Mfumo wa majimbo na ukabila ni vitu visivyoweza kutenganishwa, ni ulimi na menoUkabila huu
Mfumo wa majimbo ni mzuri tu ila kuwe na tahadhari kwa sababu bila safeguards za wazi, inawezekana kabisa kuona urais, Senate na hata Bunge vikianza kuakisi zaidi nguvu za makundi makubwa ya kikabila kuliko misingi ya uwakilishi wa kitaifa.Ndio maana nasema ccm wakazie hapo hapo maana nchi hii wananchi wenyewe ni wakabila, wadini, wakanda nk kwa kifupi wananchi ni madikteta wa kuzaliwa haina haja na haiwezekani kuwa na demokrasia halisia tz zaidi ya vurugu
Kama ni hivyo usemavyo basi sio nzuriMfumo wa majimbo ni mzuri tu ila kuwe na tahadhari kwa sababu bila safeguards za wazi, inawezekana kabisa kuona urais, Senate na hata Bunge vikianza kuakisi zaidi nguvu za makundi makubwa ya kikabila kuliko misingi ya uwakilishi wa kitaifa.
Kuna namna huu mfumo tulionao ni mzuri tu ila tu ulichokosa ni uwajibikaji, kupeana vyeo kwa kujuana na viongozi kuwa na nguvu kupitilizaKama ni hivyo usemavyo basi sio nzuri
Kama ni hivyo usemavyo basi sio mzuriMfumo wa majimbo ni mzuri tu ila kuwe na tahadhari kwa sababu bila safeguards za wazi, inawezekana kabisa kuona urais, Senate na hata Bunge vikianza kuakisi zaidi nguvu za makundi makubwa ya kikabila kuliko misingi ya uwakilishi wa kitaifa.
Ndio nikakwambia kuliko tuwe na mfumo wa kikabila ni bora tu tubaki na huu huu wa kiccm unatoshaKuna namna huu mfumo tulionao ni mzuri tu ila tu ulichokosa ni uwajibikaji, kupeana vyeo kwa kujuana na viongozi kuwa na nguvu kupitiliza
Tanzania mtu mwenye cheo kikubwa anaweza kutokea kabila lolote bila kujali ukubwa wake
Ila kukiwa na mfumo wa majimbo, hata mgawanyo wa vyeo vikubwa unaweza kuanza kupangwa mapema kwenye kampeni kwa kuangalia ukubwa na ushawishi wa makabila yenye ukaribu na kabila kubwa analotoka Rais. Makabila makubwa ya karibu yenye uwezo wa kuleta kura nyingi yanapewa ahadi wanaempigia kura akishinda watapata uongozi wa idara flani kwenye teuzi, makabila madogo huwa yanasahaulika kwenye vyeo, kura zao chache hata wakipiga,
Shida ni kwamba kadri siku zinavyokwenda, imani ya wananchi kwa CCM inaweza kuendelea kupungua. Huenda isiwe leo wala kesho, lakini kama CCM itaendelea kwenda kinyume na matarajio na matakwa ya wananchi, kuna siku inaweza kupoteza nafasi yake na kubadilishwa na chama kingine.Kama ni hivyo usemavyo basi sio mzuri
Ndio nikakwambia kuliko tuwe na mfumo wa kikabila ni bora tu tubaki na huu huu wa kiccm unatosha
Maoni Yako na yaheshimiwe!!Mfumo wa majimbo una faida kubwa sana kwa sababu unazipa sehemu mbalimbali mamlaka ya kujisimamia, kufanya maamuzi yanayohusu maeneo yao, kufaidika na rasilimali zao, kupata viongozi wao, n.k.
Hata hivyo, kuna jambo ambalo tunapaswa kulikubali mapema kabisa kwamba mfumo wa majimbo na siasa za kikabila ni vitu ambavyo ni vigumu sana kuvitenganisha.
Tukikubaliana kuingia kwenye mfumo wa majimbo, ni muhimu pia kuelewa kwamba nguvu za kisiasa zitaanza kujipanga kwa kiasi kikubwa kulingana na ukubwa na ushawishi wa makundi ya kikabila. Kwa hiyo, kama kabila moja lina idadi kubwa zaidi kuliko mengine pamoja na makabila yenye ukaribu nao, uwezekano wa kundi hilo kuwa na ushawishi mkubwa kwenye nafasi za kitaifa utaongezeka.
Kila jimbo litakuwa na mamlaka yake, lakini unapokuja kwenye serikali kuu nikimaanisha Rais (pamoja na wateule wake), Senate, Bunge, idadi na nguvu za makundi makubwa ya watu zitaendelea kuwa na uzito mkubwa.
Tunaona mifano mbalimbali barani Afrika yenye siasa za majimbo ambapo makundi ya kikabila yamekuwa yakihusiana kwa karibu. Nigeria, kwa mfano, ina historia ndefu ya siasa zinazohusisha makundi makubwa ya kikanda na kikabila, Kenya pia imekuwa na siasa ambazo mara nyingi zimehusishwa na nguvu za makundi makubwa ya kikabila.
Kwa Tanzania, changamoto yake inaweza kuwa kubwa zaidi kwa sababu hatuna makabila mawili au matatu yenye ukubwa unaokaribiana kwa kiasi kikubwa.
Wasukuma ndio kundi kubwa zaidi la kikabila, wakitajwa kuwa karibia asilimia 18
Si hivyo tu wana utani na ukaribu wa kihistoria na makabila mengine ya kanda ya ziwa, pia Wagogo, Wanyamwezi, Wafipa, Wanyaturu, n.k. ukitokea uchaguzi hawa watauwa kitu kimoja.
Na jamii hizi wanazaliana kweli kweli, familia moja watu 8,
huwezi kulinganisha na Mnyakyusa, Mchaga. Mhehe, Mngoni Mpare ambae akipata mtoto moja, wawili au kaenda sana watatu kamaliza,
Na kwenye zoezi la kura wanaangalia idadi ya watu hawaangalii utajiri, elimu, n.k. kinachoangaliwa ni idadi ya watu.
Kwa hiyo, tukijenga mfumo wa majimbo bila kuweka utaratibu wa makusudi wa kusawazisha uwakilishi na mgawanyo wa madaraka, tunaweza kujikuta tumeunda mfumo ambao, kwa vitendo, unafanya ukubwa wa kabila na makabila ya karibu kuwa moja ya vigezo muhimu vya nguvu za kisiasa.
Kitu kinachonipa shida mimi sio katiba bali ni wasimamizi wa katiba, nchi hii watu wake ni madikteta wa asili hata uweke mifumo vipi bado hawapo tayari kuisimamia hiyo mifumo kwani siku zote mifumo haijisimamii yenyeweShida ni kwamba kadri siku zinavyokwenda, imani ya wananchi kwa CCM inaweza kuendelea kupungua. Huenda isiwe leo wala kesho, lakini kama CCM itaendelea kwenda kinyume na matarajio na matakwa ya wananchi, kuna siku inaweza kupoteza nafasi yake na kubadilishwa na chama kingine.
Katiba ya Warioba inaweza kupunguza hasira nyingi za wananchi na uzuri wa katiba bado itaendelea kutumia mfumo wa mikoa sio majimbo.
Katiba haiwezi kutatua kila kitu ila kutakuwa na nafuuKitu kinachonipa shida mimi sio katiba bali ni wasimamizi wa katiba, nchi hii watu wake ni madikteta wa asili hata uweke mifumo vipi bado hawapo tayari kuisimamia hiyo mifumo kwani siku zote mifumo haijisimamii yenyewe
Tumelelewa katika familia ya baba ndio kichwa cha familia na hapingwi basi hata siasa zetu regardless katiba ndio hivyo hivyo
Sasa ikija kutokea hiyo ya makabila kushika hatamu na ku-priotize ukabila ndio kabisaa tutakuwa pabaya kama nchi kwani kuna makabila kwa udikteta ni kama pipa na mfuniko
Zanzibar ni Nchi na huu ndio ukweli ambao wengi wetu hatutaki kuukubaliKatiba haiwezi kutatua kila kitu ila kutakuwa na nafuu
Mfano Zanzibar ina hadhi ya serikali ya majimbo ndani ya Tanzania.
Wazanzibar wana nchi yao na wanachagua rais wao kama vile serikali ya majimbo wanavyochagua governor, Zanzibar wanaruhusiwa kuwa na sheria zao kama jimbo linavyoweza kufanya, Zanzibar wanataasisi zao, n.k.
Ni kitu ambacho kimekuwa kikitugawa sana, upande moja tupo serikali ya mikoa, upande mwengine unapewa hadhi ya kuwa serikali ya majimbo.
Katiba ya Warioba itatatua hili tatizo kwa kiasi kikubwa sana na kuongeza umoja, Kila mtu awe na nchi yake Tanganyika na Zanzibar.
Haiwezekani Tanzania Bara kuwe na serikali ya mikoa lakini upande mwengine unaruhusiwa kuwa na hadhi ya serikali ya majimbo
Hakuna anaekataa Zanzibar ni nchi huru, Zanzibar ni nchi huru kwa 80% haina mambo machache tu.Zanzibar ni Nchi na huu ndio ukweli ambao wengi wetu hatutaki kuukubali
Zenji ni nchi iliyoungana na Tanganyika kipindi hicho kwahiyo muungano haifanyi nchi kupoteza mamlaka yake
Ni jambo la bahati mbaya ikatokea kutokuukubali ukweli huu kwa waasisi wa taifa la Tanganyika na kutaka kuimeza Zanzibar ndio kumetufikisha hapa
Hivyo basi kuiweka Zenji kama mfano wa majimbo naona haisound fresh maana ni kama umeiweka katika upande wa ukanda na sio nchi
Hii ni hitilafu iliyofanywa na waasisi wa upande wa Tanganyika kwa kuukataa ukweli kuwa Zanzibar ni nchivingi vimekuwa vya muungano pasipo kuwepo kwa Nchi na Serikali ya Tanganyika,
Faida zitaonekana kwenye majimbo tu lakini taifa litagawanyika zaidi kwa ukabilaWewe haujachoka tu kuongozwa na akili za watu wakuamulie usiyoyataka na usiyoyataka kabisa?maana kuna mengine wanaamua unaona sawa tu muhimu hawajakuuwa but kuna mengine unaona kabisa hawa wamezidi.
Mimi natamani leo kesho tuingie free mode yaani kila mtu na akili zake alimradi asivunje sheria tu.