Tetesi: Siku za Ndalichako zehesabika WEMU, TET wanamponza.Aandaliwa kupewa Ubalozi.

Tetesi: Siku za Ndalichako zehesabika WEMU, TET wanamponza.Aandaliwa kupewa Ubalozi.

Umeshaharibu, hatakama alikua na lengo la kumtumbua hatomtumbuwa si unajua apangiwi
 
Ndalichako wa Necta (JK's) akikutana na Ndalichako waziri (JPM's) zitapigwa hatareee
 
NAONA YALE MA STORY YA;

1. Tutalipwa 700m za kishika uchumba na Acacia

2. Mazungumzo kati ya serikali na Acacia kuhusu makinikia yanaendelea vzr.

3. Tumenunua ndege zingine 6 tena kwa kulipa cash.

4. Tunataka tuwe nchi ya viwanda

YAMEPOTELEA HEWANI
 
Haya Kitila Mkumbo, wizara hiyo!
Kwani huyu ni mwanamke? Maji yanapatikana nchi nzima kama mkakati wao wa kisera na ilani inavyoeleza? Kama bado ameshindwa kufikia lengo itakuwaje kwa wizara hii ya elimu iliyozoea kujiongoza yenyewe? Atakuwa na jipya au naye atakuja na yake?
 
Inasemekana darasa la 5, 6 na 7 kwa 2019 hawana kitabu hatA kimoja
 
Rais akishamteua ubunge binadamu yoyote Yule kwa mujibu wa katiba yetu na Alisha kula kiapo Hana Tena mamlaka ya kutengua maamuzi yake Kama madc Rc na wakurugenzi, hii inadhibitisha habari yako hii Ni Ufukunuku...
Hilo limeishafabtika. Katiba ilikiukwa? Posi alifanyiwa hivyo. Sasa ni balozi.
 
Ukitaka kuwatawala watu kirahisi wanyime elimu
 
Profesa mmoja wa saikolojia ya elimu ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara fulani atapewa ubunge na uwaziri wa elimu.
Profesa PEKEE "wa Saikolojia ya Elimu" ambaye ni Katibu wa Wizara ni K. A. K. Mkumbo. (Wizara ya Minze/amazi).
 
UJUMBE KWA PROF NDALICHAKO NA TCU.
TCU ichukue hatua za haraka kuokoa hali kwa wanafunzi vyuo vikuu.

Mtakumbuka hivi karibuni Tume ya vyuo vikuu ilizifuta baadhi ya kozi zinazotolewa na baadhi ya vyuo vikuu Tanzania.
Pamoja na hilo,vipo vyuo vilifungiwa kudahili wanafunzi na vipo vilivyofutwa.
Vyuo vilivyofutwa vililazimika kuwahamishia wanafunzi katika vyuo vingine vinavyotoa kozi zinazofanana na walizokuwa wanazisoma.

Hata hivyo Chuo kikuu cha MOSHI MEMORIAL UNIVERSITY COLLEGE kilifutiwa baadhi ya kozi licha ya kukiacha kiendelee kutoa huduma.

Chakushangaza,Wanachuo waliokuwa wanasoma Bachelor of Arts in public administration and management wamehamishwa chuoni hapo kutokana na kozi hiyo kufutwa,hata hivyo Chuo kimewahamishia wanafunzi Chuo cha USHIRIKA MOSHI lakini chakushangaza ni kuwa Chuo cha USHIRIKA MOSHI hakina degree program waliyokuwa wakiisoma,yaani BACHELOR OF ARTS IN PUBLIC ADMINISTRATION AND MANAGEMENT.

Wanafunzi wa kozi hiyo wameambiwa wasome kozi ya HUMAN RESOUCE MANAGEMENT.

Inawezekanaji mwanafunzi wa kozi ya Arts in public administration and management kwenye chuo kimoja apelekwe kusoma Human resources?

Upo wapi usimamizi wa TCU.

Yupo wapi prof Ndalichako?

Hivi wanafunzi ambao ni wanufaika wa bodi ya mkopo watawezaje kurejesha madeni yao kama kizi wanazosoma ni kozi KACHUMBARI?

Napewa taarifa kuwa vyuo vingi vilivyoagizwa kuhamisha wanafunzi kutokana na kutokidhi vigezo vya kozi husika,vimefanya uhuni dhidi ya wanafunzi.

Vinawapeleka vyuo vingine kimsalagambo.hakuna principle.

Unapewa barua kutoka STEFANO MOSHI UNIVERSITY halafu unaambiwa nenda USHIRIKA MOSHI kwa facult tofauti na uliyokuwa unasoma tangu mwanzo.

Sasa mtu asome Facult moja kwa miaka mitatu hakafu umuhamishe kwenda chuo kingine kwa Facult tofauti na uliyokuwa unasoma tangu mwanzo?

Huu ni uhuni ambao wasaidizi wa Rais Magufuli wanatakiwa kuukemea na kuchukua hatua stahiki,

Rais amejipambanua kuwa mtetezi wa wanyonge,na hao wanafunzi wanaofanyiwa uhuni ndio wanyinge wenyewe.

Share ujumbe huu uwafikie watanzania wengi ili waone jinsi TCU inavyopwaya.
 
Rais akishamteua ubunge binadamu yoyote Yule kwa mujibu wa katiba yetu na Alisha kula kiapo Hana Tena mamlaka ya kutengua maamuzi yake Kama madc Rc na wakurugenzi, hii inadhibitisha habari yako hii Ni Ufukunuku...
Hivi kwa yule naibu waziri Posi, ilikuwaje vile? Tukumbushane!
 
Back
Top Bottom