Siku za kifungo Jela zinahesabikaje?

Siku za kifungo Jela zinahesabikaje?

Huku Mozambique raha sana
Kila rais anapoingia madarakani wafungwa wote huachiwa huru
 
Naomba kuuliza swali kupitia uzi huu nimegundua wajuzi wengi.
Je mtu akituhumiwa kesi ya mauaji au yeyote ile kubwa.Akakaa gerezani miaka5.Baadae akaonekana hana hatia akaachiwa.Je ana haki ya kudai fidia kwa usumbufu alioupata?na je atamdai nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu huku hata ukiua,ukitoa pesa isiyozidi hata tsh 1.5mil unatoka kiboss
Makosa mengine madogo kama wizi unatoka hata kwa tsh laki 1 tu
Kwa hiyo utaona kuwa wengi wa wafungwa ni wale wasiojiweza au ndugu zao wameamua iwe hivyo kutokana na kuchokwa na matendo yao ya kiharifu. Vinginevyo kinachoangaliwa ni pesa tu
 
Hivi ukifungwa mahakam huwa inafatilia kama Unatumikia adhabu kweli?????[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa zamani, sasa hivi ukikaa mahabusu miaka sita ukahukumiwa sita unaitumikia, ninyi mnaojifanya wanasheria mnapotosha sana clients wenu.
.
Sasa fanya kosa uone.
Hakuna cha kujifanya wanasheria tunazungumzia tunachokifahamu

Kama imebadilishwa ndio useme sio kutupiana kashfa
 
Duh...sijapata jibu bado,naona tunakachanganyana tu.Hakuna mtu mwenye document ya sheria akaiweka hapa tukafanya reference na kujifunza?
 
Hakuna cha kujifanya wanasheria tunazungumzia tunachokifahamu

Kama imebadilishwa ndio useme sio kutupiana kashfa
Boss sijatoa kashfa naheshimu maoni yako.
.
Lakini kuanzia leo tambua nilichokisema! Unachokifahamu sicho
 
  • Thanks
Reactions: T11
Kuna uvumi kama huu kuwa siku za mfungwa akiwa gerezani huwa zinahesabiwa usiku na mchana kama siku mbili tofauti!! Lakn ukweli ni kuwa siku hizi huhesabiwa kama kawaida yaan usiku na mchana inakuwa siku moja!!! Kwa hiyo mfungwa akihukumiwa kifungo cha miaka 30 atatumikia miaka thelathini kama ilivyo!! Kwa nn watu huzani kuwa siku huhesabiwa kuwa usiku na mchna ni siku mbili tofauti!?? Kwa mujibu wa sheria ya magereza sura namba 58 ukisoma kifungu cha 49 pamoja na mambo mengine kinaeleza kwamba mfungwa anayetumikia kifungo gerezani kwa kosa la jinai anaweza akapunguziwa 1/3 ya adhabu yake kutokana na kuonesha tabia njema akiwa anatumikia kifungo hicho!!! Kwa hiyo sasa punguzo hilo la 1/3 la adhabu yake humfanya mfungwa wa kosa la jinai asimalize siku alizoshitakiwa na watu kudhani kuwa siku hizo huhesabiwa kama usiku na mchana kuwa ni siku mbili tofauti!! (fair comment)
 
Bora wewe umejibu kisomi umetuletea na vifungu tusome tunaweza kukuamini
 
Nakumbuka iyo kitu ilikuwaga miaka ya nyuma mpaka katika utawala wa awamu ya nne,ila ilivyoingia awamu ya tano mheshimiwa akaifutilia mbali hukumu iyo ya 1/3,kwani wengi wa wahalifu walikuwa wanaichekelea pale wanapohukumiwa,kwaiyo sasa ivi wanahesabu saa 24 ni sawa na siku moja tu
kipindi kile cha Lulu kuhukumiwa kwnd jela,nilipata kumsikia mkuu wa magereza akieleza kuhusu hili jambo baada ya kuhojiwa na muandishi,na akasema hiyo sheria ipo hata sasa(ya kusamehewa 1/3) na lengo hasa la huo msamaha ni kuwafanya wafungwe wawe na nidhamu,Yaani kama 1/3 yako ni miezi 4,basi kila ukifanya kosa ile 1/3 inapungua ,na inaweza kuisha kabisa kama utakuwa huna nidhamu/mkorofi,ukajikuta unakaa gerezani miezi ile ile uliyohukumiwa
 
Back
Top Bottom