Siku nikifanikiwa kuwa Rais wa Tanzania; Mafisadi na familia zao zinazoneemeka kwa ufisadi, wataula wa chuya

Baba yako hakukwambia kwamba alikuwa anakusomesha kwa Hela za wizi
 
Utakapokuwa Rais ndio siku utagundua kuna mizizi imejichimbia na ni mikubwa haigusiki na una sehemu ndogo tu ya kucheza nayo, ukifanya tofauti unajikuta mgeni rasmi katika bara usilolijua.
 
Fanana kwanza na jamii inayokuzunguka ficha makucha yako uwe rafiki mzuri na kiumbe yeyote anaeitwa mwana siasa na ishi kwa matakwa ya wengi wanayotaka
 
Itabidi ujenge jela kubwa na ya kuweza kuwafungwa nusu ya wa Tanzania.
 
Yaani mimi hata nikiwa Mtendaji tu wa Kata Majizi yote nitayang'oa Makoromeo
 
Siyo rahisi hivyo mzee, ndo maana Nabii Suleiman aliomba hekima kwa Mungu namna gani atawaongoza mamilioni ya watu waliokuwa chini ya ufalme wake.
 
Anyone can be touched. Wewe ndio mjinga. Mmeshaaminishana huko kua nyie hamgusiki? Kama jiwe alishindwa ndio kila mtu atashindwa? Subiri ujionee
 
Mbona utawamaliza viongozi wote matajiri wa CCM, hawatakubali uipate nafasi hiyo hata kama vita naiwe.
 
Mbona utawamaliza viongozi wote matajiri wa CCM, hawatakubali uipate nafasi hiyo hata kama vita naiwe.
Ninaamini kila kitu kinawezekana. Kwani wao waliwezaje? Tofauti ambayo itakuwepo ni kwamba sitatumia madaraka kujinufaisha mimi na familia yangu, badala yake nitayatumia kwa maslahi mapana ya nchi na watu wake..
 
Duh!

Mkuu 'DEU87', nimeisoma mada yako kwa uangalifu hadi nilipofikia nilipofikia, kabla ya kushindwa kufika mwisho wake.

Umechanganya mambo mengi mno, kiasi kwamba mengi yanagongana.

Kuna mambo mazuri sana, kama hiyo namba 2,....

Lakini niseme wazi, mada yako inaweza kuwa mwanzo wa uchambuzi makini ni yapi yanatakiwa yafanyike kuinusuru Tanzania na unajisi inaofanyiwa nyakati hizi..

Pengine nitapata fursa ya kurudi na kufanya uchambuzi wa aina hiyo niuonao kwa upande wangu.

Lakini inabidi nikwambie hivi: Hakuna Mungu atakayekusubiri ufanye uamzi. Usije ukamsingizia Mungu kwa kushindwa kwako kufanya juhudi kutimiza malengo unayojiwekea mwenyewe.
Hili tu pekee, limekwishaonyesha udhaifu upande wako, hata kabla kazi ya kuinusuru Tanzania hujaianza.

Sasa kumbuka, ukishapata nafasi hiyo unayodhani itakuwezesha kuirekebisha Tanzania, visingizio kibao vitakuwa vikiibuka mara kwa mara, na hapo hapo ukimsingizia Mungu kutoruhusu.

Natumaini utakuwa umenielewa maana yangu.

Mwisho niseme, naungana nawe katika kuililia Tanzania yetu.
 
Deep state (not Votes) reserve the rights of winning presidence

Deep state haipigiwi Kura

Deep state can change president the way and when they wish

nazungumzia deep state ya Belarus sio ya Uzbekistan
Myth.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…