Siku utakayofanikiwa mambo yatakuwa hivi kwa sehemu kubwa

Huu ndio ukweli,hakuna haja ya kuhangaika Ili watu wakutambue nk..

Kuna jamaa huwa napenda kumnanga,namwambia aisee ukiwa na gari wadada wanapenda Sana unajilia kiulaini,sasa yeye analo tena anayo matatu ila sasa anasema hajawahi pata mwanamke Kwa kutegemea gari lake kiasi kwamba anachukua Sana [emoji3][emoji3][emoji3]

Ni hivi kitu huwa cha maana usipokuwa nacho,pili kuhangaika Ili eti watu wakutambue au ukipata kitu fulani kudhani ndio sijui itabadilisha madhila yako ni uongo..

Just be simple wala haihitaji nguvu nyiingi wala kujiumiza Ili upate,kwa sababu ukipata haitakuwa ulivyotarajia na so utaanza kukosa raha ndani Kwa ndani..

Ila yote kwa yote Bora ufanikiwe upate heshima ya ku fake kuliko kuwa maskini uje kufedheheka.
Mkuu kufedheheka ni just perception ya mtu.
 
Ndio maana wengi wa watawala wetu wakishaondoka madarakani huishia kujutia tu waliyotufanyia pindi wakiwa na mamlaka.
 
[emoji3][emoji3][emoji3]

Sasa hunipendi kwani unanijua?

Nashukuru Sana Mkuu!
Sikujui lakini maandiko yako ndiyo huwa yanafanya nikuchukie. Ila hili la leo dah ningekuwa karibu na wewe ningekupa offer ya kula au kunywa chochote.
 
Mimi siku nyingi nasema ukweli, Jambo Hilo hufanya wasioupenda huo ukweli kunichukia.

Hata hivyo najua nikifanyacho.
 
Mkuu kufedheheka ni just perception ya mtu.
Kwa hiyo uko Mzee unahangaika na kuomba Kazi ndogo ndogo au unaomba omba sio fedheha ni nini? Acha masihara mkuu..

Pili kama hujawa Mzee huwa unaona watu Wana struggle kupata basic needs ,wanaishi sehemu ambazo sio decent nk
 
Kwema Wakuu!

Siku utakayofanikiwa Wale uliodhani utawakomesha, utawaringishia wengi wao watakuwa hawapo, watakuwa wamekufa!

Siku utakapofanikiwa wengi WA watu uliokuwa unawaonea aibu na kuwahofia watakudharau usifanye kazi fulani watakuwa wamekufa, au utagundua hakuna aliyekuwa anafuatilia maisha yako. Hapo ndipo utajiona ulikuwa mjinga.

Siku utapofanikiwa wengi uliokuwa unawapenda Sana ukasema siku ukifanikiwa kimaisha utawafurahisha, wengi wao watakuwa hawapo, watakuwa wamekufa. Na hapo ndipo utaelewa kuwa unaweza kumfurahisha mtu hata Kwa kidogo ulichonacho sasa.

Hapo utayaona mafanikio hayana maana yoyote Ile Kwa sehemu kubwa.

Siku utakayofanikiwa ndio siku kila mtu utamuona amefanikiwa wewe ndio ulikuwa WA mwisho. Hiyo ni kutokana na kuwa kila mtu utamtazama katika jicho la kufanikiwa. Hapo utajua kuwa kumbe wakati mwingine mafanikio ni mtazamo wa mtu tuu.
Wakati sasa hivi unajiona huna Raha na unamaisha magumu lakini siku ukifanikiwa utawaona watu wenye maisha Kama yako ya zamani wakiishi Kwa Raha. Na hapo utagundua maisha ni kuridhika.

Siku ukifanikiwa wengi uliodhani watakuheshimu na kukutukuza utawaona Kama wanakuchukulia kawaida. Hawakuheshimu. Hapo wengi hujikuta wakilazimisha kuheshimiwa Jambo ambalo sio Sawa. Na hapo utajifunza kuwa kuheshimiwa ni mtazamo na Dhana tuu ambayo hata wasioheshimiwa huweza kuona wanaheshimiwa au kuogopwa.

Siku utakapofanikiwa utafiki kila mtu atajua umefanikiwa, utadhani kila mtu anayaona mafanikio yako. Lakini watu utawaona wanakuchukulia wewe mtu wa kawaida Kama wao. Sio ajabu ukawa unawauliza unanijua Mimi ni Nani? Hapo akili yako itakuonyesha watu wakikuona kwani wewe ni nani, mbona ni wakawaida tuu Kam wao. Basi utakuwa ukichukia mno. Na Kama hautakuwa makini utajikuta ukitenda mambo mabaya na kuwaonea watu ili wajue wewe ni Nani lakini hata ungefanyaje bado akili yako ingekuonyesha kuwa watu wanakuchukulia wakawaida. Hapo utajifunza kuwa kumbe wewe ndiye mwenye wajibu wa kujijua wewe ni Nani na sio jukumu la mtu. Kingine utajifunza kuwa mafanikio ya mtu yapo moyoni kwake na Rohoni mwake na wala sio nje yake watu wayaone. Utajifunza kuwa Wewe ni mtu Kama watu wengine.
Na uombe Mungu uligundue Hilo mapema kabla hujachelewa. Ukishagundua hilo hapo ndipo utakuwa umefanikiwa.

Utakuwa na pesa lakini hautajitamba mbele za watu kuwa unapesa. Utakuwa na Cheo lakini hautaumiza watu. Wala hautatesa watu hasa wasio na hatia.
Hapo ndipo watu utawaona wakikuona umefanikiwa, akili yako itawaona watu wakikuona Kama mtu mwenye mafanikio na mwenye bahati lakini utawazuia wasikusifie kwani utaona wakusifiwa ni Mungu pekee.

Siku utakapofanikiwa vile ulivyodhani umetumia nguvu nyingi, na muda mwingi siku hiyo utaona Kama ulitumia muda mchache, tena utaona ulijihangaisha bure kumbe Jambo lenyewe ndilo Hilo tuu. Hapo utajifunza kila kitu ni ubatili kwenye hii Dunia.

Siku utakapofanikiwa wale uliofikiri utawasaidia na kuwahurumi ndio haohao utawaona hawastahili kusaidiwa na kuhurumiwa. Kwani utawaona wanamaisha mazuri na yasiyo na shida Kama maisha yako ya mafanikio. Utawaonea wivu kwani utataka wapate shida na kuumia ili uone utofauti wako na wao. Hapo utagundua kuwa hakuna tofauti ya aliyefanikiwa na asiyefanikiwa. Mwenye elimu na asiye na elimu. Watu wote ni sawa.

Siku utakapofanikiwa kama ulitumia nguvu kubwa na kutesa watu au kuwadhulumu, au kuwaumiza watu utashangaa Wale uliowatesa wakiishi Kwa Amani na Raha huku wewe ukijiona Shetani, mtu mjinga usiyejitambua, kwani kile ulichokipigania iwe mi Utajiri au Cheo utakiona cha kawaida Sana. Hautaona tofauti Kati ya wewe mpya mwenye Cheo na Yule wa zamani usiye na Cheo. Utaishi Kwa hatia lakini utahangaika kuificha hatia yako Kwa gharama kubwa ambayo haitasaidia lolote.
Ndipo utajifunza kuwa kwenye maisha hakuna Jambo zuri Kama kuwa mwema na kutenda wema.

Siku utakayofanikiwa vile vitu ulivyokuwa unavipenda na kuvihusudu ndivyo utakavyokuwa unaviona vya kawaida na wala hautavifurahia tena. Ila wale ambao hawajafanikiwa watakuwa wanafurahia kuvipata vitu hivyo na kuenjoi. Hii ni kusema watakuwa na furaha kukushinda wewe uliyefanikiwa.
Hapo utajifunza kuwa Kitu kizuri ni kile ambacho huna na ambacho kipo Kwa mwenzako.

Siku ukifanikiwa na kuwa Tajiri vile ulivyokuwa unauchukia umasikini na mambo yake, utajikuta ukianza kuupenda na kuvutiwa nao. Hiyo itakufunza kuwa Maisha ni kuridhika Kwa kile ulicho nacho.

Siku utakapofanikiwa vile ulikuwa unashinda njaa Kwa kukosa chakula na hela ya kununulia chakula, ndivyo utakavyoshinda njaa Kwa kukosa hamu ya Kula licha ya kuwa Una chakula na hela ya kununulia chakula chochote upendacho.
Hapo utajifunza kuwa ni hakuna tofauti ya Masikini na tajiri kwenye uhitaji isipokuwa namna ya uhitaji.

Siku utakayofanikiwa Wale wanawake warembo na wazuri uliokuwa unatamani siku ukifanikiwa utaoa mmoja wao utashangaa ukitumia nguvu kubwa ili kuwafanya wakupende lakini wanaume Masikini wakijichukulia kirahisi na kuwaoa. Utagundua kuwa hawakupendi Ila wanazitamani pesa zako tuu. Jambo hilo litakuumiza kila mara kila ukimtazama Mkeo ambaye unajua kabisa hajakupenda wewe isipokuwa pesa zako.
Mbele za watu utakuwa unajivunia lakini moyoni utakuwa unaumia na kupitia maumivu makali. Hapo utaona ni Kheri Masikini anayependwa na Mwanamke Kwa moyo wake wote kuliko wewe Tajiri usiyependwa ila pesa zako ndizo zinapendwa.
Hapo utajifunza maisha na hulka na haiba, iwe ni masikini au Tajiri, msomi au asiyesoma kinachoangaliwa ni hulka na haiba.

Siku utakayofanikiwa hautaona umuhimu wa kuwa na watoto wengi Kama vile ulivyokuwa masikini, lakini siku za uzee wako utajilaumu Kwa kuzaa watoto wachache huku masikini akijivunia kuwa na watoto wengi.

Nimemaliza!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Hakunaga siku maalum ya kufanikiwa. Kufanikiwa ni matokeo ya hatua kwa hatua.
Hata wale wanaopataga mawe ya Tanzanite, ni mara chache sana utakuta alikuwa maskini hohe hahe. Utakuta alishapata kidogo kidogo. Anabadilisha mboga.
Pili: kufanikiwa ni relative term. Mtu mwenye take home ya 1M kijijini kwetu anakuwa kati ya watu waliofanikiwa sana. Lakini mtu huyo huyo katiki jiji la Dar es Salaam au Arusha au Mwanza au Dodoma ni kati ya maskini.
 
Kwa hiyo uko Mzee unahangaika na kuomba Kazi ndogo ndogo au unaomba omba sio fedheha ni nini? Acha masihara mkuu..

Pili kama hujawa Mzee huwa unaona watu Wana struggle kupata basic needs ,wanaishi sehemu ambazo sio decent nk
Still ni perception ya mtu, inaweza kuwa kwako kuomba ni aibu ila kwa mwingine ndiyo maisha yake na it's okay to him/her.
 
Kabla hata sijasoma nitangulize shukran maana umepotea kidogo mdogo angu. Na Eyce nimemuona humu.
Haya nikaanzie juu
 
Kwema Wakuu!

Siku utakayofanikiwa Wale uliodhani utawakomesha, utawaringishia wengi wao watakuwa hawapo, watakuwa wamekufa!

Siku utakapofanikiwa wengi WA watu uliokuwa unawaonea aibu na kuwahofia watakudharau usifanye kazi fulani watakuwa wamekufa, au utagundua hakuna aliyekuwa anafuatilia maisha yako. Hapo ndipo utajiona ulikuwa mjinga.

Siku utapofanikiwa wengi uliokuwa unawapenda Sana ukasema siku ukifanikiwa kimaisha utawafurahisha, wengi wao watakuwa hawapo, watakuwa wamekufa. Na hapo ndipo utaelewa kuwa unaweza kumfurahisha mtu hata Kwa kidogo ulichonacho sasa.

Hapo utayaona mafanikio hayana maana yoyote Ile Kwa sehemu kubwa.

Siku utakayofanikiwa ndio siku kila mtu utamuona amefanikiwa wewe ndio ulikuwa WA mwisho. Hiyo ni kutokana na kuwa kila mtu utamtazama katika jicho la kufanikiwa. Hapo utajua kuwa kumbe wakati mwingine mafanikio ni mtazamo wa mtu tuu.
Wakati sasa hivi unajiona huna Raha na unamaisha magumu lakini siku ukifanikiwa utawaona watu wenye maisha Kama yako ya zamani wakiishi Kwa Raha. Na hapo utagundua maisha ni kuridhika.

Siku ukifanikiwa wengi uliodhani watakuheshimu na kukutukuza utawaona Kama wanakuchukulia kawaida. Hawakuheshimu. Hapo wengi hujikuta wakilazimisha kuheshimiwa Jambo ambalo sio Sawa. Na hapo utajifunza kuwa kuheshimiwa ni mtazamo na Dhana tuu ambayo hata wasioheshimiwa huweza kuona wanaheshimiwa au kuogopwa.

Siku utakapofanikiwa utafiki kila mtu atajua umefanikiwa, utadhani kila mtu anayaona mafanikio yako. Lakini watu utawaona wanakuchukulia wewe mtu wa kawaida Kama wao. Sio ajabu ukawa unawauliza unanijua Mimi ni Nani? Hapo akili yako itakuonyesha watu wakikuona kwani wewe ni nani, mbona ni wakawaida tuu Kam wao. Basi utakuwa ukichukia mno. Na Kama hautakuwa makini utajikuta ukitenda mambo mabaya na kuwaonea watu ili wajue wewe ni Nani lakini hata ungefanyaje bado akili yako ingekuonyesha kuwa watu wanakuchukulia wakawaida. Hapo utajifunza kuwa kumbe wewe ndiye mwenye wajibu wa kujijua wewe ni Nani na sio jukumu la mtu. Kingine utajifunza kuwa mafanikio ya mtu yapo moyoni kwake na Rohoni mwake na wala sio nje yake watu wayaone. Utajifunza kuwa Wewe ni mtu Kama watu wengine.
Na uombe Mungu uligundue Hilo mapema kabla hujachelewa. Ukishagundua hilo hapo ndipo utakuwa umefanikiwa.

Utakuwa na pesa lakini hautajitamba mbele za watu kuwa unapesa. Utakuwa na Cheo lakini hautaumiza watu. Wala hautatesa watu hasa wasio na hatia.
Hapo ndipo watu utawaona wakikuona umefanikiwa, akili yako itawaona watu wakikuona Kama mtu mwenye mafanikio na mwenye bahati lakini utawazuia wasikusifie kwani utaona wakusifiwa ni Mungu pekee.

Siku utakapofanikiwa vile ulivyodhani umetumia nguvu nyingi, na muda mwingi siku hiyo utaona Kama ulitumia muda mchache, tena utaona ulijihangaisha bure kumbe Jambo lenyewe ndilo Hilo tuu. Hapo utajifunza kila kitu ni ubatili kwenye hii Dunia.

Siku utakapofanikiwa wale uliofikiri utawasaidia na kuwahurumi ndio haohao utawaona hawastahili kusaidiwa na kuhurumiwa. Kwani utawaona wanamaisha mazuri na yasiyo na shida Kama maisha yako ya mafanikio. Utawaonea wivu kwani utataka wapate shida na kuumia ili uone utofauti wako na wao. Hapo utagundua kuwa hakuna tofauti ya aliyefanikiwa na asiyefanikiwa. Mwenye elimu na asiye na elimu. Watu wote ni sawa.

Siku utakapofanikiwa kama ulitumia nguvu kubwa na kutesa watu au kuwadhulumu, au kuwaumiza watu utashangaa Wale uliowatesa wakiishi Kwa Amani na Raha huku wewe ukijiona Shetani, mtu mjinga usiyejitambua, kwani kile ulichokipigania iwe mi Utajiri au Cheo utakiona cha kawaida Sana. Hautaona tofauti Kati ya wewe mpya mwenye Cheo na Yule wa zamani usiye na Cheo. Utaishi Kwa hatia lakini utahangaika kuificha hatia yako Kwa gharama kubwa ambayo haitasaidia lolote.
Ndipo utajifunza kuwa kwenye maisha hakuna Jambo zuri Kama kuwa mwema na kutenda wema.

Siku utakayofanikiwa vile vitu ulivyokuwa unavipenda na kuvihusudu ndivyo utakavyokuwa unaviona vya kawaida na wala hautavifurahia tena. Ila wale ambao hawajafanikiwa watakuwa wanafurahia kuvipata vitu hivyo na kuenjoi. Hii ni kusema watakuwa na furaha kukushinda wewe uliyefanikiwa.
Hapo utajifunza kuwa Kitu kizuri ni kile ambacho huna na ambacho kipo Kwa mwenzako.

Siku ukifanikiwa na kuwa Tajiri vile ulivyokuwa unauchukia umasikini na mambo yake, utajikuta ukianza kuupenda na kuvutiwa nao. Hiyo itakufunza kuwa Maisha ni kuridhika Kwa kile ulicho nacho.

Siku utakapofanikiwa vile ulikuwa unashinda njaa Kwa kukosa chakula na hela ya kununulia chakula, ndivyo utakavyoshinda njaa Kwa kukosa hamu ya Kula licha ya kuwa Una chakula na hela ya kununulia chakula chochote upendacho.
Hapo utajifunza kuwa ni hakuna tofauti ya Masikini na tajiri kwenye uhitaji isipokuwa namna ya uhitaji.

Siku utakayofanikiwa Wale wanawake warembo na wazuri uliokuwa unatamani siku ukifanikiwa utaoa mmoja wao utashangaa ukitumia nguvu kubwa ili kuwafanya wakupende lakini wanaume Masikini wakijichukulia kirahisi na kuwaoa. Utagundua kuwa hawakupendi Ila wanazitamani pesa zako tuu. Jambo hilo litakuumiza kila mara kila ukimtazama Mkeo ambaye unajua kabisa hajakupenda wewe isipokuwa pesa zako.
Mbele za watu utakuwa unajivunia lakini moyoni utakuwa unaumia na kupitia maumivu makali. Hapo utaona ni Kheri Masikini anayependwa na Mwanamke Kwa moyo wake wote kuliko wewe Tajiri usiyependwa ila pesa zako ndizo zinapendwa.
Hapo utajifunza maisha na hulka na haiba, iwe ni masikini au Tajiri, msomi au asiyesoma kinachoangaliwa ni hulka na haiba.

Siku utakayofanikiwa hautaona umuhimu wa kuwa na watoto wengi Kama vile ulivyokuwa masikini, lakini siku za uzee wako utajilaumu Kwa kuzaa watoto wachache huku masikini akijivunia kuwa na watoto wengi.

Nimemaliza!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kumbe hata mimi na admire kupata kazi serikalini, siku ikitokea nimepata nitaona kawaida tu.!

Duniani hapa big deal ni kumcha Mungu tu aisee.

Nimekuelewa sana mtoa mada.
 
Kweli kabisa nikikumbuka tukiwa shule primary tukaambiwa wazuri wako olevel tukafika wakasema Hawa sio wazuri wako a level 🤣 tukafika tena wakasema wako vyuo vikuu tukafika wanasema wako mtaani.😂😂😂
Duu nilichoka
Mwisho; Maisha ni kukubaliana na uhalisia na kulidhika
 
Huwa sikupendi/kukukubali lakini leo kutoka moyoni nasema umeandika kitu cha maana na ukweli tupu. Hongera sana mkuu
Hyu jamaa taikon kwel..Kuna maada zake ziko deep@chkuliaa mfano mtu anayetaman akinunuaa gari mfn ist.ili ataambee mtaan kwakee!akiwa njian..akapitwa na range Rover..cjui anajichukuliaje@mfano unanihusu!maisha n ubatili mtupu aisee
 
Yuko sahihi sana, mimi nilikuwa nadhani nikinunua gari basi ntakuwa na raha isiyo na kifani, lakini sasa naona kama gari ni chanzo cha mimi kukosa furaha na sioni thamani yake tofauti na thamani ya fedha tu.
 
Back
Top Bottom