Mhe makamu wa Rais siku ya wanawake hujaitendea haki!
Katika mazingira ambayo Tanzania ingesimama na Makamu wa Rais basi ni siku ya leo,siku ya wanawake.
Mama usoni unaonekana muungwana na mwenye huruma kiasi kwamba unanishawishi niamini kwamba moyoni huridhishwi na yanayoendelea nchini.
Mhe Makamu wa Rais,kuna sehemu nataka nikukumbushe kwamba wewe haupo ikulu kuunga mkono tu jitihada za Rais tu ila upo pia kudhihirisha uwezo wako wa kiuongozi Mungu aliokujalia,haupo kuunga mkono jitihada za wanaume tu, upo Ikulu ili kupishana kimawazo na Rais ili kujua jambo gani sahihi la kutekeleza kwa wananchi.
Onyesha kwa mabinti walioko mtaani na wale waliopo shuleni na vyuo vikuu kwamba hukufika hapo kutokana na kutafuta usawa wa kijinsia isipokua uwezo wa kiuongozi uliojaaliwa na Mungu,Fanya hivyo tuwaone akina Samia Suluhu wengine baada yako.
Mhe Makamu wa Rais, sikulazimishi ila fanya kadri utakavyoona inakufaa.
Simama katika nafasi yako vizuri udhihirishie UMMA wa Watanzania kuwa unaweza kuwa mshauri wa Rais kama cheo chako kilivyo.
Heri ya siku ya wanawake.
Elia F Michael.
Diwani Gwarama.
Mwenyekiti wa madiwani wa CHADEMA kanda ya Magharibi.
08/03/2018.