Consigliere
Platinum Member
- Sep 9, 2010
- 12,901
- 27,423
Umeonyesha hofu kama mtu mwingine yeyote aliyedanganywa akavalishwa hofu kwa makusudi, ila kwenye marlezo yako sijaona hoja hata moja ambao angalau imejaribu kushikilia maelezo yako yaliyopwaya au angalau kuishikilia na kuithibitisha hofa yako.Mfumo wa majimbo una faida kubwa sana kwa sababu unazipa sehemu mbalimbali mamlaka ya kujisimamia, kufanya maamuzi yanayohusu maeneo yao, kufaidika na rasilimali zao, kupata viongozi wao, n.k.
Hata hivyo, kuna jambo ambalo tunapaswa kulikubali mapema kabisa kwamba mfumo wa majimbo na siasa za kikabila ni vitu ambavyo ni vigumu sana kuvitenganisha.
Tukikubaliana kuingia kwenye mfumo wa majimbo, ni muhimu pia kuelewa kwamba nguvu za kisiasa zitaanza kujipanga kwa kiasi kikubwa kulingana na ukubwa na ushawishi wa makundi ya kikabila. Kwa hiyo, kama kabila moja lina idadi kubwa zaidi kuliko mengine pamoja na makabila yenye ukaribu nao, uwezekano wa kundi hilo kuwa na ushawishi mkubwa kwenye nafasi za kitaifa utaongezeka.
Kila jimbo litakuwa na mamlaka yake, lakini unapokuja kwenye serikali kuu nikimaanisha Rais (pamoja na wateule wake), Senate, Bunge, idadi na nguvu za makundi makubwa ya watu zitaendelea kuwa na uzito mkubwa.
Tunaona mifano mbalimbali barani Afrika yenye siasa za majimbo ambapo makundi ya kikabila yamekuwa yakihusiana kwa karibu. Nigeria, kwa mfano, ina historia ndefu ya siasa zinazohusisha makundi makubwa ya kikanda na kikabila, Kenya pia imekuwa na siasa ambazo mara nyingi zimehusishwa na nguvu za makundi makubwa ya kikabila.
Kwa Tanzania, changamoto yake inaweza kuwa kubwa zaidi kwa sababu hatuna makabila mawili au matatu yenye ukubwa unaokaribiana kwa kiasi kikubwa.
Wasukuma ndio kundi kubwa zaidi la kikabila, wakitajwa kuwa karibia asilimia 18
Si hivyo tu wana utani na ukaribu wa kihistoria na makabila mengine ya kanda ya ziwa, pia Wagogo, Wanyamwezi, Wafipa, Wanyaturu, n.k. ukitokea uchaguzi hawa watauwa kitu kimoja.
Na jamii hizi wanazaliana kweli kweli, familia moja watu 8,
huwezi kulinganisha na Mnyakyusa, Mchaga. Mhehe, Mngoni Mpare ambae akipata mtoto moja, wawili au kaenda sana watatu kamaliza,
Na kwenye zoezi la kura wanaangalia idadi ya watu hawaangalii utajiri, elimu, n.k. kinachoangaliwa ni idadi ya watu.
Kwa hiyo, tukijenga mfumo wa majimbo bila kuweka utaratibu wa makusudi wa kusawazisha uwakilishi na mgawanyo wa madaraka, tunaweza kujikuta tumeunda mfumo ambao, kwa vitendo, unafanya ukubwa wa kabila na makabila ya karibu kuwa moja ya vigezo muhimu vya nguvu za kisiasa.
HITIMISHO
Mfumo wa majimbo ni mzuri ila bila tahadhari za mapema kabla ya utekelezaji wake, inawezekana kuona faida zake kwenye majimbo pekee lakini mambo yakawa tofauti kabisa kitaifa kwenye urais, Senate na hata Bunge litaendeshwa na makundi makubwa ya kikabila kuliko misingi ya uwakilishi wa kitaifa. Mfano ni kama Kenya wala sio mbali.
Kuna namna huu mfumo tulionao kwa sasa ni mzuri ila tu unahitaji kurekebishwa kuhimiza uwajibikaji, kupunguza kupeana vyeo kwa kujuana kuzidi uwezo na viongozi kuwa na nguvu kupitiliza. Mfumo huu mtu mwenye cheo kikubwa anaweza kutokea kabila lolote bila kujali ukubwa wake, Mfumo wetu umeweza sana kupunguza mambo ya kikabila kwa kiasi chake sheria ya nchi ni mikoa yote sio kama Kenya au Nigeria kila jimbo na sheria zake, Mfumo wetu wa sasa unachohitaji ni marekebisho ya katiba iliyopendekezwa na Warioba. Watanganyika wawe na nchi yao, Wazanzibar wawe na nchi yao, uwajibikaji uongezeke, Viongozi wapunguziwe nguvu.
Labda nikuulize, wewe umeelewa ulichokisndika? Au umeelewa kimoyomoyo?