Siku tutayothubutu kuingia rasmi mfumo wa Serikali ya Majimbo sioni Rais mwingine zaidi ya Msukuma. Makabila mengine mtasubiri sana

Siku tutayothubutu kuingia rasmi mfumo wa Serikali ya Majimbo sioni Rais mwingine zaidi ya Msukuma. Makabila mengine mtasubiri sana

Kenya hawana mfumo wa majimbo. Wanaita ugatuzi tu, yaani devolution. Inafanana sana na mfumo wa majimbo. Na lengo lake ni kupambana na siasa za ukabila. Nigeria majimbo mengi yalianzishwa wakati wa utawala wa kijeshi. Lengo ni kupambana na nguvu ya siasa za kikabila, hasa kabila la waigbo. Sasa wewe unapata wapi hili la kusema mfumo wa majimbo unaleta siasa za ukabila!!!? Unaambiwa jambo unameza tu bila hata kulitafakari!!
Uite vyovyote ila una kila elements za mfumo wa majimbo na kama lengo ni kupambana na siasa za kikabila mfumo umefeli kabisa, umekuza zaidi ukabila.

Nigeria viongozi wa Hausa Fulani wanasimam hadharani kabisa wanasema utawala wa nchi ni lazima uwe chini yao kwasababu ni kabila lenye watu wengi zaidi, kabila lengine wayoruba na wao wanasema nchi iwe chini yake kwasababu ni kabila la pili kwa ukubwa lenye ukaribu na makabila mengine yenye watu wengi.

Kenya story ni ile ile rais lazima awe Mkikuyu au Mkalejin, Wajaluo ni kabila lililoelimika zaidi Kenya lakini mfumo huu umewaingiza kwenye ukabila, wakiwa chini ya Raila Odinga wamempigia sana kura kikabila kwasababu tu ni mjaluo mwenzao,
 
Nigeria marais wanatoka kila kabila. Tinubu muyoruba, Buhari mfulani nk. Kenya hivyo hivyo. Mfumo wa majimbo unatumika kupambana na si kuleta siasa za ukabila. We wanasiasa wanaongea unayaleta jukwaani.
 
Ndizo faida nilizotaja ambazo zipo upande mmoja wa shilingi wa mfumo wa Serikali ya Majimbo.

Lakini upande wa pili wa shilingi mfumo huo huamua siasa za level ya taifa kwenye ukabila. Rais, Senete, Bunge, Wateule wa Rais, n.k.

Kwa hiyo, unapozungumzia faida za Serikali ya Majimbo katika ngazi ya jimbo kama vile mamlaka zaidi kwa wananchi na maamuzi kufanyika karibu na wananchi ni muhimu pia kujiuliza gharama zake katika ngazi ya taifa.

Ni lazima uwe tayari kukubali kwamba mfumo huo unakuletea mazingira ambayo siasa za kitaifa zitakuwa chini ya makabila yenye idadi kubwa ya watu, au yenye ukaribu na makabila mengine makubwa.

Mfano kwa Kenya mtu akiwa amezaliwa kabila dogo ana nafasi ndogo sana kuja kuwa na chei kikubwa kisiasa, Ni tofauti kabisa na Tanzania.

Hivyo jambo muhimu ni kupima mzani, kila upande una hasara na faida zake.
Ukabila, Udini na Ukanda unatokana na mfumo wa Uchaguzi.

Kama mfumo wa Uchaguzi ukiwa uwakilishi wa Uwiano ukabila hauwezi kuwepo.

Pia tunaweza kuwa na Utaratibu Rais na Waziri mkuu wanachaguliwa na Bunge au kama Uingereza chama chenye viti vingi Ndio kinaunda Serikali
 
Soma vizuri kuhusu types of government.
Mtoa hoja anaongelea mfumo unaoitwa Federal Government, ambao Tanganyika haikuwahi kuwa nao.
Tanganyika, na baadaye Tanzania, haikuwahi kuwa na mfumo wa shirikisho (federal system) ambapo majimbo yangekuwa na serikali na mamlaka zao za kikatiba, kisha majimbo hayo yaungane kuunda Serikali ya Shirikisho.

Hayo unayoyaweka hapo yalikuwa provinces, yaani mgawanyo wa kiutawala wa Tanganyika wakati wa utawala wa kikoloni. Hayakuwa “majimbo” kwa maana ya Federal States.

Kwa mfano, kulikuwa na Central, Eastern, Lake, Northern, Southern, Southern Highlands, Tanga na Western.

Baadaye, mwaka 1962, Provinces zilibadilishwa kuwa Regions (Mikoa).
Kwa hiyo, kuwepo kwa Central, Eastern, Lake, Northern, Southern n.k. hakumaanishi kwamba Tanganyika ilikuwa na Federal Government, bali hayo yalikuwa ni maeneo ya kiutawala yaliyotumiwa na Serikali ya kikoloni kusimamia Tanganyika na serikali huru za majimbo zenye mamlaka ya kikatiba kama ilivyo katika mfumo wa federal.

Kwa kifupi, usichanganye administrative divisions (mgawanyo wa kiutawala) na federal states (majimbo yenye mamlaka ya kikatiba). Tanganyika ilikuwa na mgawanyo wa kiutawala wa provinces, lakini haikuwa Federal Government.
Wewe ndio either hujamuelewa mleta mada au mleta mada hajaelewa Sera ya Chadema kuhusu majimbo.

Federal government ni kitu tofauti kabisa na wanacho zungumza Chadema.

Federal government inawezekana kati ya Tanganyika na Zanzibar ila sio ndani ya Tanganyika.

Chadema wanazungumzia kuhusu ugatuzi/devolution
 
Nigeria marais wanatoka kila kabila. Tinubu muyoruba, Buhari mfulani nk. Kenya hivyo hivyo. Mfumo wa majimbo unatumika kupambana na si kuleta siasa za ukabila. We wanasiasa wanaongea unayaleta jukwaani.
Ume proove niichokuwa nakuambia kwamba Nigeria makabila mawili makuu ndio yameshikilia siasa

Hausa Fulani

Yoruba

KENYA- Kikuyu, Kalenjin

uwezi kukuta kabila dogo linaongoza huko kama kwetu, ni ukabila kwanza
 
Nigeria kuna kabila la Hausa ambao wanaongoza kwa wingi wakifuatiwa na wayoruba lakini kwenye kabila la wahausa sikuhizi linafahamika kama Hausa Fulani

Fulani wamekuwa wakishikilia vyeo vikubwa kwa muda mrefu wakiwemo marais kwa mgongo wa kura za wahausa.

Hao wafulani wachache ila wameji attach kwa strategy kwenye kabila la wahausa, wamefanikiwa kueneza propaganda kuwa wao ni kitu kimoja, wao ndio waliwatawala wahausa kwa miaka mingi sana hivyo walitumia mbinu zao kuforce kuonekana kabila moja

Rais akiwa mfulani jua kwamba kapata kura za wahausa

..bado Hausa ni wengi lakini hawajashika uongozi Nigeria.

..kupata Uraisi kunategemea mambo mengi, lakini muhimu kuliko yote, ni uwepo wa mwanasiasa sahihi ktk muda sahihi.
 
..bado Hausa ni wengi lakini hawajashika uongozi Nigeria.

..kupata Uraisi kunategemea mambo mengi, lakini muhimu kuliko yote, ni uwepo wa mwanasiasa sahihi ktk muda sahihi.
Nigeria kulikuwa na kabila la Hausa lakini sikuhizi wanaitwa Hausa Fulani.

Fulani ni kabila Kupe lililoji Attach kwa wahausa kunufaika na idadi yao kubwa, hao fulani wapo involved sana na mambo ya ugaidi, na pia ni hao hao wamejaa vyeo vikubwa jeshini kwa kisingizio ni wahausa na wanaongea kihausa ila kamwe hawawezi kuacha asili yao.

wamefanikiwa kueneza propaganda kuwa wao ni kitu kimoja, ukienda kwenye miji ya wahausa hadi wabunge ni hao hao wafulani, wanajua sana hii michezo ya kushika power.

Na hawajaanza leo, kihistoria waliwatawala wahausa kwa miaka mingi sana

Rais akiwa mfulani jua kwamba kapata kura za wahausa
 
Wewe ndio either hujamuelewa mleta mada au mleta mada hajaelewa Sera ya Chadema kuhusu majimbo.

Federal government ni kitu tofauti kabisa na wanacho zungumza Chadema.

Federal government inawezekana kati ya Tanganyika na Zanzibar ila sio ndani ya Tanganyika.

Chadema wanazungumzia kuhusu ugatuzi/devolution

..Nadhani kilichotokea Tanganyika mwaka 1962, ni majimbo kugawanywa, halafu yakabadilishwa jina na kuitwa mikoa.

..Chadema tayari wana mfumo wa kanda / majimbo. Na kanda hizo hazijagawanywa kwa kufuata tribal lines. Na mpaka sasa hivi sijasikia changamoto za ukabila zilizosababishwa na mfumo wao.

..Pia uko sahihi ktk hoja yako kwamba kuweka mfumo wa majimbo Tanganyika hakumaanishi kwamba tutakuwa na serikali ya Shirikisho.

..Zaidi maamuzi ya kwamba majimbo / kanda yawe na mamlaka gani hayo yatakuwa ni maamuzi yetu wenyewe. Mamlaka ya majimbo ya Nigeria, ni tofauti ya majimbo ya Ghana, Msumbiji, Kenya, na kwingineko.

..Kama tunaogopa ukabila basi tuwe macho na hila za CCM kurejesha MACHIFU nchini.
 
Nigeria kulikuwa na kabila la Hausa lakini sikuhizi wanaitwa Hausa Fulani.

Fulani ni kabila Kupe lililoji Attach kwa wahausa kunufaika na idadi yao kubwa, hao fulani wapo involved sana na mambo ya ugaidi, na pia ni hao hao wamejaa vyeo vikubwa jeshini kwa kisingizio ni wahausa na wanaongea kihausa ila kamwe hawawezi kuacha asili yao.

wamefanikiwa kueneza propaganda kuwa wao ni kitu kimoja, ukienda kwenye miji ya wahausa hadi wabunge ni hao hao wafulani, wanajua sana hii michezo ya kushika power.

Na hawajaanza leo, kihistoria waliwatawala wahausa kwa miaka mingi sana

Rais akiwa mfulani jua kwamba kapata kura za wahausa

..hujajibu hoja kwamba Hausa ndio wengi lakini hawajatawala.

..Ndio maana nikakwambia Wahausa sio kigezo cha wao kupata madaraka.

..Na Wahausa percentage yao ktk population ya Nigeria ni kubwa sana kuliko jamii yoyote ile ya Tanganyika.

..Tukirudi Tanganyika mikoa tuliyonayo ni majimbo madogo madogo yaliyokuwepo wakati wa ukoloni mpaka 1962.
Sijui kwanini unaunga mkono mikoa huku ukipinga majimbo.
 
1789911414647.png

Huwezi kuelewa bila kujua historia ya wahausa na wafulani

Mhausa ni mfulani na mfulani ni mhausa.

Ingia google au kwenye ai search Hausa Fulani

Hilo ni kabila moja,

Wahausa wameanza kuamka siku hizi wameanza harakati za chini chini kuhoji kama wao ni kabila moja na wafulani kwanini wafulani wana nguvu kuwazidi.
 
Mfumo wa uchaguzi kimajimbo haujumlishi Idadi zote za kura kama huu tulionao, wenyewe unaangalia chama,au mtu ameshinda Jimbo gani then baada ya hapo wanajumlisha Idadi ya majimbo uliyoyashinda.
Mfano,
JIMBO LA KANDA YA ZIWA:
Paskali kura 2,000
Mbogamboga kura 20,000

JIMBO LA PWANI:
Paskali kura 1,000
Mbogamboga kura 6,000,000

JIMBO LA NYANDA ZA JUU KUSINI:
Paskali kura 40,000
Mbogamboga kura 30,000

JIMBO LA KASKAZINI:
Paskali kura 30,000
Mbogamboga kura 25,000

JIMBO LA KANDA YA KATI:
Paskali kura 20,000
Mbogamboga kura 15,000

JIMBO LA KUSINI:
Paskali kura 15,000
Mbogamboga kura 10,000

Kutokana na matokeo ya hapo juu, Paskali ameongoza majimbo 4
Mbogamboga majimbo 2
Hivyo basi, mshindi ni Paskali.
Lakini ukisema mshindi apatikane kwa kujumlisha Idadi ya kura , kura ambazo Mbogamboga wamepigiwa kwenye Jimbo la PWANI tu zingetosha kumgaragaza Paskali.
Samahani inawezekana nikawa sijafuata utaratibu mzuri wa kiuandishi na kusababisha kero kwa atakayesoma.

..Demokrasia yetu ni ya " KURA MOJA MTU MMOJA. "

..Kuunda majimbo au kanda haimaanishi kwamba tunabadili mfumo wetu wa demokrasia na kuufanya usiwe wa " one man one vote. "
 
Ume proove niichokuwa nakuambia kwamba Nigeria makabila mawili makuu ndio yameshikilia siasa

Hausa Fulani

Yoruba

KENYA- Kikuyu, Kalenjin

uwezi kukuta kabila dogo linaongoza huko kama kwetu, ni ukabila kwanza
Kabla ya "majimbo" Kenya imewahi kutoa Rais nje ya Mkikuyu na Mkalenjin?
 
Ume proove niichokuwa nakuambia kwamba Nigeria makabila mawili makuu ndio yameshikilia siasa

Hausa Fulani

Yoruba

KENYA- Kikuyu, Kalenjin

uwezi kukuta kabila dogo linaongoza huko kama kwetu, ni ukabila kwanza
Pia unatakiwa kuelewa kuwa kila nchi ina mgawanyiko wake. Nchi zingine kimakabila na zingine kidini. Nchi yetu mgawanyiko mkubwa ni wa kidini kuliko kikabila. Ndiyo maana unaona Urais unaangaliwa kidini zaidi. Mkatoliki na Muislamu(Sunni). Rais hajatoka bado nje ya hapo.
 
Hv ni kwamba huna kazi ya kufanya mpaka uandike uchafu km huu? Ndiyo maana watu wengi ni maskini akili km hii yako huwezi kufungua ht kioski. Hakuna sensa iliyowahi kuhusisha kabila la mtu hiyo asilimia 18 we umeitoa wapi, we ht taahira atadharau! Halafu ni aibu kujadili ukabila karne hii ya 21, kweli mwafrika uwezo wake ni afadhali ya NYANI.
Anaweza kuwa katumia takwimu za sensa 2022 za kanda ziwa. Mtu mwingine atadai kanda hiyo hawaishi wasukuma pekee, ni sawa lakini kwingineko wasukuma pia wapo na walihesabiwa. Hivyo takwimu za kanda ya ziwa pekee zinaashiria ukweli 99%
 
..asilimia ngapi ya wasukuma wanaishi kanda ya ziwa, na wangapi wako nje.

..watu wanajiaminisha kwamba kushinda Uraisi wa Tz ni lazima ushinde kanda ya ziwa.

..Mimi kwa maoni yangu, ku-dominate kura ktk jiji la Dsm unajiongezea nafasi kuliko kuungwa mkono kanda ya ziwa.

..Nashauri tukaangalie matokeo ya uchaguzi wa 2015 kati ya Magu vs Edo yanaweza kutupatia different pathways za kushinda kura za Uraisi.
 
Hakuna anaekataa Zanzibar ni nchi huru, Zanzibar ni nchi huru kwa 80% haina mambo machache tu.

shida iliyopo ni namna serikali ya muungano ilivyo, vitu vingi vimekuwa vya muungano pasipo kuwepo kwa Nchi na Serikali ya Tanganyika,

Kama Zanzibar wanaweza kuwa na Nchi yao why not Tanganyika ?
Kama Zanzibar wanaweza kuwa na Serikali yao why not Tanganyika ?
Kama muungano ni Tanganyika na Zanzibar, where is Tanganyika ?

Kuna muda unalazimika kuhoji hali ya kiakili aliyokuwa nayo Nyerere wakati anaingia huu muungano,

Solution ni katiba ya Warioba
Orodha mambo matano ya msingi ambayo Mtanganyika anayakosa kwa sababu ya aina ya Muungano tulionao.
 
Hv ni kwamba huna kazi ya kufanya mpaka uandike uchafu km huu? Ndiyo maana watu wengi ni maskini akili km hii yako huwezi kufungua ht kioski. Hakuna sensa iliyowahi kuhusisha kabila la mtu hiyo asilimia 18 we umeitoa wapi, we ht taahira atadharau! Halafu ni aibu kujadili ukabila karne hii ya 21, kweli mwafrika uwezo wake ni afadhali ya NYANI.
Kwani Kenya wapo karne ya 18? Ukabila hukwepeki
 
Pia unatakiwa kuelewa kuwa kila nchi ina mgawanyiko wake. Nchi zingine kimakabila na zingine kidini. Nchi yetu mgawanyiko mkubwa ni wa kidini kuliko kikabila. Ndiyo maana unaona Urais unaangaliwa kidini zaidi. Mkatoliki na Muislamu(Sunni). Rais hajatoka bado nje ya hapo.
Ukabila upo sana ila Nyerere alifanikiwa kucheza nayo
 
Back
Top Bottom