Siku hizi tumeamua kukinunua kifo kwa gharama zetu wenyewe

Joshua Mbezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
1,994
Reaction score
4,446
Katika jamii zetu kumekuwa na visa vya mara kwa mara vya ajali za moto na watu kupoteza maisha hatuwezi kupingana na husemi husemao kuwa hakuna ajuaye siku ya kifo chake yawezekana ikawa ni baadae kidogo au ata kesho

Lakini je hivi vifo vingine vinavyotokea katika jamii haviwezi kudhibitiwa? Mfano ajali za watu kuungulia ndani ya Nyumba

Watu wengi wamepiga hatua katika kuwa na makazi Bora na imara lakini je ni nani anayezingatia dharula au Kinga wakati wa kujenga Nyumba kwa ajiri ya makazi?

Leo hii mtu anajenga Nyumba, milango ya chuma,madilisha ya chuma, juu kwenye celling board anaweka zege tena lenye saruji Kali

Lakini je kwenye hizo Nyumba Bora na imara nani anakumbuka kuweka mlango wa dharula?

Au hata andaki litakalomwezesha kujiokoa pindi majanga yanapotokea?

Nafikiri watu wahimizwe kujenga Nyumba ambazo zinakuwa na sehemu ya dharula ili kupunguza baadhi ya athari hasi zinazoweza kujitokeza katika maisha yetu ya kila siku.
 
Attachments

  • 1749901882699.jpg
    1749901882699.jpg
    397.5 KB · Views: 32
Uzi nimeusoma ukanikubusha kuna mafuta robo lita ya petroli nilijisahau nikaingia nayo jikoni na kuwasha jiko la mkaa, haraka nikakatoa nje fasta hako ka chupa cha petroli, kalikuwa kamefungwa. Duh! Ningepoteza maisha kizembe
 
Katika jamii zetu kumekuwa na visa vya mara kwa mara vya ajali za moto na watu kupoteza maisha hatuwezi kupingana na husemi husemao kuwa hakuna ajuaye siku ya kifo chake yawezekana ikawa ni baadae kidogo au ata kesho
Lakini je hivi vifo vingine vinavyotokea katika jamii haviwezi kudhibitiwa? Mfano ajali za watu kuungulia ndani ya Nyumba
Watu wengi wamepiga hatua katika kuwa na makazi Bora na imara lakini je ni nani anayezingatia dharula au Kinga wakati wa kujenga Nyumba kwa ajiri ya makazi?
Leo hii mtu anajenga Nyumba ,milango ya chuma,madilisha ya chuma, juu kwenye celling board anaweka zege tena lenye saruji Kali
Lakini je kwenye hizo Nyumba Bora na imara nani anakumbuka kuweka mlango wa dharula?
Au ata andaki litakalomwezesha kujiokoa pindi majanga yanapotokea?
Nafikiri watu wahimizwe kujenga Nyumba ambazo zinakuwa na sehemu ya dharula ili kupunguza baadhi ya athari hasi zinazoweza kujitokeza katika maisha yetu ya kila siku.
Sisi wanadamu nadhani hata panya wanatuzidi maarifa,wachimbapo shimo huacha sehemu ya kutorokea,lkn wanadamu wanajizibia mpk njia za kujiokolea
 
Back
Top Bottom