UJUMBE KWA PROF NDALICHAKO NA TCU.
TCU ichukue hatua za haraka kuokoa hali kwa wanafunzi vyuo vikuu.
Mtakumbuka hivi karibuni Tume ya vyuo vikuu ilizifuta baadhi ya kozi zinazotolewa na baadhi ya vyuo vikuu Tanzania.
Pamoja na hilo,vipo vyuo vilifungiwa kudahili wanafunzi na vipo vilivyofutwa.
Vyuo vilivyofutwa vililazimika kuwahamishia wanafunzi katika vyuo vingine vinavyotoa kozi zinazofanana na walizokuwa wanazisoma.
Hata hivyo Chuo kikuu cha MOSHI MEMORIAL UNIVERSITY COLLEGE kilifutiwa baadhi ya kozi licha ya kukiacha kiendelee kutoa huduma.
Chakushangaza,Wanachuo waliokuwa wanasoma Bachelor of Arts in public administration and management wamehamishwa chuoni hapo kutokana na kozi hiyo kufutwa,hata hivyo Chuo kimewahamishia wanafunzi Chuo cha USHIRIKA MOSHI lakini chakushangaza ni kuwa Chuo cha USHIRIKA MOSHI hakina degree program waliyokuwa wakiisoma,yaani BACHELOR OF ARTS IN PUBLIC ADMINISTRATION AND MANAGEMENT.
Wanafunzi wa kozi hiyo wameambiwa wasome kozi ya HUMAN RESOUCE MANAGEMENT.
Inawezekanaji mwanafunzi wa kozi ya Arts in public administration and management kwenye chuo kimoja apelekwe kusoma Human resources?
Upo wapi usimamizi wa TCU.
Yupo wapi prof Ndalichako?
Hivi wanafunzi ambao ni wanufaika wa bodi ya mkopo watawezaje kurejesha madeni yao kama kizi wanazosoma ni kozi KACHUMBARI?
Napewa taarifa kuwa vyuo vingi vilivyoagizwa kuhamisha wanafunzi kutokana na kutokidhi vigezo vya kozi husika,vimefanya uhuni dhidi ya wanafunzi.
Vinawapeleka vyuo vingine kimsalagambo.hakuna principle.
Unapewa barua kutoka STEFANO MOSHI UNIVERSITY halafu unaambiwa nenda USHIRIKA MOSHI kwa facult tofauti na uliyokuwa unasoma tangu mwanzo.
Sasa mtu asome Facult moja kwa miaka mitatu hakafu umuhamishe kwenda chuo kingine kwa Facult tofauti na uliyokuwa unasoma tangu mwanzo?
Huu ni uhuni ambao wasaidizi wa Rais Magufuli wanatakiwa kuukemea na kuchukua hatua stahiki,
Rais amejipambanua kuwa mtetezi wa wanyonge,na hao wanafunzi wanaofanyiwa uhuni ndio wanyinge wenyewe.
Share ujumbe huu uwafikie watanzania wengi ili waone jinsi TCU inavyopwaya.