Wafitini hamlali....Kila siku wanawake amekuwa rais wa wanawake hajua huwa hawapendani ,asitegemee watambeba kwa Kura kwenye uchaguzi thubutu
USSR
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wafitini hamlali....Kila siku wanawake amekuwa rais wa wanawake hajua huwa hawapendani ,asitegemee watambeba kwa Kura kwenye uchaguzi thubutu
USSR
Hii ni udhalilishaji wa kijinsia kwa hali ya juu kabisaInshort ameligeuza hili taifa limekua taifa la kike.
Kwenye "uchafuzi" wa 2020, MaCCM waliteua wagombea wanawake wasiozidi 25 kugombea kwenye majimbo, CHADEMA iliteua wanawake zaidi ya 50... ni muhimu kukumbushana hili leo ikiwa ni siku ya Demokrasia na Mh Rais anakutana na wanawake... Tanzania ina majimbo 264Siku ya Demokrasia Duniani huadhimishwa kila Septemba 15, ikitoa fursa ya kuangalia hali ya Demokrasia ulimwenguni kote. Miongoni mwa misingi muhimu ya Demokrasia ni kuheshimu #HakiZaBinadamu
Umoja wa Mataifa (UN) umesisitiza Nchi kuheshimu na kulinda Uhuru wa Kujieleza, Uhuru wa Habari pamoja na Haki nyingine
#JamiiForums #DemocracyDay #Democracy
View attachment 1938342
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 15, anazungumza na Wanawake wa Tanzania ikiwa ni siku ya Demokrasia duniani.
Ni katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Mkoani Dar Es Salaam.
Unatamani leo azungumzie nini? Je, awamu yake inaimarisha Demokrasia Nchini? Nini Mategemeo yako kwenye Hotiba yake ya leo?
Tupe maoni yako.
Tutatoa Updates kwa kila kinachojiri Ukumbini.
Karibuni sana.
=====
UPDATES
=====
AMOS MAKALLA, MKUU WA MKOA WA DAR
Mheshimiwa Rais, Mkusanyiko hu una Shamrashamra zote hizi ni kwasababu tupo salama. Dar es Salaam ni salama.
SAUM RASHID, MWENYEKITI – WANAWAKE VIONGOZI (WANASIASA)
Kiukweli ndani ya mioyo yetu wanawake tulitamani tuwe na rais Mwanamke na leo hii ndoto zetu zimetimia.
Hii haikutokea kwa bahati mbaya; ni uadilifu wako na uwajibikaji wako.
Na wnawake wote tuna wa Tanzania tunaahidi kwako kuwa tutaendelea kujenga mazingira ya amani na utulivu ili uendelee kuchapa kazi sawasawa
ASENI MURRO, MWENYEKITI – MTANDAO WA WANAWAKE, KATIBA, UCHAGUZI NA UONGOZI
Tunakuomba utaratibu wa kuweka wa kukutana na sisi wanamtandao na Wanawake kwa vipindi ambavyo utajipangia mwenyewe. Ulivyokuwa Makamu wa Rais ulijiwekea utaratibu wa kukutana na sisi kwa miezi sita kuteta maendeleo ya nchi na ajenda za wanawake.
Tunaomba ikikupendeza urasimishe utaratibu wa kukutana na sisi na kuchukua wataalamu nje ya mfumo wako wa serikali kuweza kukusaidia shughuli zako za serikali.
Aidha tunaahidi na tunapenda na kukuwezesha kujenga kanzidata ya wataalamu walio kwenye mtandao na wanaharakati kwa ujumla ili uweze kutumia hii kanzi data unapowahitaji katika teuzi zako.
Tunaamini Wizara inayoshughulikia wanawake ikipewa nguvu zaidi kirasilimali na ki-mandate ikaweza kusimamia wizara zingine ili kusimamia masuala ya wanawake kwa ufanisi zaidi katika sekta mbalimbali za serikali.
Tunakutakia neema na hekima kutoka kwa Mungu katika uongozi wako.
SALOME ANYOTI, MWENYEKITI -- MTANDAO WA SEXTORTION
Suala la Rushwa ya Ngono sisi kama wanawake wa Tanzania na wanamtandao tunafurahi kuwa tumelifikisha mahali – tumefanya mazungumzo na tafiti na sasa limekuwa sheria na imeingia TAKUKURU kama corruption (rushwa)
Pamoja na mafanikio hayo, suala hili lina changamoto zake katika kutekeleza na kuendeleza hiyo Sheria ya Rushwa ya Ngono. Hapo ndiyo tunaamini tutashirikana na wewe kuiweka hiyo Sheria iwe kidogo nyepesi na rahisi ili kesi zisikilizwe.
Siku ya Demokrasia Duniani huadhimishwa kila Septemba 15, ikitoa fursa ya kuangalia hali ya Demokrasia ulimwenguni kote. Miongoni mwa misingi muhimu ya Demokrasia ni kuheshimu #HakiZaBinadamu

JULIA BROUSSARD, MWAKILISHI MKAZI – UN WOMEN, TANZANIA
Tunakubali kuwa ushiriki wa wanawake unakuza demokrasia na ili kuwa na jamii ya kidemokrasia, maamuzi yanayochukuliwa ni lazima yawahusishe wanawake.
Ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi zote za maamuzi ni kiashiria muhimu cha demokrasia imara.
Tafiti zinaonesha kuwa kuweka wanawake katika ngazi za uongozi hazinufaishi tu wanawake peke yao, bali pia jamii kwa ujumla. Inapelekea kuwepo kwa sera zinazotazama masuala ya kijinsia, jamii zenye amani na shirikishi, lakini pia ugawaji wa rasilimali za nchi zinazohakikisha huduma za kijamii kama vile elimu, afya pamoja na maendeleo ya watoto na wazee zinapatikana.
Lakini pia inasaidia kuondoa fikra kandamizi na fikra potofu lakini pia kuongeza wanawake wengi zaidi katika ngazi za uongozi ikiwa ni pamoja na siasa na utuishi wa umma.
Bahati nzuri Tanzania imepiga hatua kubwa katika eneo hili, na ni kwasababu ya kujitoa kwa nchi katika uwezeshaji wa wanawake na ndiyo maana tumeweza kujiunga na wewe kusherehekea kuwa na Rais wa Kwanza Mwanamke wa JMT, Mh. Samia Suluhu Hassan.
Kwa niaba ya UN Women, ningependa kukupongeza kwa jitihada zako kuendeleza ushiriki wa wanawake. Kujitoa kwako katika kuongeza idadi ya wanawake katika maeneo muhimu ya kimkakati katika uongozi kumekuwa ni jambo la kutia moyo kuhusu mustakabali wa ushirikishaji wa wanawake na ulingo wa kidemokrasia.
Leo uwiano wa wanawake umesimama katika asilimia 38, uwiano ambao ni asilimia 14 zaidi ya wastani wa dunia. Wanawake kwa sasa wanashikilia asilimia 30 ya Baraza la Mawaziri na tunakupongeza kuweka wanawake katika wizara muhimu ikiwa ni pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya TAMISEMI, Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Ulinzi na JKT pamoja na Wizara ya Mawasiliano.
Teuzi zote hizi zinaendelea kuboresha mazingira au nafasi ya kukuza Demokrasia katika nchi na kwakweli hiki ni kitu cha kujivunia, siyo tu kwa wanawake na si tu kwa demokrasia bali katika kufanikisha maendeleo endelevu ya nchi nzima.
Nitumie nafasi hii kukushukuru na kuishukuru jitihada za Serikali ya Tanzania katiak kujiunga na Kampeni ya Umoja wa Mataifa ya Generation Equality katika ile coalition ya Haki ya Kiuchumi mwaka huu. Hii inaonesha hatua zilizopigwa na wanawake na nchi katika kukuza ushiriki wa wanawake katika ngazi mbalimbali za kisiasa. Ninaamini kuwa kutakuwa na nafasi nyingi zaidi na faida nyingi zaidi za wanawake, lakini pia wanaume, vijana na mabinti katika jamii na katika kukuza uchumi wa nchi.
[emoji16][emoji16][emoji16] aibu hii aiseee, badala ya kujadili Mambo ya msingi kuhusu demokrasia wao wanaleta hadithi za mende kaangusha kabati
Sawa, tumemsikia lakini nashauri Mama afanye ufuatiliaji wa matumizi ya hizo fedha kwani mpaka sasa mitaani kuna manunguniko kuwa ada na michango vimesharudishwa mashuleni!
Kweli dunia gunia!View attachment 1938941
Huyu tusipoungana kumkemea bila kujali vyama atatuvuruga sana. Hana anachowaza kabisa hapo ikulu. Anawaza uchaguzi na uwanawake tu. Wanawake wanawake wanawake. Vipi anataka na wanaume waanzishe kampeni?