SEHEMU YA PILI **********
*****************************
Wakati fatmah ameniambia kuwa anakaa kwa dadaake sakina jibu lilinishangaza sana ikumbukwe usiku wa jana nilimuota fatmah kaja kwangu usiku na aliniambia anakaa kwa dadaake ambae ni msusi sakina, basi nikamwambia leo jioni uje kwangu akasema usijali nitakuja jioni leo utafurahi uwepo
SEHEMU YA 03
****************
SIKU ile ilikuwa siku nzuri sana kulionja penzi la Fatumah ni mwanamke mzuri sana kuwahi kumuona katika hii dunia ya watoto wa Adam na Hawa[emoji18]
Basi tuliongea mengi sana na Fatmah siku hiyo alinionyeshea mahaba mazito hadi nikawa najisimemea sasa mke si ndio huyu nimepata kumbe sikujua kuwa nilikuwa nimepatikana[emoji29]
Tulionjoi sana nakumbuka usiku wa siku hiyo ya kwanza ya Fatmah kuja kwangu alinipika wali na kabichi na alinionyeshea upendo mmoja sijawahi pata kwanza alikuwa muda wote yupo kifuani kwangu amejilaza ananiambia maneno matamu mume wangu nashukuru mungu nimekupata wewe ni wangu nitakupa mahaba mazito maneno yake yalikuwa yakinipa faraja nikujua kuwa sasa nimepata mke
Nilihisi dunia ni yangu kufupisha stori siku hiyo ndio ikawa mwanzo wa mapenzi yangu mimi na Fatmah ambae ni jini bila kumjua basi usiku ukapita asubuhi nikiwa nimelala na Fatmah aliniamsha mume mimi leo naondoka naenda kwa dada nikamwambia mbona mapema hapo ilikuwa mida ya saa moja asubuhi nikamwambia kwa dadaako ungeenda hata mchana Fatmah akajifikiria basi akanijibu sawa basi ngoja mimi niamke nioge nikufanyie usafi leo
Basi akaamka pale kitanda ni mwanamke mrembo aisee yaani ukiambiwa kuwa ni jini unaweza bisha mazima basi mimi nikiwa kitandani pale nimejilaza Fetty akawa anaosha vyombo punde si punde akaanza kupika chai katika kitu ambacho kilikuwa kinanipa furaha ni jinsi Fatmah alivyokuwa akifanya kazi yaani ilishukua dk 30 kashapika chai kashaosha vyombo kashaoga kamaliza kila kitu akaja kuniambia amka uoge chai tayari nilishangaa sana nikamuuliza aisee umenishangaza sana yaani wewe mchapakazi mno dk 30 ushamaliza kila kitu akawa anacheka
Basi nikaenda bafuni kakuta maji nimeekewa na sabuni kila kitu kinaoga niliporudi sebuleni nilimkuta amekaa kwenye kitu akawa anatabasamu akaniambia mume umependeza ulivyoloana na maji alikuwa akiniangalia garden love zangu basi nikavaa nguo pale basi Fetty akaniambia mume nina zawadi nataka nikupe nikamwambia nipe tu akaniambia nina hii perfume ni kwaajili yako akanipa nilipoipuliza pale ilikuwa ni perfume yenye manukato makali mno yaani inanukia vizuri sana yeye Fetty akawa anafurahi tu nikamwambia ni nzuri mno ndio maana wewe unanukia vizuri kumbe unatumia perfume hii akasema ndio basi tukanywa chai pale huku tukipiga stori Fetty aliniambia swali moja ambalo lilinipa hofu aliniuliza......
Mimi nataka nizae na wewe watoto halafu nije niishi na wewe hivi karibuni upo tayari?
Swali lake lilinishtua mno ukiangalia na maisha yangu ya kuunga unga ningewezaje kuishi na Fatmah walihali sina kitu nikamjibu natamani niishi na wewe hata leo nizae na wewe pia ila sasa maisha yangu ndio bado najitafuta nilipomjibu hivyo akatabasamu halafu akaniambia usijali kuanzia sasa maisha yako yameshakuwa mazuri niamini mimi na kesho utapata dili la hela nyingi ambalo haujawahi kupata
Maneno yake yalinipa furahaa na kunipa wasi wasi pia nikamuuliza umejuaje?
Akacheka halafu akaniambia nimeota tu jana jambo ndoto sio lazima itimie muda mwingine inaweza kutokea kweli au isitokee jibu lake likanifanya nicheke nikamvuta karibu yangu na kumwambia nakupenda sana ni mwanamke wa kipekee sana huku nikamshika na kumpiga busu moja zito mdomoni mwake utamu wa busu langu ulimfanya Fatmah kulalama na kunishika kwa nguvu huku akiendelea na yeye kujivinjali utamu wa mate yangu mdomoni mwake kitendo kilichofanya wote kuangukia kitandani na sasa game kati ya yanga na simba ikaanza rasmi dimbani kwa mkapa stadium huku refa wa mchezo akiwa ni martin saanya ilipigwa mechi ya karibia masaa 2 bila mapumziko huku sauti ya chaga za kitanda zikisikika kwachuuu kwachuuu kachwuuuu baaada ya muda wote tukajikuta tupo hoii hooi tumechoka
Tukiwa tumetulia kitandani Fatmah akaniambia nakupenda sana nitahakikisha nakupa kila kitu kinachokiweza nikamwambia nitafurahi basi ikabidi twende kuoga na Fatmah asikwambie mtu mahaba tuliyokuwa nayo ni zaidi ya Julliette na Romi basi kufupisha stori baada ya kuoga tukavaa then Fattuma akaniambia sasa anataka kwenda kwa dadaake ila alinisisitiza nisije kumsaliti kwani ananipenda sana aliniambia kuja kwangu tena itachukua siku 3 atakuja tena basi nikamsindikiza hadi mtaa wao anapoishi na dadaake Sakina yule fundi msusi wa saloon maarufu kipindi hicho mtaa x.... Chanika tukaagana na mimi nikawa nimeenda kumcheki mwanangu Juma ni kama kakaangu kwani tumekuwa tukisaidiana kwenye shida na raha alikuwa hakai mbali na mimi bahati nzuri nimefika kwake nimekuta ndio nae amefika kutoka mizunguko yake
ooh kaka mambo vp adimu sana kaka sema una balaa ww juma aliniambia huku anacheka akinikalibisha ndani nikamwambia mimi nipo vp balaa gani tena akacheka sana akaniambia nimepata taarifa zako mtaani sasa hivi una bonge moja la demu mtoto shombe shombe, akaongezea haya buana dunia yako hii sema watoto wazuri wanataka hela nikamwambia ndio ni kweli nimepata tu demu kizali zali bro basi akaniambia ni jambo jema basi tukawa tunapiga stori zingine za kawaida,
Bro juma akaniambia vp madili yako ya ufundi yanaendeleaje?
Nikamwambia daah madili magumu sasa maana nilishagombana fundi mkuu akasema pole sana ila tuzidi kupambana basi tulipiga piga stori pale na bro basi ikabidi nimuage niende magetoni
Basi nikiwa nipo njiani naelekea ghetto nikaona sms imeingia kwenye simu yangu sms ilisomeka ni Fatmah hello mume wangu kwa mapenzi uliyonipa jana na leo nimekuachia zawadi ila ni surprise sikukwambia ipo kwako nenda angalia kitandani kwenye ule mto wa mwekundu utaiona nakupenda,
Sms hiyo ilinishtua sana nikajaribu kumpigia fatmah simu yake haipatikani nikawaza zawadi gani hiyo ikabidi nipige mguu wa haraka kurudi nyumbani huku maswali mengi kichwani nilipofika nyumbani kitu cha kwanza nilipofungua mlango ni kwenda kitandani kuutafuta huo mtu mwekundu kujua kuna nn sikuamini nilipotoa foronya ya mto ndani nilikutana na kitita cha elfu 10 kumi tupu ikabidi nizichukue niziesabu zilikuwa ni shs laki 4 nikashangaa sana ikabidi nijiulize hizi hela zote Fatmah amenipa kwaajili ya nini na kazitoa wapi nikiwa katika wimbi la mawazo nilipigwa na mshangao nilipoona mlio wa simu yangu ikimaanisha kuna sms imekuja ikabidi niusome huo ujumbe alikuwa ni fatmah ujumbe ulionishtua...
Itaendelea usikose sehemu ya 04 kujua nn kiliendelea baada ya kuziona laki 4 nilizopewa na fattmah na je nilipatwa na mshangao gan baada ya kusoma ujumbe ...
MUENDELEZO Soma
Siku niliyokutana na jini kwenye daladala