Siku muungano ukivunjika Tanganyika itapata hasara kubwa sana

Tanganyika ilikuwa na mipaka yake kabla ya muungano, muungano haujabadilisha mipaka, hizo hadithi za sijui tutapara hasara ni aina ya mazungumzo ya kipumbavu
 


sasa ww n wakili gan washetan huna akili??
 
Kabla ya muungano
Mpaka wa Tanganyika ulikuwa wapi huko baharini? Na mpaka wa Zanzibar nao ulikuwaga wapi?
 
Na wazanzibari mkae mkijua.. Siku huu Muungano ukivunjika mwaka mmoja hautaisha mtakuja bara kuomba ukimbizi..
 
Mwandishi Asibezwe ana Hoja!
Kwa kiasi kikubwa yupo sahihi!
Yupo sahihi Muungano ukivunjika Bara itaathirika Kiusalama na Kiuchumi.
Sheria ya Mipaka ya Bahari Kuu inatoa faida zaidi kwa zanzibar dhidi ya Bara, huo ni mkweli mchungu.
bandari ya Zanzibar itakuwa lulu, wakati Bandari za Tanga na Dar zitapoteza mvuto.
Hata hivyo Zanzibar nayo itaathirika Kiusalama na Kiuchumi kwani ni mtegemezi mkubwa wa chakula, nishati na Biashara wa Bara. bila Bara ZnZ haitakuwa na soko. Pia inaitegemea sana Bara kiusalama.
Hofu yangu kubwa ni kuwa Kisiwa kinaweza geuka kuwa pango la magendo na kila aina ya crimes za hatari jambo litakalofanya Bara nayo iathirike.

Kimsingi Muungano una tija nyingi kwa pande zote mbili. Kuvunjika kwake kutakula kwetu pande zote.
Cha muhimu ni uwazi na wananchi wapewe fursa ya kuainisha aina ya muungano wautakao, tusilazimishane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…