Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Wiki hii nzima, nimekuwa jijini Dodoma kuhudhuria mikutano 3 muhimu ya mambo ya habari. Tulianza na Mkutano Mkuu wa 13, wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, TEF, Mgeni rasmi ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dotto Biteko. Ukaja Mkutano wa Baraza la Habari Tanzania, MCT, mgeni Rasmi ni Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, na Ijumaa tukaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa habari, Mgeni Rasmi ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Hivyo mimi kama kawa na zile makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, zenye swali, maelezo, kisha jibu, utatoa wewe msomaji mwenyewe. Hoja ya leo ni Siku ya Uhuru wa Habari Tanzania, Je kuna Uhuru wa Habari, Bila Uhuru wa Kiuchumi wa Media/Waandishi wa Habari?. Mtu mwenye njaa anaweza kuwa huru?. Media yenye njaa inayomtegemea source kwa usafiri na waandishi wa habari wenye njaa na umasikini uliotopea, kiasi cha kutegemea zile bahasha, wanaweza kuwa huru?!.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi na watendaji wa Serikali waondoe ukiritimba kwenye suala la upatikanaji wa habari ili kuwawezesha wanahabari kupata taarifa sahihi na kufanya kazi zao kwa ufanisi.
“Viongozi na Watendaji wa Serikali na Mashirika zingatieni Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa ya Mwaka 2016 na ondoeni ukiritimba katika suala la upatikanaji wa habari ili wanahabari wawezeshwe kupata taarifa sahihi na wafanye kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu,”
Japo sheria ya upatikanaji taarifa imefungua milango ya upatikanaji habari ni haki, lakini ukiritimba kwenye kanuni za Utumishi wa umma kuhusu utoaji habari uko pale pale, Wasemaji wa Serikali ni zuga tuu kama matarishi, badala ya kuwa wasemaji rasmi wa taasisi zao, wengi ni watoa taarifa tuu, yaani Press Release, lakini kikanuni wasemaji wakuu ni Watendaji wakuu na sio Wasemaji. Ukiritimba huu uondolewe kwenye kanuni, wasemaji wa serikali waisemee serikali na taasisi zake.
Kuhusu habari za uchunguzi, Waziri Mkuu amesema uandishi wa habari hizo unahitaji rasilimali fedha za kutosha ili kutoa mafunzo na kuifanya kazi yenyewe. “Niwaombe wadau wote muhimu wakiwemo taasisi, asasi za kiraia na mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi washirikiane na vyombo vya habari katika kufanikisha utafiti na uandishi wa habari za uchunguzi na kuvisaidia vyombo vya habari kukua kitaaluma na kiuchumi.”
Hili ni eneo muhimu sana ambalo vyombo vyetu vya habari vinashindwa kutokana na kukabiliwa na ukata mkubwa wa rasilimali fedha, hivyo hakuna uhuru wa habari bila uhuru wa kiuchumi wa vyombo vya habari.
Waziri Mkuu amewahimiza wanahabari wote wazingatie uzalendo, weledi na maadili ya taaluma ya uandishi kwa kutoa mchango chanya kwa jamii kwani wasipofanya hivyo tasnia hiyo inaweza kuwa chanzo cha kufifisha maendeleo na hata kuhatarisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa, hili ni jambo muhimu sana.
Waziri Mkuu amesema vyombo vya habari vinayo nafasi kubwa ya kuitangaza nchi pamoja na kuijengea taswira chanya kimataifa na kuwapongeza wanahabari kwa kazi wanayoifanya ya kuuhabarisha umma.
“Vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa katika kuhamasisha uwekezaji, kutangaza vivutio vya utalii na kuchangia katika kuinua uchumi wa Taifa letu. Kwa niaba ya Serikali na wananchi wote wa Tanzania ninavipongeza sana vyombo vyetu ya habari kwa kazi kubwa inayofanywa katika kuutumikia umma.”
Akisisitiza umuhimu wa vyombo hivyo, Waziri Mkuu amesema vina mchango mkubwa wa kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika shughuli na utekelezaji wa mipango ya Serikali pamoja na kampeni muhimu za kitaifa.
“Waandishi wa habari wana nguvu ya kuongeza sauti kwa jamii kuhusu mmomonyoko wa maadili, athari za kimazingira, kufichua rushwa na uzembe na kuunga mkono masuluhisho yatakayochochea maendeleo endelevu na ustahimilivu katika maeneo muhimu.
Kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kwa mwaka 2024 inasema: “Uandishi wa Habari na Changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi.”
Mapema, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, alisema hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini imeimarika ikilinganishwa na ilivyokuwa awali.
“Hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini inaendedelea kuimarika. Bado hatujafika tunakotaka kwenda lakini kwa hakika hatupo tulipokuwa jana. Tumefika hapa kutokana na juhudi za Mheshimiwa Rais, tumetekeleza 4R za Mheshimiwa Rais na ndiyo maana tuko hapa tulipo,” alisema.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo mabalozi wa Marekani, Uswisi, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, UNESCO, Asasi za Kiraia, Wawakilishi kutoka Muungano wa Klabu 28 za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Jukwaa la Wahariri na wanavyuo.
Wiki Ijayo nitawaletea Mkutano wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, TEF.
Paskali