nchi hii kila mtu aliye kuwa na madaraka kidogo alifanya alicho kitaka.

Mtu ambaye analiona Taifa lake liko katika hali hii na bado anatetea maandishi ya katiba, sidhani kama huyo mtu analitendea haki Taifa letu. Atakuwa ni mtu wa ajabu sana. What is katiba? Itakuwa ni ujinga kwa Taifa kuzingatia maandishi au vipengee ambavyo vimebuniwa na kuandikwa na binadam wakati ambao kulikuwa hakuna internet na Smartphones na Globalization. Huko ni kujiua mwenyewe.
Katiba yetu inatakiwa iende na wakati na sio kung'ang'ania vitu ambavyo havitatupa manufaa yeyote maadam vimeandikwa kwenye katiba. Huo ni upuuzi.

Kwa uelewa wangu wa demokrasia ni hali ambayo ina mruhusu mtu au kundi la watu kupiga kura ya kumchagua mtu wanao mwona anafaa kuwaongoza, kulingana na itikadi za kisiasa za chama chake, lakini hata hivyo serikali ya nchi yenye mfumo wa kidemokrasia na yenye kufuata mfumo wa vyama vingi haizuiwi au kukatazwa kuwalinda wananchi wake inapo onekana kuwa kuna vurugu inanukia kutokea. Kwa misingi hiyo Jeshi la Polisi nchini lina wajibu wa kulinda amani na kuitetea demokrasia yetu. Jeshi la Polisi halijaichukulia tamko la Rais kama ni sheria.

Kitu ambacho mleta mada ulitakiwa ukitambue ni kwamba demokrasia, haki za binadam na mfumo wa vyama vingi ni Elements tu za Human dignity. Na katika nchi nyingi zilizoendelea kama Ujerumani kwa mfano sheria yao ya kwanza ina sema "Menschenwürde ist unantastibar" maana yake ni kwamba "Human dignity is inviolable".kwa kiingereza. Hii ina maana kuwa awali ya yote Ubinadamu kwanza.
Hatuwezi tuka yaweka maisha ya binadam at risk eti kwa sababu ya demokrasia. Na serikali inayo hatarisha maisha ya wananchi wake kwa kutumia kauli mbiu za demokrasia na haki za binadam kwa kuruhusu fujo na uaribifu wa mali za watu itokee, serikali ya namna hiyo inapaswa kuondolewa madaralani haraka iwezekanavyo na kuwekwa serikali nyingine na watu wanao tumia kauli mbiu hizi kuhatarisha maisha ya watu wengine kwa kuleta fujo na kuharibu mali zao wanapaswa kushtakiwa na kuhukumiwa.

Rais wa nchi kama The Head of State ni lazima kwa ukubwa wa majukumu yake kuzunguka nchi nzima kuona kama ilani ya chama chake inatekelezwa kwa manufaa ya wananchi wote, elewa kuwa Rais ana accountability kwenye chama chake na pia kama kiongozi wa serikali kwa wananchi wake. Ni wajibu wake kuzunguka nchi nzima kukionyesha chama chake utekelezaji wa ilani yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom