Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,641
- 11,958
Habari wana Jamvi.
Kwanza nimshukuru Mungu kwa kutupa uzima tena hadi wakati huu. Mambo mengi yametokea katika wiki hii lakini cha muhimu tuko hai basi tumshukuru Mungu.
Nikienda kwenye mada moja kwa moja ni kwamba, katika wiki hizi mbili kuelekea siku ya leo ambayo ni siku ya UKIMWI duniani kumekuwa na taharuki kubwa hususani hapa JF.
Mada za UKIMWI zimekuwa nyingi na huku shuhuda mbalimbali zikitolewa kueleza namna watu wanavyo ukwaa ugonjwa huu hatari huku wengine wakieleza jinsi wanavyomudu maisha wakiwa na maambukizi.
Lakini jambo nililo ligundua ni hili, kwamba mada hizi zimeletwa makusudi kabisa kwa lengo la kuleta Taharuki kwa watu katika siku hii muhimu duniani, ili kuvuta macho na masikio ya watu wengi waweze kuamka usingizini wajue kuwa UKIMWI upo na wasijisahau.
Kwa kiasi kikubwa hili limefanikiwa sana Mana asilimia kuwa ya wana JF tumejikuta tukifuatilia kwa karibu mada hizi huku baadhi wakiwa na woga mwingi labda kutokana na rafu walizo cheza hapo kabla.
Hii inatupa picha kuwa.
1. Hapa jukwaani walio wengi wamejisahau sana na kuto kujali afya zao na vitendo vya zinaa kuongezeka kwa wingi.
2. Ngono zembe limekuwa ni tatizo kubwa sana kwa sasa, walio wengi wamesahau kabisa matumizi ya kinga linapokuja suala zima la mapenzi, pia hawajali afya zao na wenza wao na kupima ili kujiridhisha.
Nje ya JF pia kuelekea siku ya UKIMWI duniani mashirika tofauti tofauti yametoa takwimu zinazoonyesha kuongezeka kwa kasi ya maambukizi hasa kwa vijana wa miaka 18 - 25.
Hivyo basi kuwapo kwa mada hizi nyingi ni njia mojawapo iliyoletwa kwa makusudi kuwakumbusha watu kuhusu uwepo wa gonjwa hatari la UKIMWI.
Hapa JF wengi wamekuja na ID mpya na kutunga story nyingi za kuogovya ili kuleta Taharuki kwa watu kwa makusudi kabisa.
Nyingi katika mada hizo hazikuwa na ukweli wowote ila tu zilikuwa na lengo fulani na kweli lengo limefanikiwa.
Mwisho, nawaomba wana jamvi punguzeni hofu mlizonazo lakini sasa uwe ni mwanzo mpya kuchukua hatua katika kujali na kulinda afya zetu, usimuamini mtu yoyote yule, siku zote amini kuwa kila mtu ana UKIMWI isipokuwa wewe tu ndio huna, lakini pia licha ya UKIMWI bado kuna magonjwa mengine mengi ya zinaa ambayo ni hatari kwa maisha yetu. Hivyo tafakari na uchukue hatua.
Kwa wale mabaharia wanaokula matunda ki masihara sasa ni wakati wa kuacha kuyala kwa masihara bali myale kwa makini kwasababu mkiyafanyia masihara hayo matunda mjue kabisa kuwa UKIMWI utawafanyia masihara pia na mtakwenda kaburini kimasihara kabisa na mtawaacha watoto na wapendwa wenu wakiwa yatima kimasihara kabisa.
Muwe na amani wakuu, amani na irudi tena JF kama hapo awali.
Ahsanteni.