Nilifika Jumamosi jioni nikakuta ni siku ya wali maharage so nikala coz angalau masosi ulikuwa mzuri, kesho yake asubuhi nikapewa uji kwenye kikombe lakini nikashindwa kunywa nikamwaga.
Nilipotoka home nilipewa nyama za kukaanga ndio zinanipa kiburi, zilipoisha ikabidi nianze tu kula maharage sema shule haikuwa na uzio na wali nyama centre walikuwa wanauza buku tu so nikawa natoroka naenda centre kula jamaa wakanibadilisha jina wakaanza kuniita Bourgeoisie (Bujwazii).
Niliwahi kupewa adhabu ya kuchimba visiki kwa kumuita Head Boy Kibaraka wa Walimu.
Nilienda shule na simu na DVD Player zile portable basi raia wengi wakawa rafiki zangu.
Kuna siku jamaa kakuta nanyoosha nguo Jumapili akashangaa hii ndio Pasi ya Umeme? Nikamjibu ndio basi akaomba aishike ajaribu kunyoosha.
Nakumbuka pia siku moja tunacheza inter class madogo wa O Level wakampiga jamaa wa Form Five, usiku tukakaa kikao kwamba haiwezekani waaibishe mwenzetu basi tukapanga mipango ya kupiga O Level kesho yake, tumeamka asubuhi tukakuta Polisi wanafanya kwata nje ya bweni letu hadi tunaenda assemble Polisi wapo tu, tukawaambia sisi hatufanyi fujo tumewachia walimu. Polisi wakaondoka ( Ni mwendo wa dakika 2 tu kati ya Polisi Post na Shule). Kile kitendo cha kuondoka Polisi tukaanzisha timbwili tukachapa O level wote coz maraia tulikuwa tumeficha fimbo kuanzia kiunoni kwenda miguu na wenye mikanda walitumia mikanda. Tulichapa hadi Mwalimu wa Michezo, Second Master akakimbilia kwake. Mara Polisi haoooo na Defender lao piga sana mabomu lakini tulikuwa tushafahamishana kila mtu awe na chupa ya maji.
Sasa kituko kikatokea kwenye kukimbia aise, nilikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo mwanzo tunakimbia kwenye matuta, dah nikapoteza steps kwenye kuruka matuta nikaanguka basi raia wote wa nyuma wakanikanyaga nikajikuta sina nguvu na Polisi wanakuja, pona pona yangu ikawa ni shimo la mchanga nililoliona mita chache kutoka nilipoanguka nikaingia humo na kukaa hadi mchana kila nikatoka kwenda kutafuta wenzangu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].
Tumerudi shule jioni tunakuta waliokamatwa wamekula vitasa balaa. Baada ya timbwili hilo angalau tulianza kuheshimia na O level.