Glenn
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 69,329
- 164,730
Mkuu sio mara zote gari husumbua, tatizo hilo laweza kujitokeza baada ya miaka 3, hapo si furaha yake ilishakamilika?Ha ha ha! Haya Bwana! Ni sawa, Hakuna mtu kakatisha ndoto ya mtu! Naweza nisiwe na Range Rover, Ila nikawa na ya thaman zaidi!
Magari Ni zaidi ya unavyofikiri! Ninayajua Sana! Kwa hiyo Najua machoongea! Hilo gari laitaji uwe Na gari zaidi ya Moja na uwe na hela sio Za ku save miaka 10!
Hilo gari Laweza likakorofisha Umeme lisiwake, ikabidi lifuatwe na winch, sio gari ya mchezo! Sio kwamba twamkatisha tamaa, twamweleza tu ukweli.
Ukiona mtu Ka save miaka 10 kununua gari, especially hili Ambali si ghali kivile; ujue ate save miezi 6 ku service, Na asipopata Fundi mzuri litavurugwa.
Ninavyojua magari mengi kama haya stori zake huanzia kwa mafundi wabovu na vijiweni hupokea korasi yake.
Mimi ni muhanga wa haya mambo.
Kuna gari nilinunua nikapewa muda kuwa sitaweza kulihudumia.
Lakini hadi sasa ni mwaka wa 6 na sijawahi kupata tatizo kubwa zaidi ya kubadili pressure plate tu na gari iko poa mno na huwa nachanja kila mahali, sio tope wala barabara mbovu porini...
Na gari hii mnayoisema sio mbovu ki vile inavyosemwa bali spare zake na fuel consuption iko juu.
Je! Itaharibika kila siku?
Je! Ataenda masafa marefu kila siku?
Kama una ka harrier chako si unabadilisha mara moja moja?
Hii inafaa zaidi kwenda kula bata...mwacheni kijana ale sawa na urefu wa kamba yake[emoji16][emoji16]