Wanabodi,
Leo ni Siku ya Wanawake Duniani, katika safari ya kuelekea usawa wa kijinsia, kuna wanawake wengi wenye sifa na uwezo, lakini wamenyimwa fursa za kushika nafasi za juu kisiasa kutokana na nyingi ya nafasi hizo, kuhodhiwa na wanaume, katika kitu kinachoitwa "mfumo dume!"
Swali ni je, nafasi hizo za juu kisiasa zimeshikwa na wanaume kwa sababu hatuna wanawake wenye sifa, au zimeendelea kushikwa na wanaume kwa sababu ya mfumo dume tuu, nikimaanisha wanawake wenye sifa wapo, lakini hawajateuliwa kushika nafasi hizo?
Kufuatia kilio cha muda mrefu cha wanawake kunyimwa fursa, je ni kweli tunao wanawake wenye sifa na uwezo wa kutupeleka kwenye 50/50?. Hebu na tuanzie na wanawake wenye sifa za urais, je tunao?
Hebu tuwakumbuke the top ten female politicians in Tanzania, na nafasi wanazoshika! Je, wamefikaje hapo, kwa kupanda wenyewe, au wamebebwa ndipo wakafika hapo? Je, wana sifa za urais?
- Top No.1 ni Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Huyu mama ni very powerful in Zanzibar na miongoni mwa wanawake wachache wa shoka kutoka Zanzibar. Ni Mjumbe wa CC na NEC wa CCM.
Very high profile woman from Zanzibar, baada ya kuhudumu kwa miaka 10 kwenye Baraza la Wawakilishi, ameingia Bunge la JMT for 5 years sasa ni VP kumuandaa ama kuwa rais wa Zanzibar kisha kuja bara, au kumpumzusha JPM 2020
Paskali.