Siku ya Kwanza Kuongea Kiingereza mbele ya Kadamnasi kidogo nizimie

Siku ya Kwanza Kuongea Kiingereza mbele ya Kadamnasi kidogo nizimie

Mi nakumbuka siku nimeenda interview ya kwanza pale CRDB azikiwe mwaka 2003 nilikuwa natetemeka huku sauti (KUPAYUKA kama vile napiga Adhana ya alfajiri msikitini) mpaka Human resource officer/manager akaniambia Relax ndugu hii si vita!

Yaani nikikumbukia hii interview nakua mdogo kama piriton. Sasa sijaelewa enzi zile ni kwamba ulimi ulikuwa mzito au nili-panic tu na mambo ya interview daah!

Aprili, 2016
Wadau baada ya pale nilifanya jitihada binafsi ikiwemo kusoma sana magazeti ya kiingereza (Daily News, vitabu na kuangalia news za kiingereza tu hasa BBC, CNN na Al-jazeera) sasa natema YAI kwa kiwango cha kujiridhisha, yaani naweza unganisha sentensi nikaeleweka na mwingereza! inshort, hata nikihojiwa na TV za kimataifa sihitaji sub-title kwenye screen. Slaying imenyooka!
 
Jamani kidhungu mkisikiage tu kwa watu ni kirahisi ukimsikia MTU anasema ngoja iwe zamu yako.Nakumbuka enzi zile Mbeya day sec school nikiwa form one,kulikuwa na mambo ya Ballotspeech 'morning talk'Basi bwana huku na kule bila kutegemea wala kuambiwa mapema eti nikachagulia kuwa Kiongozi Wa Morning talk ya kila siku,nilipoitwa jina tu kwanza mwili uligoma ukizingatia kwa wakati huo kulikuwa na Ticha mmoja Mnoko sana Mwakasala....jamani bada ya kufika mbele nikajikuta nasema my name is... My name is....my name is ..kama Mara kumi wkt Mimi ndo nilitakiwa kuwa mfano Wa kuongea na si kwamba nilikuwa sijui ila kiingereza mbele za watu halafu for the first time it real shocked me,kilichokuja kunitesa ni bada ya hapo wanafunzi ikawa ndo salamu yao sasa my name is... na ukizingatia nilikuwa MTU maarufu sana.Ilinisumbua.
 
Ndugu Hello pole sana aisee, sasa baada ya pale vipi ulifanya jitihada zaid ya kupata confidence ya kuongea kiingereza mbele ya kadamnasi?
 
Niliipata baada ya pale na woote waliokuwa kimbelembele kunifanyia dhihaka walijuta kila asubui lazima niwachague waongee.
 
Siku moja tupo kwenye seminar ya koz moja inaitwa rural agricultural economy maarufu kama YELLOW BOOK kwa waliosoma SUA wataelewa, basi picha moja ilikua imebandikwa ukutani ikapulizwa upepo ikadondoka chini jamaa kule mbele akiwa na maiki alisema "what is that, ooh the picture drop down without becouse" basi tulicheka sana

hahahaaa
 
Imenigusa hii mada.mimi nakumbuka ilikuwa form two,nikachukua form ya kugombea uprifekti sasa ishu ikaja kujinadi mbele ya hadhira kwa kiingereza jasho lilinitoka sikujua hata limetoka wapi huku naona kizunguzungu nilichanganya kikwetu na kiingereza sijui kama walinielewa.
hii simple sema peopleeees.!
peopleeees!!! afu unamalizia na thank u.! unarudi kukaa!
 
Kwenye ukaguzi wa usafi kila jmosi Secondary kiongozi anamkaribisha Mwl Kwa ajiri ya inspection yeye ikamtoka "welcome for suspension Sir"
 
lugha hii ya kiingereza ni mtihani kwa asilimia kubwa ya wabongo hususani pale inapolazimika uongee mbele ya kadamnasi (wasikilizaji) badala ya kufikiria content (cha kuongea) unafikiria aibu utakayopata kwa kuvunja/kuchapia kiingereza
 
english-medium schools kwa watoto wetu ndo ukomboz wa kuepeukana na aibu hii. Sasa tulivyo wa ajabu tunashangilia "ELIMU BURE" duniani hakunaga bure mtalipa tu "in kind" baadae likiwamo hili la kutokujua lugha adhimu ya kiingereza maana si mnajua walimu wenyewe wa Kayumba full FAILURES kiingereza nacho mgogoro wanaishia kuuzia watoto wetu ubuyu huko madarasani badala ya kufundisha
 
Siku napresent kwa mara ya kwanza ilikuwa ni shughuli pevu, chuoni hiyo mbele ya watu kama 80 hivi! Cha kushangaza kama sio presentation wakati tukiwa kama 30 mpirani kupiga tizi kwa kiswahili napiga hotuba hata dk 20, ilikuwa ikigeuzwa ngeli tu naweza kuwa bubu! Alafu lecturer wangu alikuwaga noma, hataki usome, basi ni full lugha gongana. Unajikuta unaongea dk 3 maneno yameisha unajikuta umetamka Manchester united kwenye presentation bila kujua.
Ila alhamdullilahi, nilijimix na wanaokijua nikawa baadae tunajipanga wenyewe madenti kama kumi hivi tunapiga videbate na kujiongelesha kizungu, pia kuangalia movi, kina cnn, documentary za mbele imesaidia sana! Sasa hivi ni mwendo mdundo kwenye kuongea, ile stage fear haipo, ingawa stage fear inakuja kutokana na audience yako ni kina nani, ila kwa ujumla mambo kwa sasa yako poa!
Ila nina shida kidogo kuwasikiliza vizuri waingereza wa LANCASHIRE. Accent yao lazima nitulie ndo niwaelewe vizuri.
St. Kayumba ni shida!
 
kuna msela wetu mmoja wakati wa presentation alikuwa lazima ashikwe na kikohozi...yaani kila baada ya maneno mawili utackia,koh koh koh,mmgh!basi alikuwa akifika tu kwenye podium pale mbele madent tunaanza kukatika mbavu kwanza,ila wanagrup wake walikuwa wanampangia kajipande kidogo tu as walikuwa wanajua atawachukulia muda mwingi kwa kikohozi chake cha kiingereza...
 
kiingereza ni kitu cha ajabu sana aisee yaani kikiona Kadamnasi mtu unapata ubarid/kigugumizi ghafla
 
Siku moja tupo kwenye seminar ya koz moja inaitwa rural agricultural economy maarufu kama YELLOW BOOK kwa waliosoma SUA wataelewa, basi picha moja ilikua imebandikwa ukutani ikapulizwa upepo ikadondoka chini jamaa kule mbele akiwa na maiki alisema "what is that, ooh the picture drop down without becouse" basi tulicheka sana
Hahahaaa......nimecheka mpaka kamkojo kamenitoka.
 
Back
Top Bottom