Siku muungano ukivunjika Tanganyika itapata hasara kubwa sana

MUUNGANO UDUMU MILELE HAKUNA WA KUUVUNJA NA ATAKAYEJARIBU KUFANYA HILO ATAVUNJIKA YEYE NA ATAUACHA. Si mwanaccm si mwanachadomo si yeyote yule hata awe nani.
 
Mimi toka utoto nimeuliza hata Walimu wangu shuleni kote nilikopita, kuwa, "Kwanini Tanganyika iliungana na Zanzibar?"
nikajibiwa eti ni kwa sababu za kiusalama.

Sijawah kulielewa hilo jibu, hata humu JF bado sijaona sababu za msingi za jambo hilo.

Nafkiri ni uwoga na kukataa kubeba majukumu, kwamba ili uwe salama inahitaji uuze uhuru wako kwa mtu unayedhani anaweza kukudhuru?

Sasa mleta mada hicho ulicholeta hapa kabla sijakujibu, hv Rwanda, Congo wana maeneo ya bahari?
 
Kwanza tuanze kwa kuzungumza kuhusu sheria za mambo ya bahari. Sheria za kumataifa zinasema kuwa kutoka pwani ya nchi hadi nautical miles 12(22Km)kuingia baharini(1NM=1.85km). Ni eneo la bahari la nchi husika. Yaani hapo nchi inamiliki
Zanzibar ndio watateseka muungano ukifa nadhani hata kula yao itakuwa mashakani.
 
Hata kama uko sahihi, je Uganda wana eneo kiasi gani cha bahari? Rwanda, Zambia, etc. Ndoa ikishavunjika Kila upande unapoteza na maisha yanaendelea.
 
Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki TANZANIA

Mungu ubariki muungano udumu milele
Aamin
 
muungano uvunjwe tu. maana hicho kijiji ca zanzibar tunaweza tukakiteka anytime tukikihitaji
 
Hawakukosea wakina mwalimu Nyerere kuungana, ila kosa ni huo muundo wa muungano.
Lakini pia hawakufikiri kesho ,kesho kutwa wala mtondogoo! Lau wangefikiri hivyo wangeacha mwanya wa kuuvunja muungano.

Wangechofanya ni kufanya taifa moja, lenye serikali moja, au muungano wa aina huu wenye serikali tatu.

Lakini kubwa la maana wangeacha mwanya wa kuvunja muungano, kwa sababu binadamu hazidhini au hatosheki na hali moja aliyo nayo kwa wakati aliopo.
Ikiwa shetani alishindwa kuendelea kushirikiana na Mungu wakatengana vipi kwa sisi binadamu.
 
neno hili Zamani kilikuwa kinamilikiwa na Tanganyika si sahihi.
Nchi ya Zanzibar ilikuwa na utawala rasmi kwa miaka 1000 nyuma kabla ya Tanganyika. Wakati Wakoloni wa Kizungu akina Vasco Da Gama wankuja waliikuta Zanzibar ikiwa inaikalia Tanganyi kwa jina la Zenji Epire.
Wajerumani na Waingereza waliikuta Zanzibar ikiwa na Ukanda wote wa Afrika mashariki kuanzia Somalia hadi Msumbiji. 200 inland.
Baadae zanzibar Ikapewa Ukanda wa Pwani kwa Maili 20 in Land.
Halafu Wakati wa Muingereza zanzibar ikabaki na Visiwa Vikubwa viwili, Pwani ya Mombasa Kenaya na Kisiwa cha Mafia kilikuwemo.
Ikatolewa dar es salaam na Tanga na Mtwara tu.
Hadi Tunapeana Uhuru 1961 kwa Tanganyika na 1963 kwa zanzibar Mipaka iliyotambulka kwa Zanzbar Ni kuanzia Lantham island Hadi Pemba . Pamoja na Pwani yake.
Kisiwa cha Latham kipo karibu na Kisiju ya Tanganyika. na hapo ndio mwanzo wa Zanzibar.
Visiwa vya Bongoyo pale Dar Havimo.

Kuhusu Utawala ki inchi Zanzibar ndiyo ilikuwa Organized state kabla ya Tanganyika , Maka hiya ya Karne ya 15 tawala za tnaganyika zilikuwa za Kchifu tuu na Kitemi wakati Zanzibar tukiwa na Mfalme Sayid Said mwanzoni mwakarne ya 17
 
Mjerumani alinunua Mafia kutoka kwa Sultan wa Zanzibar. Pamoja na pwani ya Tanganyika na visiwa vyake, pamoja na hicho kisiwa cha Latham. Ndiyo maana utaona kipo karibu na pwani ya Tanganyika kuliko kisiwa cha Unguja.
 
Muungano hauna muda
Your browser is not able to display this video.
 
Mjerumani alinunua Mafia kutoka kwa Sultan wa Zanzibar. Pamoja na pwani ya Tanganyika na visiwa vyake, pamoja na hicho kisiwa cha Latham. Ndiyo maana utaona kipo karibu na pwani ya Tanganyika kuliko kisiwa cha Unguja.
UWE NA NYARAKA ZA KUTHIBITISHA KUWA LANTHAM NI YA TANGANYIKA
Kama huna, bado inakuwa ni mali ya zanzibar
 
Khaaa ndugu kuna nchi hazina bahari kabisa lakini wametukanyaga kiuchumi vibaya vibaya hiyo bahari yote chukueni ninyi wa Zanzibar sisi tuachieni Tanganyika yetu tu basiiii
 
Ndiyo Congo wana eneo la bahari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…