Siku ya mtoto wa Afrika; Je, mtoto yu wapi na anafanya nini?

Siku ya mtoto wa Afrika; Je, mtoto yu wapi na anafanya nini?

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2018
Posts
17,499
Reaction score
25,295
Wasalaam.

Leo tumeazimisha siku ya mtoto wa Afrika . Bila shaka wapo waliotengeneza kofia na mafulana yao kusherehekea siku hii adhimu kwao, kama kweli wapo waliokimbilia kwenye radio, televison na mitandao kuazimisha siku hii kwao.

Lakini swali la kujiuliza ni moja nalo ni huyu mtoto wa Africa ni nani na yupo wapi?
  • Je, Ni yule aliyepo Mererani akichimba madini?
  • Je, Ni yule anayelala nje Kariakoo kama mtoto wa mtaani?
  • Je, Ni yule anayesoma kayumba huku akiambiwa asome sayansi bila hata kuwa na mwalimu bandia wa somo husika.
  • Je, Ni yule anayesoma sant JOHN akila na kusaza huku likizo anakwenda ulaya kuwatembelea ndugu wengine.
Kweli siku ya mtoto wa Afrika inawagusa watawala hata kutunga na kutengeneza mikakati ya kuwasaidia?

Watoto wanahudumiwa na wizara ya afya na nini sijui jina refu mbwembwe tu. je idara ya ustawi wa jamii ina bajeti ya kutosha kuwahudumia watoto husika mfano AFISA USTAWI WA JAMII analo fungu la kibajeti kuwahudumia watoto? jibu ni hakuna.

Je, ofisi ya kamishina inameno na uwezo wa kuwahudumia watoto au mpaka kwa hisani ya wamarekani na waingereza?

Maswali ni mengi kuliko majibu. Kuna haja ya kuazimisha siku hii sasa?
 
Back
Top Bottom