Siku ya Demokrasia Duniani (2021): Rais Samia azungumza na Wanawake wa Tanzania, jijini Dar es Salaam

Siku ya Demokrasia Duniani (2021): Rais Samia azungumza na Wanawake wa Tanzania, jijini Dar es Salaam

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Siku ya Demokrasia Duniani huadhimishwa kila Septemba 15, ikitoa fursa ya kuangalia hali ya Demokrasia ulimwenguni kote. Miongoni mwa misingi muhimu ya Demokrasia ni kuheshimu #HakiZaBinadamu

Umoja wa Mataifa (UN) umesisitiza Nchi kuheshimu na kulinda Uhuru wa Kujieleza, Uhuru wa Habari pamoja na Haki nyingine

#JamiiForums #DemocracyDay #Democracy

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 15, anazungumza na Wanawake wa Tanzania ikiwa ni siku ya Demokrasia duniani.

Ni katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Mkoani Dar Es Salaam.

Unatamani leo azungumzie nini? Je, awamu yake inaimarisha Demokrasia Nchini? Nini Mategemeo yako kwenye Hotiba yake ya leo?

Tupe maoni yako.

Tutatoa Updates kwa kila kinachojiri Ukumbini.

Karibuni sana.

samia.jpg
=====

UPDATES

AMOS MAKALLA, MKUU WA MKOA WA DAR
Mheshimiwa Rais, Mkusanyiko huu una Shamrashamra zote hizi ni kwasababu tupo salama. Dar es Salaam ni salama.

SAUM RASHID, MWENYEKITI – WANAWAKE VIONGOZI (WANASIASA)
Kiukweli ndani ya mioyo yetu wanawake tulitamani tuwe na rais Mwanamke na leo hii ndoto zetu zimetimia.

Hii haikutokea kwa bahati mbaya; ni uadilifu wako na uwajibikaji wako.

Na wanawake wote wa Tanzania tunaahidi kwako kuwa tutaendelea kujenga mazingira ya amani na utulivu ili uendelee kuchapa kazi sawasawa

ASENI MURRO, MWENYEKITI – MTANDAO WA WANAWAKE, KATIBA, UCHAGUZI NA UONGOZI
Tunakuomba kuweka utaratibu wa kukutana na sisi wanamtandao na Wanawake kwa vipindi ambavyo utajipangia mwenyewe. Ulivyokuwa Makamu wa Rais ulijiwekea utaratibu wa kukutana na sisi kwa miezi sita kuteta maendeleo ya nchi na ajenda za wanawake.

Tunaomba ikikupendeza urasimishe utaratibu wa kukutana na sisi na kuchukua wataalamu nje ya mfumo wako wa serikali kuweza kukusaidia shughuli zako za serikali.

Aidha, tunaahidi na tunapenda na kukuwezesha kujenga kanzidata ya wataalamu walio kwenye mtandao na wanaharakati kwa ujumla ili uweze kutumia hii kanzi data unapowahitaji katika teuzi zako.

Tunaamini Wizara inayoshughulikia wanawake ikipewa nguvu zaidi kirasilimali na ki-mandate ikaweza kusimamia wizara zingine ili kusimamia masuala ya wanawake kwa ufanisi zaidi katika sekta mbalimbali za serikali.

Tunakutakia neema na hekima kutoka kwa Mungu katika uongozi wako.

SALOME ANYOTI, MWENYEKITI -- MTANDAO WA SEXTORTION
Suala la Rushwa ya Ngono sisi kama wanawake wa Tanzania na wanamtandao tunafurahi kuwa tumelifikisha mahali – tumefanya mazungumzo na tafiti na sasa limekuwa sheria na imeingia TAKUKURU kama corruption (rushwa)

Pamoja na mafanikio hayo, suala hili lina changamoto zake katika kutekeleza na kuendeleza hiyo Sheria ya Rushwa ya Ngono. Hapo ndiyo tunaamini tutashirikana na wewe kuiweka hiyo Sheria iwe kidogo nyepesi na rahisi ili kesi zisikilizwe.

JULIA BROUSSARD, MWAKILISHI MKAZI – UN WOMEN, TANZANIA
Tunakubali kuwa ushiriki wa wanawake unakuza demokrasia na ili kuwa na jamii ya kidemokrasia, maamuzi yanayochukuliwa ni lazima yawahusishe wanawake.

Ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi zote za maamuzi ni kiashiria muhimu cha demokrasia imara.

Tafiti zinaonesha kuwa kuweka wanawake katika ngazi za uongozi hazinufaishi tu wanawake peke yao, bali pia jamii kwa ujumla. Inapelekea kuwepo kwa sera zinazotazama masuala ya kijinsia, jamii zenye amani na shirikishi, lakini pia ugawaji wa rasilimali za nchi zinazohakikisha huduma za kijamii kama vile elimu, afya pamoja na maendeleo ya watoto na wazee zinapatikana.

Lakini pia inasaidia kuondoa fikra kandamizi na fikra potofu lakini pia kuongeza wanawake wengi zaidi katika ngazi za uongozi ikiwa ni pamoja na siasa na utuishi wa umma.

Bahati nzuri Tanzania imepiga hatua kubwa katika eneo hili, na ni kwasababu ya kujitoa kwa nchi katika uwezeshaji wa wanawake na ndiyo maana tumeweza kujiunga na wewe kusherehekea kuwa na Rais wa Kwanza Mwanamke wa JMT, Mh. Samia Suluhu Hassan.

Kwa niaba ya UN Women, ningependa kukupongeza kwa jitihada zako kuendeleza ushiriki wa wanawake. Kujitoa kwako katika kuongeza idadi ya wanawake katika maeneo muhimu ya kimkakati katika uongozi kumekuwa ni jambo la kutia moyo kuhusu mustakabali wa ushirikishaji wa wanawake na ulingo wa kidemokrasia.

Leo uwiano wa wanawake umesimama katika asilimia 38, uwiano ambao ni asilimia 14 zaidi ya wastani wa dunia. Wanawake kwa sasa wanashikilia asilimia 30 ya Baraza la Mawaziri na tunakupongeza kuweka wanawake katika wizara muhimu ikiwa ni pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya TAMISEMI, Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Ulinzi na JKT pamoja na Wizara ya Mawasiliano.

Teuzi zote hizi zinaendelea kuboresha mazingira au nafasi ya kukuza Demokrasia katika nchi na kwakweli hiki ni kitu cha kujivunia, siyo tu kwa wanawake na si tu kwa demokrasia bali katika kufanikisha maendeleo endelevu ya nchi nzima.

Nitumie nafasi hii kukushukuru na kuishukuru jitihada za Serikali ya Tanzania katiak kujiunga na Kampeni ya Umoja wa Mataifa ya Generation Equality katika ile coalition ya Haki ya Kiuchumi mwaka huu. Hii inaonesha hatua zilizopigwa na wanawake na nchi katika kukuza ushiriki wa wanawake katika ngazi mbalimbali za kisiasa. Ninaamini kuwa kutakuwa na nafasi nyingi zaidi na faida nyingi zaidi za wanawake, lakini pia wanaume, vijana na mabinti katika jamii na katika kukuza uchumi wa nchi.

Mzee JOHN CHEYO
Ukweli unaotoka ndani ya moyo wangu ni kuwa kwa kazi ambayo tumeiona kwa miezi sita, ni kama ulitengenezwa kuchukuwa nchi hii na kuipeleka juu zaidi – na ni mwanamke. Kwa akina mama, mshiwe na mashaka… acheni wasiwasi. Uwezo mnao, nchi hii twendeni pamoja kama mama anavyotuomba kila wakati, tuhakikishe nchi hii inakwenda kwa amani. Chokochoko zile tuache!

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN
Tuzo hizi si zangu, ni za wanawake wote wa Tanzania. Wanawake ambao kila siku wanatafuta mbinu za namna ya kulea familia, kama alivyosema Mzee Cheyo. Lakini wanawake ambao kila siku wanaamka kwenda mashambani, kazini na kwenye biashara. Ni za wanawake wajasiriamali ambo kila siku wanabuni miradi ili kuinua vipato na ustawi wa familia.

Pia tuzo hii ni kwa ajili ya wanawake majasiri waliothubutu kuingia katika siasa na shughuli za kufanya maamuzi katika fani na ngazi mbalimbali na kuondoa dhana ya kuwa shughuli hizo ni kwaajili ya wanaume.

Wanawake hawa mahiri na mashuhuri tulionao hapa ndani ni zao la demokrasia na katiba nzuri ya Tanzania.

Kama tujuavyo, demokrasia ni dhana pana iliyobeba tafsoiri nyingi n ahata hivyo kwa kuzingatia tafsiri inayokubalika kimataifa, inahusisha makubwa manne: uwepo wa uhuru katika nchi, kuheshimu haki za binadamu, kuheshimu utawala wa sheria, ushiriki wa wananchi kuweka serikali kupitia uchaguzi huru na wa haki.

Masuala mengine yanayohusisha demokrasia ni ugawaji wa rasilimali kwa uwiano lakini pia utawala bora

Kwa kuzingatia hayo yote, hakuna shaka kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongozwa kwa kufuata misingi ya demokrasia.

i. Uchumi wa Wanawake
Kwenye uchumi wa wanawake nchi yetu imepiga hatua kubwa sana mpaka leo tunazungumzia wanawake wajasiriamali, wanawake wafanyabiashara wakubwa lakini wanawake makontrakta wapo wengi nchini. Ingawa bado kuna changamoto ndogondogo tunazopaswa kuzifanyia kazi ili waweze kufanya kazi zao vizuri.

Katika kuangalia uchumi wa wanawake, njia rahisi niiliyoiona nilipokuwa Makamu wa Rais ni kupitia majukwaa ya kiuchumi ya wanawake na nilihamasiasha mikoa kuunda majukwaa. Mpaka naachia mkono majukwaa, kulikuwa na majukwaa 23, pamoja na lile la Dar es Salaam. Siku nazindua jukwaa la la Dar es Salaam lilikuwa na wanachama 15,000. Sasa hivi sijui liko hali gani.

Nilikuwa na nia thabiti ya kulea majukwaa yaendelee, lakinikama mnavyojua, kwenye positive kuna negative. Lilitazamwa kwa jicho silo likalegalega.

Nataka kuwaahidi kwamba napanga kuyalea majukwaa. Kwa mwaka huu nilikuta bajeti tayari imeanzishwa kwahivyo nisingeweza kupenyeza hiyo ajenda. Lakini kwa bajeti ya mwakani, majukwaa yale ambayo yame-survive, majukwaa 18 yajipange na ambao hawakuwa na majukwaa wayarudishe ili tuendeklee na safari ya maendeleo kwa wanawake.

ii. Uhuru binafsi
Nadhani kila mtu anapenda kuwa huru. Awe huru mwenyewe, awe huru nafsi yake.

Jambo lililopo mbele yetu ni wanawake kujitambua kujua unataka uwe nani, unataka uishi vipi na unataka uweje. Huo ni uhuru binafsi – ni maamuzi yako binafsi.

Kuna uhuru mwingine umetafsiriwa kikatiba kama uhuru wa kutoa maoni, uhuru wa kukusanyika au kujiunga kwenye vikundi n.k

Tunapozungumzia uhuru wa kutoa maoni Tanzania tumefanya kazi nzuri, tumefanya kazi kubwa.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa wingi wa vyombo vya habari.
  • Magazeti 257
  • Redio 197
  • Televisheni 50
  • Televisheni Mtandao 451
  • Blogu 122
Na hii ni kwa mujibu wa taarifa ya mwezi Mei, 2021.

Na katika vyombo hivyo vya habari, zaidi ya asilimia 75 vinamilikiwa na watu binafsi. Na kila chombo kinatoa habari kinachoona inafaa kwa wakati huo.

Kwa uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza Tanzania tupo vizuri sana.

Kuhusu uhuru wa kujiunga kwenye vikundi, hapa kuna wawakilishi wa asasi za kiraia 120 za wanawake.

Huko nje kuna asasi nyingi, vyama vingi na mushika kwa kutumia uhuru wetu wa kujiunga.

Lakini hiyo kama haitoshi, nchi yetu ina vyama vya siasa takribani 20. Tuna vyama vya wafanyakazi, tuna vyama vya wanataaluma mbalimbali, na uhuru wa kukusanyika upo kwa kiasi kikubwa.

ii. Haki za Binadamu
Haki za Binadamu pia zimetambuliwa kwenye katiba yetu. Tumesaini na kuridhia mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu Haki za Binadamu au haki mbalimbali

Pamoja hna hayo tunmeanzisha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora hapa nchini ambapo moja ya majukumu yake ni kupokea malalamiko ya na kufanya uchunguzi wa mambo yanayohusu uvunjajiwa Haki za Binadamu.

Pia nchi yetu inaongozwa na Sheria na hakuna alliye juu ya sheria.

Chaguzi zinazofanyika nchini ni Ushahidi nchi yetu inafuata misingi ya kidemokrasia.

Hata hivyo, nakiri kuwa bado kuna changamoto za kidemokrasia nchi ni hii ni kwakuwa hakuna taifa lolote duniani lenye ukamilifu wa kidemokrasia.

Demokrasia ni mchakato, ukimaliza jambo moja linafuata lingine

Kwa kiasi kikubwa nchi yetu Tanania ipo vizuri kwenye demokrasia

iv. Haki za Wanawake na Usawa wa Jinsia
Ni vigumu kuzungumzia demokrasia bila kugusia masuala ya wanawake na usawa wa kijinsia.

Kwenye nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania, wanawake licha ya kuwa ni wengi, lakini wameachwa nyuma. Hii ni dosari.

Kwa sisi Tanzania kubwa ni kushikana na kufanyia kazi changamoto ili tuendelee na safari ya maendeleo.

Naahidi kuwa serikali itajitahidi kushughulikia masuala ya Haki za Wanawake na Usawa wa Kijinsia ili kukuza demokrasia nchini.

Katika Malengo endelevu kuhusu wanawake, nchi yetu imechukuwa malengo kama 8 na tumeweza kuyatekeleza kwa vizuri sana.

1. Kuondoa umasikini: Hatujafanikiwa lakini kwa kiasi tumefanikiwa kuitoa nchi kutoka hatua moja kwenda nyingine. Huku chini bado kuna wanawake wanaozongwa na umasikini.​
2. Kuondoa Njaa: Tanzania kwa miaka mingi tumeweza kujitosheleza kwa chakula.​
3. Afya Bora: Mmeona jitihada za serikali kusambaza huduma Tanzania nzima. Na baada ya kuona bajeti ya serikali haitoshi, tumetumia njia ya kuongeza vijisenti kwenye matumizi ya simu ili tuweze kwenda haraka kusambaza afya na elimu kwa wananchi wetu.​
4. Elimu Bora: Kama mnavyojua Tanzania tunaongezeka kwa takribani asilimia 8. Tuna vijana wengi wanaoingia la Kwanza na Sekondari kila mwaka. Katika hili Hayati Dkt. Magufuli alisema watoto wote wasome bure. Nami naliendeleza hilo.​
5. Usawa wa Jinsia: Hatujafika tunapokusudia. Mtaendelea kusikia wanawake zaidi wanaingia (kwenye nafasi za uongozi). Nisipofanya mimi, hakuna atakayefanya. Bora tuanze waje watuguse watuone sisi nani. Nafurahi Ulingo kutaka kunipa kanzidata kupata wanawake wenye vigezo.​
6: Upatikanaji wa Nishati ya Kijani na Nafuu: Naendelea kutimiza hili​

7. Inclusive Economic Growth (Ukuaji wa Uchumi Shirikishi): Hapa ndiyo maana tunazungumza masuala ya wanawake na kuwashirikisha ili kufikia huku​
8. Uharibifu wa Mazingira: Hili pia bado tunalifanyia kazi ili kuikinga nchi yetu kuingia kwenye majanga makubwa ya kimazingira.​

Rais Mwanamke tutamuweka mwaka 2025
Leo hii mmempa Tuzo Rais Mwanamke kwa bashasha na furaha kubwa ila nataka niwaambie Wanawake bado hatujaweka Rais Mwanamke, tulichokichangia sisi ni ile kusukuma mpaka Mwanamke akawa Makamu wa Rais ila kufika hapa kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana

Ndugu zangu Rais Mwanamke tutamuweka mwaka 2025, mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana, wameanza kutuchokoza, kuandika kwenye vigazeti ‘Samia hatosimama (kugombea Urais)’ nani kawaambia!?

Fadhila za Mungu zikija mikonononi mwako usiziachie, hizi ni fadhila za Mungu, Wanawake tumefanya kazi kubwa kuleta uhuru na kujenga soda za Nchi hizi, tumebeba sana Wanaume katika siasa za Nchi hizi, leo Mungu ametupa baraka mikononi tukiiachia Mungu atatulaani

 
Atoe mfano wa Yeye Mwenyewe kama zao la kuheshimu demokrasia kuwa alipokea madaraka kwa kuzingatia demokrasia na katiba kwenye nchi ambayo kwa sehemu kubwa ni male dominated
 
Aachane na kesi ya Mbowe, pia sio kila kinacholetwa kwenye faili anakibeba kama kilivyo
 
[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706] tupu, yaani hata wanaomsikiliza huyo mama naona kichwani hsmnazo,
Hivi inakuaje siku ya demonrasia unaenda kuzungumza na wanawake,...? Siku ya wanawake alikuwa wapi?
 
Women and Democracy?
Au mi ndio sielewi?..

hapakua na most relevant audience mfano vyama vya siasa ?

mhh haya bwn..
 
[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706] tupu, yaani hata wanaomsikiliza huyo mama naona kichwani hsmnazo,
Hivi inakuaje siku ya demonrasia unaenda kuzungumza na wanawake,...? Siku ya wanawake alikuwa wapi?
Inshort ameligeuza hili taifa limekua taifa la kike.
 
Wadau msilalamike sana, wengi wenu ndiyo wale tulio shangilia kwa kusema "ANAUPIGA MWINGI" imekuwaje tena leo 😁!.

Ndiyo ameshakuwa Rais hivyo, zile biashara za kujipa moyo kuwa mtu mpya ataleta neema, watanzania tubadilika.
 
Back
Top Bottom