Salaam, shalom!!
Nitaeleza Kwa ufupi.
Siku Moja mpendwa wetu mmoja alifiwa na ndugu yake Kijiji fulani, tukalazimika kusafiri Toka Kijiji kimoja kwenda Kijiji kingine Kwa ajili ya maziko.
Tulipofika, kilikaa kikao na kuazimia mbuzi wawili wachinjwe Ili ipatikane nyama ya kulika msibani Kwa siku hiyo.
Mbuzi walichinjwa na kuandaliwa vyema muda ya asubuhi, ilipofika mchana, kililetwa chakula na watu wakala mchana na mbuzi alikuwa safi kabisa.
Sasa baada ya kuzika, nyama iliyobaki ilitunzwa Ili iliwe jioni siku hiyo,
Utata ukaja ilipofika jioni saa 12 wakati wa chakula,
Nilipokwenda kwenye pitapita ZANGU kama mmoja wa viongozi wa msafara, nilipata hamaki kubwa kuona yafuatayo,
Nyama Ile ya mbuzi sufuriani ilionekana kubadilika RANGI na kuonekana Kwa RANGI ya Bluu, na ilionekana kuota ukungu na kuwa kama nyama iliyooza na kukaa siku nyingi ni kama mzoga vile.
Nilipoona Yale, niliwaita ndugu nilioongozana nao msibani na kuwaonya kuwa, yule Si mbuzi tuliyekula mchana, niliwambia nyama imebadilishwa, na Si njema Kwa matumizi ya chakula.
Sasa Kwa kuwa wengi wao hawakuwa na macho ya Roho, walirudi kuiangalia nyama na kuiona Iko sawa na wakapuuza ujumbe na maonyo Yale na walikula chakula na nyama Ile jioni Ile.
Kilichofuata baada ya robo sana hivi, umati Ule uligeuka tafrani, tumbo la kuhara liliwashika wote waliokula nyama Ile, watu waliharisha mfululizo na Kwakuwa mazingira ya vijijini hakuna vyoo vya kutosha, uharibifu wa mazingira ulifanyika vichakani,
Watu wale pale kijijini waliokula nyama Ile waliendesha Kwa usiku kucha, na kesho yake, Kila Mmoja alijutia uamuzi mbovu wa kutosikia maonyo ya mtumishi wa Mungu. Baadae ilikuja fahamika kuwa kundi la wachawi mahasimu waliamua kuchukua nyama Ile nzuri wakaila wao na kuleta mzoga Ili kuwakomoa wafiwa Kwa faida zao kichawi.
FUNZO.
1. Makinika na ulaji wa nyama kwenye misiba, wengi hutafutwa kuangamizwa kichawi katika Makusanyiko ya aina Ile.
2. Ombea maji na chakula chochote kabla ya kula Kwa Imani, na ukisita kula usilazimishe.
3. Pata macho ya rohoni Ili uone sawasawa, uepuke hatari mbeleni.
Ikiwa hujampa Yesu maisha Yako, fuatisha Sala hii,
EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN.
Source: Mtumishi wa Mungu ( Jina linahifadhiwa Kwa sababu maalum).