Japo mimi niko kwenye lile kundi linalosisitiza Samia asipangiwe, aachwe afanye vile anaona inafaa, lakini kuhusu huu uteuzi usiozingatia kabisa gender balance, honesty, I don't believe huyu ni Samia huyu niliye zungumza hapa!.
Wanabodi, Leo asubuhi nimeangalia kipindi cha mahojiano ya Makamo wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumzia Siku ya Wanawake Duniani kwenye TBC akihojiwa na Shabani Kissu. Kwa Waliosikiliza kipindi hiki, kiukweli huyu ni mwanamke wa kupigiwa mfano, mtanisamehe sina maneno ya Kiswahili ya...
Jee inawezekana Tanzania ni hatuna wanawake wa kutosheleza gender balance?, au wapo wamesahaulika?.
Kama tuna wanawake wenye sifa hadi za urais, tunakosaje wanawake wa kutosha wenye sifa za kubalance gender balance?.
P
Wanabodi,
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...
Kila nipatapo fursa, nitakuwa naendeleza zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo zina lengo la kusaidia nchi yetu, serikali yetu na viongozi wetu. Makala ya leo ni swali tuu, ni hoja na swali.
Hoka ni "Kufanya Kosa Si Kosa, Kosa Kurudia Kosa", tangu rais Samia ashike usukani, jana ndio uteuzi wake mkubwa wa kwanza wa viongozi wengi kwa mpigo. Kwa maoni yangu, kwenye uteuzi huu, nina swali, "Jee ni Kweli Tanzania Hatuna Wanawake wa Kutosha Wenye Sifa za Uongozi Kustahili Uteuzi?. Kwa maoni yangu uteuzi huu una walakin, ila Rais Samia hajafanya kosa lolote, bali tukubali, tukatae, kule nyuma, kuna makosa yalifanyika. Sasa ni jukumu letu sisi tuliibahatika kuyaona makosa hayo ya nyuma, ambayo Rais Samia ameyarithi, tumsaidiwe, rais Samia, kwa kuyataja makosa hayo, ili rais Samia asirudie makosa ya nyuma, kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa, kwenye maa RC kuna kosa la gender balance, kwa vile wanakuja ma RAS, wanakuja ma DED, wanakuja ma DC, wanakuja ma DAS, tumsaidie Tanzanite Lady wetu, Mama Samia, huko mbele, tusirudie makosa!.
Kosa lenyewe ni jibu la swali hili, " hivi ni kweli kabisa, Tanzania hatuna wanawake wenye sifa, wa kutosha kufikia 50/50 ya gender balance kwenye nafasi za uteuzi?.
Kabla haujasoma hoja za bandiko hili, naomba nikupe homework ndogo ya kusoma bandiko langu hili
Kwa vile Mama Samia amejitanabaisha wazi yeye ni kama JPM, kwenye upande wa uteuzi wa JPM, we had gender problem!.
Uteuzi wa JPM, Kwa mfano idadi ya mawaziri wanawake ni 4 tu kati ya 19, hii ni asilimia 21%. wanaume ni asilimia 79%. Kwenye Baraza la Mawaziri la Samia, lina mawaziri 25, wanawake ni 6 ambao ni asilimia 24% wanaume 19 ambao ni asilimia 76%. Hivyo hapa gender imbalance imeendelezwa!.
Kwenye uteuzi wa Wakuu wa Mikoa, kati ya wakuu wa mikoa 26 wa Magufuli, wanawake ni 4 tu ambao ni asilimia 15% wakati wanaume ni 21 ambao ni asilimia 85%!. Sasa rais Samia anapita mule mule, alikopita JPM kwenye uteuzi wa wakuu wa mikoa wa Samia ameteuwa ma RC wanawake 4 tu kati ya ma RC 25, hii ni asilimia 16% ndio wanawake na wakati wanaume ni 21 ambao wanafanya asilimia 84%!.
Kwenye wakuu wa wilaya, kati ya wakuu wa wilaya 134 wa Magufuli, wanawake ni 25 tu ambao ni asilimia 18%, wakati wanaume ni 109 ambao ni asilimia 82%. Na kwa upande wa Wakurugenzi, kati ya wakurugenzi wa halmashauri na wilaya 185 wa Magufuli, wanawake ni 33 tu!, ambao ni asilimia 17% tuu, wanaume asilimia 83%.
Kwa trend reading, kama ni kweli kabisa Samia ni kama Magufuli, then you know what to expect, kwenye uteuzi wa ma DC na Wakurugenzi. Hili ni kosa, lisiachwe liendelee!.
Hii maana yake, kati ya Watanzania milioni 60, ni kweli hakuna wanawake capable wa kutosha kuteuliwa kuwa ma RC, ndio wamepatikana hao 4 tuu!. Is this so?!.
Conclusion.
Kwa vile hatukumpangia JPM nini cha kufanya, hivyo nilisisitiza tangu mwanzo, tusimpangie Samia, lakini huku kutompangia Samia, hakumaanishi tunapoona mapungufu mahali, au mambo yanakwenda ndivyo sivyo, tunawajibu wa kumshauri ili kumsaidia. Katika safari ya kuelekea gender balance ya 50/50 katika uongozi, mimi siamini kuwa Tanzania hatuna wanawake wa kutosha hadi uteuzi wa wanawake uwe that low.
Kwa fikra zangu, Naamini uteuzi huu wa ma RC ni mama Samia, ameendelea kubeba some luggages na baggages za mtangulizi wake. Hilo ni kosa!. Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa!. JPM alifanya kosa kwenye gender balance.
Gender balance kwenye baraza la mawaziri hatuwezi kulaumu, kwasababu ili mtu uwe waziri ni lazima kwanza uwe mbunge, ikitokea hakuna wanawake wa kutosha kujaza nafasi za kufikia kiwango cha 50/50, hili litaeleweka, kwasababu Mama Samia, ameingia na kuwakuta wabunge tayari wapo, ikitokea wabunge wote hadi wa viti maalum, hawana sifa za uwaziri, hatuwezi kulaumu, kwasababu sio kosa lake. Huwezi tuu kujiteulia watu hawana sifa ili tuu kutimiza gender balance. Lakini kwenye ma RC, ma DC , ma RAS, ma DAS ns na DED, yaani Wakurugenzi, haiwezekani Tanzania ndani ya hii milioni 60, wakakosekana wanawake wenye sifa.
Naamini rais Samia, kaletewa majina na kuongeza wachache tuu, hivyo sasa tunamuomba, kwenye ma DC, ma RAS, ma DED na ma DAS, awatendee haki wanawake wa Tanzania.
Nisimalize bila kumpongeza Mama Samia kwanza kwa ku heal the nation kwa kutenda haki, na pili ni pongezi kwa kuyaishi maneno yake ya kuteua yoyote hata kutoka upinzani.
Tanzania ni yetu sote,
Mungu mbariki Mama Samia.
Mungu ibariki Tanzania.
Paskali