Siku mbili, Wanaharakati wawili: Collins Otieno Apatikana akiwa hai.

Siku mbili, Wanaharakati wawili: Collins Otieno Apatikana akiwa hai.

Wakaguongo

Member
Joined
Sep 23, 2026
Posts
95
Reaction score
38
Mwanaharakati mwengine Collins Otieno amepatikana akiwa hai, siku moja tu baada ya mwanaharakati mwenzake Boniface Mulinge Muteti pia kupatikana baada ya kuripotiwa kutoweka.
550.jpg


Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Hussein Khalid wa Vocal Africa, Collins alipatikana kando ya Thika Road majira ya saa 4:30 alfajiri Jumamosi, baada ya mwendesha bodaboda aliyekuwa akipita kumwona na kumpeleka hospitalini.
551.jpg


Kwa sasa anapokea matibabu katika hospitali ya Neema Uhai eneo la Kasarani, huku Khalid akisema yuko dhaifu, amechanganyikiwa na ana majeraha, hali inayofanana na ile aliyokuwa nayo Muteti alipopatikana jana huko Lukenya.

Collins na Muteti walikuwa miongoni mwa Wanaharakati waliokamatwa wakati wa maandamano ya Nairobi CBD mnamo Septemba 21 ya kushinikiza kuachiwa kwa Mwanasiasa wa Uganda Kizza Besigye. Baadaye Collins alitoweka wakati akijaribu kusaidia kufuatilia alikokuwa Muteti.

Hivyo ndani ya takribani siku mbili, kumekuwepo na matukio mawili yanayofanana: Wanaharakati wawili wamepatikana wakiwa 'wametupwa' pembeni mwa bara bara usiku.

Je, ni nani anatekeleza utekaji huu na je, mamlaka zitaanzisha uchunguzi wa kina kuhusu matukio haya mawili na kutoa majibu kuhusu walikokuwa wanaharakati hawa kabla ya kupatikana?
 
Back
Top Bottom