Siku ya pili sasa familia Mdude Nyagali ipo kwenye maumivu makali

Pantosha

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
869
Reaction score
1,282
Hii hali ya kuteka, kutesa na kupoteza watu ni torture kubwa sana kwa ndugu wa mtu aliyetekwa na kupotezwa. Najaribu kujiweka kwenye nafasi ya ndugu zake Mdude, aisee ni maumivu makali sana wanapitia ndugu zake.

Kwa kosa gani kijana mdogo yule atendewe aliyotendewa?

Kwa kosa gani alilolifanya Mdude, familia yake wapitie psychological torture?

Yuko wapi wa kukemea huu uovu?

Ni raha gani mtu unaipata kuongoza watu wasiokuwa na upendo na huruma?

Naamini ni busara rais kukemea haya maovu.
 
Nimemuwaza mtu mmoja humu, alikuja kuweka uzi akimuonya hakimu, aliyewafanyia mabaya kwenye kesi yao. Alimpa mpaka Jumatano, yule hakimu alifariki. Toka siku hiyo, mtoa uzi naye hakuonekana. I wish aje atusaidie sasa na hawa wenye madaraka ya damu.
 
Nitag kwenye huo uzi dada angu..
Muhimu sana
 
Mdude kupatina ni -5%, mpaka sasa naamini hatupo naye, hawa jamaa walivyokana jana nikajua tayari wameshakatisha uhai wake
 
Nimemuwaza mtu mmoja humu, alikuja kuweka uzi akimuonya hakimu, aliyewafanyia mabaya kwenye kesi yao. Alimpa mpaka Jumatano, yule hakimu alifariki. Toka siku hiyo, mtoa uzi naye hakuonekana. I wish aje atusaidie sasa na hawa wenye madaraka ya damu.

Duuuh ,true story? Weka uzi huo tuupitie ,je nani alithibitisha kifo cha huyo hakimu?
 
Nimemuwaza mtu mmoja humu, alikuja kuweka uzi akimuonya hakimu, aliyewafanyia mabaya kwenye kesi yao. Alimpa mpaka Jumatano, yule hakimu alifariki. Toka siku hiyo, mtoa uzi naye hakuonekana. I wish aje atusaidie sasa na hawa wenye madaraka ya damu.
Hakimu wa mahakama ya Ilala hakumaliza siku 7😂
 
Back
Top Bottom