Kuna shule inaitwa Mwakavuta (wenyeji wanaiita Mwakauta) nikavuta siku za kuripoti kwa kua nilitaka nitoke nyumbani baada ya valentine day.
Nafika siku hiyo ni jumapili siku ya wali. Nikala kidogo nikaugawa, naenda kuosha sahani ghafla ukungu umetanda kiasi hauwezi kuona hatua mbili mbele.
Nikasimama pale pale kwa zaidi ya dakika 45 ili ukungu upite nisije nikapotea nikaingia msituni. Sehemu yenye baridi kali kama haujavaa viatu au ni vyepesi vidole vya miguuni unaanza kuhisi vinachomwa chomwa na sindano. Nahisi ni dalili za kua frostbitten.
Ukungu unamalizikia vidole vikawa vinaonyesha kama damu imevilia. Tumelala bwenini nakutana na watu kutoka Chunya, Kilimanjaro, Moshi, Kigoma, Mafinga n.k. na wote wanasema baridi la pale si mchezo.
Asubuhi naamka. Njia za shule zote zina theluji, boksa niliyoiacha jana kwenye kamba imeganda kwa barafu.
Nikaanza kupima pros na cons.
-Kwanza walimu walituambia watoto wa O Level wote wana ngoma, kumbe na wale watoto waliambiwa sisi wote tuna ngoma. Ingawa wakinga siyo wabanaji lakini hilo doa litachukua muda wangu.
-Shule haina mabinti wazuri, hao waliopo wavuna mbao na wanakijiji wote mnawagombea.
-Unaweza kua na hela lakini hakuna cha kununua.
-Umbali mpaka wilayani ni 22KM na gari ni moja likipita limepita ama utembee, nilitembea aisee nilikoma, kila sehem ya mwili iliuma. Nilienda kupiga PPS hadi PPS zinatoka ndo nagundua kuna makamasi yalikua yananitoka. Sijui mpiga picha alidhani urembo.
-Rate ya kupiga puchu ikawa juu.
-Walimu wawili wa masomo yangu walikua wanakukaririsha kitu cha kitabuni hawakichambui wala nini halafu ni unasomewa sasa akiwa anasoma unagundua na yeye kuna vitu anavijua hapo. Mmoja alienda Mbeya akakaa zaidi ya mwezi huku somo limesimama.
-Chakula kibaya sijapata kujua. Kuna wadudu hua wanaranda randa kwenye balbu ukiwaua wanatoa harufu mbaya, sasa wale unawakuta kwenye maharage wapo kibao. Wali ikawa ndiyo luxury food, ugali unaula kidogo, asubuhi unanywea uji, makande, unakula kidogo asubuhi unanywea uji.
Wali ulisababisha watu wapigane, kulikua kuna paper two sasa form six wanajihisi wao ndiyo wanatakiwa kuanza, jamaa wa form five akafosi kingi ebwana washkaji wawili akaanza kumpiga.
Ila baadaye na yeye aliwatafuta mmoja mmoja na wakamheshimu.
Nilifeli kwa mengi.