Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Leo ni Siku ya Wanawake Duniani, katika safari ya kuelekea usawa wa kijinsia, kuna wanawake wengi wenye sifa na uwezo, lakini wamenyimwa fursa za kushika nafasi za juu kisiasa kutokana na nyingi ya nafasi hizo, kuhodhiwa na wanaume, katika kitu kinachoitwa "mfumo dume!"
Swali ni je, nafasi hizo za juu kisiasa zimeshikwa na wanaume kwa sababu hatuna wanawake wenye sifa, au zimeendelea kushikwa na wanaume kwa sababu ya mfumo dume tuu, nikimaanisha wanawake wenye sifa wapo, lakini hawajateuliwa kushika nafasi hizo?
Kufuatia kilio cha muda mrefu cha wanawake kunyimwa fursa, je ni kweli tunao wanawake wenye sifa na uwezo wa kutupeleka kwenye 50/50?. Hebu na tuanzie na wanawake wenye sifa za urais, je tunao?
Hebu tuwakumbuke the top ten female politicians in Tanzania, na nafasi wanazoshika! Je, wamefikaje hapo, kwa kupanda wenyewe, au wamebebwa ndipo wakafika hapo? Je, wana sifa za urais?
Natoa wito kwa wanawake, kama ni kweli mna uwezo, jitokezeni kwenye urais, ili hata msiposimamishwa, angalau 2015, tuwe na makamo rais mwanamke, au Waziri Mkuu Mwanamke!
Paskali.

- Top No.1 ni Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Huyu mama ni very powerful in Zanzibar na miongoni mwa wanawake wachache wa shoka kutoka Zanzibar. Ni Mjumbe wa CC na NEC wa CCM.
Very high profile woman from Zanzibar, baada ya kuhudumu kwa miaka 10 kwenye Baraza la Wawakilishi, ameingia Bunge la JMT for 5 years sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamo wa Rais. Ndiye alikuwa Makamo Mwenyekiti wa Bunge la Katiba. Huyu ni presidential material, sasa ni kumuandaa kwanza kuwa rais wa Zanzibar kwa kumpumzisha Dr. Shein kipindi chake cha pili, kisha 2020 aje urais wa Muungano, ili hili ifanyike, itabidi, CCM iachane na ule utaratibu wake wa two terms za urais, kwasababu kusubiria 2025, kwa huyu mama itakuwa too little too late, age itakuwa imemtupa mkono. - Gutrude Mongela-Huyu alikuwa Mwenyekiti wa ule mkutano maarufu wa Wanawake wa Beijing, na Spika wa Kwanza wa Bunge la Afrika. Huyu pia ni Mwanamke wa shoka. Yeye alifika kote huko kwa deserving. Ni presidential material, ila kwa siasa zetu za Tanzania, she is already a spent force!, age sio rafiki.
- Mhe. Anna Makinda- Huyu ni Spika wa Bunge la Tanzania- ameupata usipika kwa kubebwa na mbeleko ya jinsia, ukimlinganisha na spika Sitta aliyemtangulia, Mama Makinda anaonekana wazi amepwaya kwenye Uspika!, lakini likija suala la Urais wa JMT, Mama Makinda ni presidential material, anauweza sana urais, kwa sababu ni mtu mwenye msimamo usioyumba!. Maamuzi ya ki Raisi wa nchi, hayahitaji mijadala kama maamuzi ya Bunge, hivyo Mama Makinda ni predidential material.
- Dr. Asha Rose Migiro- Huyu ni top most high profile woman from Tanzania kwenye International arena, ni mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Deputy SG wa Umoja wa Mataifa akimsaidia Ban Ki Moon, kwa sasa ni mjumbe wa CC ya CCM, na waziri wa sheria wa Tanzania. Amefika kote alikofika kwa deserving ya brain power, ndio the one and only female kupata 1st Class ya Sheria ya UDSM!. Lakini tukija kwenye u presidential material, she is presidential material interms of brain power, but she lack Presidential drive, anachotakiwa kufanya sio kusubiri Chama ndio kimpush, anatakiwa kuonyesha nia na kujitokeza, sio lazima kutangaza kuwa anautaka urais, ili asije kuingia vitani na wasaka urais, bali kujitokeza hadharani kusema yeye ni presidential material, ana sifa na uwezo, wakati wa kutangaza ukifika, atafikia maamuzi au atangaze kujitupa kwenye kinyanganyiro au laa!, na sio kukaa kimya kuisubiria mbeleko ya CCM kubebea watu kwa utaratibu ule wa "sasa ni zamu ya mwanamke!".
- Prof. Anna Tibaijuka
- Anna Abdallah
- Mary Nagu
- Hellen Kijo Bisimba
- Dr. Stagomena Tax Bamwenda
- tuendelee kuwataja wengine.
Natoa wito kwa wanawake, kama ni kweli mna uwezo, jitokezeni kwenye urais, ili hata msiposimamishwa, angalau 2015, tuwe na makamo rais mwanamke, au Waziri Mkuu Mwanamke!
Paskali.