Siku tutayothubutu kuingia rasmi mfumo wa Serikali ya Majimbo sioni Rais mwingine zaidi ya Msukuma. Makabila mengine mtasubiri sana

Uite vyovyote ila una kila elements za mfumo wa majimbo na kama lengo ni kupambana na siasa za kikabila mfumo umefeli kabisa, umekuza zaidi ukabila.

Nigeria viongozi wa Hausa Fulani wanasimam hadharani kabisa wanasema utawala wa nchi ni lazima uwe chini yao kwasababu ni kabila lenye watu wengi zaidi, kabila lengine wayoruba na wao wanasema nchi iwe chini yake kwasababu ni kabila la pili kwa ukubwa lenye ukaribu na makabila mengine yenye watu wengi.

Kenya story ni ile ile rais lazima awe Mkikuyu au Mkalejin, Wajaluo ni kabila lililoelimika zaidi Kenya lakini mfumo huu umewaingiza kwenye ukabila, wakiwa chini ya Raila Odinga wamempigia sana kura kikabila kwasababu tu ni mjaluo mwenzao,
 
Nigeria marais wanatoka kila kabila. Tinubu muyoruba, Buhari mfulani nk. Kenya hivyo hivyo. Mfumo wa majimbo unatumika kupambana na si kuleta siasa za ukabila. We wanasiasa wanaongea unayaleta jukwaani.
 
Ukabila, Udini na Ukanda unatokana na mfumo wa Uchaguzi.

Kama mfumo wa Uchaguzi ukiwa uwakilishi wa Uwiano ukabila hauwezi kuwepo.

Pia tunaweza kuwa na Utaratibu Rais na Waziri mkuu wanachaguliwa na Bunge au kama Uingereza chama chenye viti vingi Ndio kinaunda Serikali
 
Wewe ndio either hujamuelewa mleta mada au mleta mada hajaelewa Sera ya Chadema kuhusu majimbo.

Federal government ni kitu tofauti kabisa na wanacho zungumza Chadema.

Federal government inawezekana kati ya Tanganyika na Zanzibar ila sio ndani ya Tanganyika.

Chadema wanazungumzia kuhusu ugatuzi/devolution
 
Nigeria marais wanatoka kila kabila. Tinubu muyoruba, Buhari mfulani nk. Kenya hivyo hivyo. Mfumo wa majimbo unatumika kupambana na si kuleta siasa za ukabila. We wanasiasa wanaongea unayaleta jukwaani.
Ume proove niichokuwa nakuambia kwamba Nigeria makabila mawili makuu ndio yameshikilia siasa

Hausa Fulani

Yoruba

KENYA- Kikuyu, Kalenjin

uwezi kukuta kabila dogo linaongoza huko kama kwetu, ni ukabila kwanza
 

..bado Hausa ni wengi lakini hawajashika uongozi Nigeria.

..kupata Uraisi kunategemea mambo mengi, lakini muhimu kuliko yote, ni uwepo wa mwanasiasa sahihi ktk muda sahihi.
 
..bado Hausa ni wengi lakini hawajashika uongozi Nigeria.

..kupata Uraisi kunategemea mambo mengi, lakini muhimu kuliko yote, ni uwepo wa mwanasiasa sahihi ktk muda sahihi.
Nigeria kulikuwa na kabila la Hausa lakini sikuhizi wanaitwa Hausa Fulani.

Fulani ni kabila Kupe lililoji Attach kwa wahausa kunufaika na idadi yao kubwa, hao fulani wapo involved sana na mambo ya ugaidi, na pia ni hao hao wamejaa vyeo vikubwa jeshini kwa kisingizio ni wahausa na wanaongea kihausa ila kamwe hawawezi kuacha asili yao.

wamefanikiwa kueneza propaganda kuwa wao ni kitu kimoja, ukienda kwenye miji ya wahausa hadi wabunge ni hao hao wafulani, wanajua sana hii michezo ya kushika power.

Na hawajaanza leo, kihistoria waliwatawala wahausa kwa miaka mingi sana

Rais akiwa mfulani jua kwamba kapata kura za wahausa
 

..Nadhani kilichotokea Tanganyika mwaka 1962, ni majimbo kugawanywa, halafu yakabadilishwa jina na kuitwa mikoa.

..Chadema tayari wana mfumo wa kanda / majimbo. Na kanda hizo hazijagawanywa kwa kufuata tribal lines. Na mpaka sasa hivi sijasikia changamoto za ukabila zilizosababishwa na mfumo wao.

..Pia uko sahihi ktk hoja yako kwamba kuweka mfumo wa majimbo Tanganyika hakumaanishi kwamba tutakuwa na serikali ya Shirikisho.

..Zaidi maamuzi ya kwamba majimbo / kanda yawe na mamlaka gani hayo yatakuwa ni maamuzi yetu wenyewe. Mamlaka ya majimbo ya Nigeria, ni tofauti ya majimbo ya Ghana, Msumbiji, Kenya, na kwingineko.

..Kama tunaogopa ukabila basi tuwe macho na hila za CCM kurejesha MACHIFU nchini.
 

..hujajibu hoja kwamba Hausa ndio wengi lakini hawajatawala.

..Ndio maana nikakwambia Wahausa sio kigezo cha wao kupata madaraka.

..Na Wahausa percentage yao ktk population ya Nigeria ni kubwa sana kuliko jamii yoyote ile ya Tanganyika.

..Tukirudi Tanganyika mikoa tuliyonayo ni majimbo madogo madogo yaliyokuwepo wakati wa ukoloni mpaka 1962.
Sijui kwanini unaunga mkono mikoa huku ukipinga majimbo.
 


Huwezi kuelewa bila kujua historia ya wahausa na wafulani

Mhausa ni mfulani na mfulani ni mhausa.

Ingia google au kwenye ai search Hausa Fulani

Hilo ni kabila moja,

Wahausa wameanza kuamka siku hizi wameanza harakati za chini chini kuhoji kama wao ni kabila moja na wafulani kwanini wafulani wana nguvu kuwazidi.
 

..Demokrasia yetu ni ya " KURA MOJA MTU MMOJA. "

..Kuunda majimbo au kanda haimaanishi kwamba tunabadili mfumo wetu wa demokrasia na kuufanya usiwe wa " one man one vote. "
 
Ume proove niichokuwa nakuambia kwamba Nigeria makabila mawili makuu ndio yameshikilia siasa

Hausa Fulani

Yoruba

KENYA- Kikuyu, Kalenjin

uwezi kukuta kabila dogo linaongoza huko kama kwetu, ni ukabila kwanza
Kabla ya "majimbo" Kenya imewahi kutoa Rais nje ya Mkikuyu na Mkalenjin?
 
Ume proove niichokuwa nakuambia kwamba Nigeria makabila mawili makuu ndio yameshikilia siasa

Hausa Fulani

Yoruba

KENYA- Kikuyu, Kalenjin

uwezi kukuta kabila dogo linaongoza huko kama kwetu, ni ukabila kwanza
Pia unatakiwa kuelewa kuwa kila nchi ina mgawanyiko wake. Nchi zingine kimakabila na zingine kidini. Nchi yetu mgawanyiko mkubwa ni wa kidini kuliko kikabila. Ndiyo maana unaona Urais unaangaliwa kidini zaidi. Mkatoliki na Muislamu(Sunni). Rais hajatoka bado nje ya hapo.
 
Anaweza kuwa katumia takwimu za sensa 2022 za kanda ziwa. Mtu mwingine atadai kanda hiyo hawaishi wasukuma pekee, ni sawa lakini kwingineko wasukuma pia wapo na walihesabiwa. Hivyo takwimu za kanda ya ziwa pekee zinaashiria ukweli 99%
 
Anaweza kuwa katumia takwimu za sensa 2022 za kanda ziwa. Mtu mwingine atadai kanda hiyo hawaishi wasukuma pekee, ni sawa lakini kwingineko wasukuma pia wapo na walihesabiwa. Hivyo takwimu za kanda ya ziwa pekee zinaashiria ukweli 99%

..asilimia ngapi ya wasukuma wanaishi kanda ya ziwa, na wangapi wako nje.

..watu wanajiaminisha kwamba kushinda Uraisi wa Tz ni lazima ushinde kanda ya ziwa.

..Mimi kwa maoni yangu, ku-dominate kura ktk jiji la Dsm unajiongezea nafasi kuliko kuungwa mkono kanda ya ziwa.

..Nashauri tukaangalie matokeo ya uchaguzi wa 2015 kati ya Magu vs Edo yanaweza kutupatia different pathways za kushinda kura za Uraisi.
 
Orodha mambo matano ya msingi ambayo Mtanganyika anayakosa kwa sababu ya aina ya Muungano tulionao.
 
Kwani Kenya wapo karne ya 18? Ukabila hukwepeki
 
Ukabila upo sana ila Nyerere alifanikiwa kucheza nayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…