Siku ukipata nafasi ya kuishi russia utaichukia sana

ward41

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2022
Posts
749
Reaction score
2,533
Wazungu kwa ujumla ni wabaguzi sana. Ukienda Europe, America ubaguzi ni kawaida sana.

Ila kuna maeneo ubaguzi umezidi sana hasa kwetu Sisi watu weusi. Russia ni miongoni mwa nchi ambazo ubaguzi umekithiri sana. Watu weusi Sisi ni takataka nchini Russia. Watu weusi wanabaguliwa sana Russia na nchi za eastern Europe
Ni tofauti kidogo na western Europe na USA
Western Europe na USA pamoja na chuki zote, lakini kuna unafuu sana. Wao kidogo wana Ustarabu.
Nashangaa sana mu Africa kuichukia USA na ulaya magharibi na kuipenda Russia.
Ndugu zanguni Russia ni nchi ya kishenzi sana. Russia ni nchi ya kibaguzi sana.
 
Umewai golini Mpira umeuacha nyuma,Umepiga kiguu na njia mpaka Russia,CCM hukuiona.
Screenshot_20230901-182500.png
Screenshot_20230908-180255.png
 
Wazungu kwa ujumla ni wabaguzi sana. Ukienda Europe, America ubaguzi ni kawaida sana.

Ila kuna maeneo ubaguzi umezidi sana hasa kwetu Sisi watu weusi. Russia ni miongoni mwa nchi ambazo ubaguzi umekithiri sana. Watu weusi Sisi ni takataka nchini Russia. Watu weusi wanabaguliwa sana Russia na nchi za eastern Europe
Ni tofauti kidogo na western Europe na USA
Western Europe na USA pamoja na chuki zote, lakini kuna unafuu sana. Wao kidogo wana Ustarabu.
Nashangaa sana mu Africa kuichukia USA na ulaya magharibi na kuipenda Russia.
Ndugu zanguni Russia ni nchi ya kishenzi sana. Russia ni nchi ya kibaguzi sana.
Hakuna cha ajabu hapo. Ubaguzi ni hulka ya binadamu wote.

Kama ccm tu inawabagua wapinzani! Sembuse hao Warusi kuwabagua Waafrika!!
 
Sio kweli mkuu

Me niko hapa miyomboni
Tunabonga na kula pis zao fresh tu
We unasema russia gan?

Au unamaanisha kwa putin?
 
Umewahi ishi Russia au unatuletea hadthi za kusadikika?!! Je, unafikiri nchi zote za Africa Ni adui wa wamagharibi na rafiki wa Russia? Kuna chi Ni marafiki wa urusi na maadui wa marekani, vivyo kuna nchi Ni marafiki wa wamagharibi. Usipende hizo haste generalization
 
Hata mimi ningezaliwa mzungu obviously ningewachukia watu weusi, haiwezekani watu weusi walio huru wanaenda kuomba msaada wa mbolea na nafaka kwenye nchi ya watu weupe walio vitani, hao watu weusi ningeamini wamelaaniwa na hairuhusiwi kuwa karibu nao kwa sababu watakuambukiza laana yao
 
Ungekuww karibu nikupongeze na kikombe cha mbege.
Siku watu wakiweza kuchagua viongozi watakaowaajibisha,mambo yataenda sawa.
Kwa sasa,kila mmoja ana formula zake na familia yake.
 
Hata wewe ukienda kulelewa kwa shangazi yako hawezi kukupenda wewe kuliko watoto wake na watoto wake hawatakutazama kama mwenzao kwa asilimia 100
 
Hii haitobadilisha chochote juu ya ile SMO,, magaidi wa west lazima watimulie popote duniani watakapoleta chokochoko.
Cc. Hamas, hizbollah, houthi, putin, kiduku, xi jing pi, bila kusahau taifa teule iran
 
Wazungu kwa ujumla ni wabaguzi sana. Ukienda Europe, America ubaguzi ni kawaida sana.

Ila kuna maeneo ubaguzi umezidi sana hasa kwetu Sisi watu weusi. Russia ni miongoni mwa nchi ambazo ubaguzi umekithiri sana. Watu weusi Sisi ni takataka nchini Russia. Watu weusi wanabaguliwa sana Russia na nchi za eastern Europe
Ni tofauti kidogo na western Europe na USA
Western Europe na USA pamoja na chuki zote, lakini kuna unafuu sana. Wao kidogo wana Ustarabu.
Nashangaa sana mu Africa kuichukia USA na ulaya magharibi na kuipenda Russia.
Ndugu zanguni Russia ni nchi ya kishenzi sana. Russia ni nchi ya kibaguzi sana.
Binafsi mi sijaishi Russia lakin naelewa siyo nchi ya kuishobokea hata kidogo Kama we ni mwafrika,wanabagua waafrika hujawai ona ikiwemo ujerumani,lakin kwa upande wa USA,Canada na ungereza utabaguliwa lakin siyo ivyo,lakin itashangaa watu wanaishobokea miradi mingap APA bongo imefadhiliwa imepigwa lebo ya united states ni kibao lakin tafuta ya Russia
 
Wacha tubaguliwe tu ****@&ke zetu. Kama viongozi wetu hata kumaliza migogoro ya wafugaji na wakulima wameshindwa halafu ndo usibaguliwe? Mjomba PUTIN kanyaga twende hawa mashoga mpaka wakose mabasha safari hii
 
Binafsi mi sijaishi Russia lakin naelewa siyo nchi ya kuishobokea hata kidogo Kama we ni mwafrika,wanabagua waafrika hujawai ona ikiwemo ujerumani,lakin kwa upande wa USA,Canada na ungereza utabaguliwa lakin siyo ivyo,lakin itashangaa watu wanaishobokea miradi mingap APA bongo imefadhiliwa imepigwa lebo ya united states ni kibao lakin tafuta ya Russia
Hivi chuo cha pale mbeya Iyunga(MTC) siku hizi MUST kilijengwa na USA sio?
 
Kuna vitu mnakutana navyo ninyi mnao safiri huko kwa watu weupe lakini sisi tusio safiri tuna sababu zetu tofauti tofauti.

Binafsi sifurahishwi na tabia ya west kuinyonya nchi zingine, kuipangia nini cha kufanya, kulazimisha ajenda zao zitekelezwe kwenye nchi zingine, Kuyalinda maslahi yao ya kiuchumi kwa kuwadhurumu wengine na hata mauaji, ubabe n.k
Nchi za west kama zote zingekuwa kama canada, uhispania au uswisi basi hizi chuki zingepungua sana.

Kwa vyovyote vile watu walioumizwa na nchi hizi za west lazima wataziunga mkono zile nchi kinzani na west
 
Linapokuja suala la ubaguzi dhidi ya watu weusi basi Russia, China, India na waarabu ni wabaya kuliko wengine wote, wao wanajua mtu mweusi ni nyani tu wa kurushiwa ndizi.
 
Je, umewahi kuishi Russia. Uliishi miaka ipi ambapo ubaguzi ulikuwa wa kiwango kikubwa?
Uliishi mji gani?

Miaka hiyo tuligoma kwenda chuo for a week baada ya raia wa Mongolia kuuwawa na skinheads baada ya kumaliza degree yake ya udaktari.
Niliwahi kukimbizwa na skinheads mji wa Saint Petersburg, hadi nafika kwenye subway niko hoi.
Baada ya tukio la kuuwawa kwa jamaa sikuwahi kusikia tena coz Putin stood firm against racism.
 
Back
Top Bottom