Siku ya Kwanza Kuongea Kiingereza mbele ya Kadamnasi kidogo nizimie

Hahahaha umenikumbusha muuza genge mzungu anataka Lady fingers jamaa kagoma kabisa mwambieni muuzaji hayupo wakati yeye ndo muuzaji huku sura kaikunja aisee nilicheka sana
 
mbona mnapenda kumsingizia nyerere? unataka kusema waliosoma kipindi cha nyerere hawajui kiengereza ila waliosoma kipindi cha mtalii kikwete ndiyo mnajua kiingereza? nyerere ndiye aliyeanzisha shule za kata?
Sisi wanafunzi wa kwanza wa upe tulianza na kimombo tangu darasa la kwanza Ndiyo maana Sasa hivi yai linapanda Ile mbaya... Kwa walio na umri wa zaidi Ya miaka 40 wanafahamu Nini maana Ya upe
 
Kuna jamaa alidanganywa kunywa kiroba kiingereza kinakuja chenyewe tu,akaenda kwenye interview kapga v3 alijibu na maswali ambayo hakuulizwa,

Chezea viroba wew!
 
hiz kura pia noma, kama kuna ticha mmoja wakati tupo o level walikuja wazungu kutoka marekani walileta vitabu, walimu wakawa wanajitambulisha paredi, maadam mmoja alisema 'my name is madaam sanga, am married by two childrens'
nimejikuta nacheka..... I'm married by two childrens.... Huyo ni mwalimi. Na mwanafunzi angeambiwa ajitambulishe ingekuwa kasheshe kabisa
 
Shikamoo English. Aliyeleta hii lugha huku kwetu ajee aifuate.
 

hahahahahahahahahahahahaha da u make my day umenichekesha sana
 
Sitasahau siku nilimuomba ruhusa second master na kumwambia " my headache is paining" doh
Unaweza ukajikuta.Darasani mkojo umekubana nusu ya kujikojolea. Ukikumbuka kuomba ruhsa ni kwa kingereza unajikuta. Unabana mkojo. Hata somo unalofundishwa linakuwa hulielewi tena. Unawaza mda wa kutoka uwahi toilet. bora ningezaliwa KENYA tu
 
aseee hivi leo mmekunywa viroba vya mwisho mwisho? yaani kila anae reply ni vikesho tu.....penda sana jf!!!
 
niliwambia form four kuandika narrative essay kuhusu kwenda tour serengeti national park. nikasema wamalizie na sentensi...it was a good day indeed...daaa nilichoka na hivyo vingeleza...mmoja akaanza sas....long period ago iam.go serengeti national park to look animals......i see many many animals one tall and cheter eat meet....jamani nyie achen tu
 
Mimi mzee hakukulia Tanzania ko English ndo ilikua lugha inayotumika nyumbani. Sina kumbukumbu ya kujifunza hii lugha.
 
kama huyu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…