Mfumo wa majimbo una faida kubwa sana kwa sababu unazipa sehemu mbalimbali mamlaka ya kujisimamia, kufanya maamuzi yanayohusu maeneo yao na kupata viongozi wao
Hata hivyo, kuna jambo ambalo tunapaswa kulijua mapema kabisa kwamba mfumo wa majimbo na siasa za kikabila ni vitu ambavyo ni vigumu sana kuvitenganisha/
Nigeria na Kenya ni nchi zenye elimu kubwa sana lakini wameshindwa kabisa kukwepa ukabila kwasababu ya mfumo wa seikali za majimbo. hio ndio maana halisi ukishakubali mfumo huu hutaweza kuukwepa ukabila, Ni lazima ukabila utaongezeka tu !
Kila jimbo litakuwa na mamlaka yake, lakini siasa za kitaifa nikimaanisha Rais, Mawaziri, Senate, Bunge, huko kutaongozwa na makundi yenye kura nyingi ambayo ni makabila makubwa pamoja na makabila ya karibu waliyozoeana.
Kwa Tanzania, hali inaweza kuwa tofauti kwa sababu hatuna makabila mawili au matatu yenye ukubwa unaokaribiana kwa kiasi kikubwa.
Wasukuma ndio kundi kubwa zaidi la kikabila, wakitajwa kuwa karibia asilimia 18
Si hivyo tu wana utani na umoja wa kihistoria na makabila mengine ya kanda ya ziwa, pia ongeza Wagogo, Wanyamwezi, Wafipa, Wanyaturu, n.k. ukitokea uchaguzi hawa watakuwa kitu kimoja kwenye sanduku la kura.
Na jamii hizi wanazaliana kweli kweli, familia moja watu 8 hadi 10,
huwezi kulinganisha na Mnyakyusa, Mchaga. Mhehe, Mngoni Mpare ambae akipata mtoto moja, wawili au kaenda sana watatu kamaliza,
Na kwenye zoezi la kura wanaangalia idadi ya watu hawaangalii utajiri, elimu, n.k. kinachoangaliwa ni idadi ya watu.
Kwa hiyo, tukijenga mfumo wa majimbo bila kuweka utaratibu wa makusudi wa kusawazisha uwakilishi na mgawanyo wa madaraka, tunaweza kujikuta tumeunda mfumo ambao, kwa vitendo, unafanya ukubwa wa kabila na makabila ya karibu kuwa moja ya vigezo muhimu vya nguvu za kisiasa.
HITIMISHO
Mfumo wa majimbo ni mzuri ila bila tahadhari za mapema kabla ya utekelezaji wake, inawezekana kuona faida zake kwenye majimbo pekee lakini mambo yakawa tofauti kabisa kitaifa kwenye urais, Senate na hata Bunge litaendeshwa na makabila makubwa kuliko misingi ya uwakilishi wa kitaifa. Mfano ni kama Kenya, wameelimika sana lakini ukabila umeenea sana kwenye siasa za kitaifa.
Kuna namna huu mfumo tulionao kwa sasa ni mzuri ila tu unahitaji kurekebishwa kuhimiza uwajibikaji, kupunguza kupeana vyeo kwa kujuana kuzidi uwezo na viongozi kuwa na nguvu kupitiliza. Mfumo wa sasa unatoa nafasi kwa usawa hata kwa makabila madogo, Mfumo tulionao ume proove umesaidia kupunguza ukabila, sheria ya nchi inatumika mikoa yote sio kama Kenya au Nigeria kila jimbo na sheria zake, Mfumo wetu wa sasa unachohitaji ni marekebisho ya katiba iliyopendekezwa na Warioba. Watanganyika wawe na nchi yao, Wazanzibar wawe na nchi yao, uwajibikaji uongezeke, Viongozi wapunguziwe nguvu.