Siku Ukijua Kinachokutokea Usiku, Akili Yako Itaruka!

Natamani sana itokee walau siku moja nione au nishuhudie hii kitu kama ni kweli yapo hayo uliyoandika na kutuita eti tuna kiherehere.
 
Mbona hiyo ni Sleep paralysis mkuu?
 
Mbona hawapo? Nitajiungaje na watu/viumbe wasiokuwepo?
 
Kuna dawa ukipaka usoni mara tatu kwa kunuia, utaona jinsi vitu vilivyo. Unavyoviona sivyo vilivyo. Amini usiamini.Ila usiitumie hiyo dawa kwani utakosana na kila mtu.
 
Mwehu amevamia jukwaa, mtu mwenye akili timamu hawezi kuandika huu uchafu, vilevile inawezekana we ni mchawi
 
Zaburi 91:5-6 β€” β€œHutaogopa hofu ya usiku, wala mshale urukao mchana; wala tauni ipitayo gizani, wala uharibifu uangamizao adhuhuri.”
Zaburi 121:3-4 β€” β€œHatakuruhusu mguu wako usogee; yeye akulindaye hatasinzia. Tazama, yeye akulindaye Israeli hasinzii wala halali.”
Zaburi 4:8 β€” β€œKwa amani nitajilaza na kulala usingizi; maana Wewe, BWANA, ndiwe unayenifanya nikae salama.”
Mithali 3:24 β€” β€œUtakapolala hutaogopa; naam, utalala, na usingizi wako utakuwa mtamu.”
Zaburi 91:11 β€” β€œKwa kuwa atawaamuru malaika zake wakulinde katika njia zako zote.”
Zaburi 127:2 β€” β€œ...maana humpa mpendwa wake usingizi.”
Kwa maombi ya kabla ya kulala, Zaburi 91 ni sura nzuri sana ya kusoma na kumkabidhi Mungu wewe, familia yako, nyumba yako na mifugo yako. Mungu akulinde usiku huu na akupe amani na usingizi salama. πŸ™
 
Mfumo tuliokuwa nao ,ni mfumo bora kabisa ,yaani haujui kitu hata siku yako ya kifa so unakuwa happy ,hayo mengine bora tumefichwa .. Fikiria tu hili la mtu anakuchukia ila anakuchekea na wewe unaishi naye fresh tu ,kama ingekuwa tunajua ingekwua balaa zaidi.

Tungekuwa na maadui wengi zaidi hata kukosa watu wa kuongea nao ,tungeishi kwa wasiwasi sana ; assume mtu anajua umebakiza hata mwaka ili ufe ,utakosa furaha sana .
 
Unajua watu tunaowaita mabaharia wengi akili ziko faster na wako poa sana , ni watu wa kupiga hustlers na kupeana matumaini ya good life,wewe mbona kama mchawi , kutishana na kukata tamaa ya maisha , badilisha jina
 
Kuna dawa ukipaka usoni mara tatu kwa kunuia, utaona jinsi vitu vilivyo. Unavyoviona sivyo vilivyo. Amini usiamini.Ila usiitumie hiyo dawa kwani utakosana na kila mtu.
πŸ˜…πŸ˜… Binadamu tunaishi kwa uongo ,yaani ile una miaka 40 na kuendelea ,unakuja kuona hayo mambo ya nyuma ya pazi ,basi unajiona miaka ya nyuma yote ulikuwa unaishi katika uongo mkubwaπŸ˜…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…