Siku zinavyozidi kwenda nazidi kuutilia Shaka uwepo wa Mungu

Usitushirikishe ujinga wako bwana!
 
Dunia sio sehemu salama kwa watu wadhaifu.

Nchi inavyomtuma mwanajeshi vitani mabalaa yote yanayomtokea huko wao hawajui ila wanachosubiri ni ushindi tu, kwahiyo afanye anavyofanya alete ushindi nyumbani tumtunuku ushujaa au aanze kulia lia wakamate kichwa wachinje tumsahau kama aliwahi kuwepo.
 
Habari mchanganyiko, muhimu kutuchanganya
 
Si uona hizi robots sasa zinavyotengenezwa na binadamu ipo siku wataweza kutengenezana wenyewe kwa wenyewe. Watakuwa na mamlaka na uwezo wa kutawala ndio hao watakataa hawakutengenezwa na binadamu kabisa .

Ndio binadamu ambaye mwanzo wake haujui anavyomkataa Mungu hii inatokana na kizazi zaidi kinapopata maarifa ya kutawala ulimwengu, kama ishu za Atheists basi walikuwepo tangu karne ya kwanza.
 
Kuwa na akiba ya maneno kijana
 
Unachofanya unataka kumnyamazisha mtoa mada.
Braza Hoja haipigwi nyundo.

Toa jibu la hoja.....

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Msadie kujibu, maana nimeuliza kulingana na maelezo yake. Kama unaona wewe ndiye mwenye jibu, then jibu maswali yangu na niulize baada ya kuyajibu.
 
Hakuna yeyote anayeweza kuthibitisha uwepo wa Mungu, ila kwa kutazama yatuzungukayo duniani na ulimwenguni, tunashawishika Kudhani kuna designer mmoja au wengi walifanya kazi kutengeneza systems kadhaa zilizopo.
Ni dhana tu, hatuna uhakika.

Uongo ulianzia pale binadamu alipoanza kujifanya yeye ni wakala wa Mungu, mungu kaongea naye na yeye anajua Mungu anataka nini na hataki nini. Hao wote ni waongo wakuu. Maandiko yao ni uzushi mtupu na stori za vijiweni tu.

Hata kama Mungu aliwahi kuwepo au bado yupo, hakuna ajuaye chochote kuhusu nia, uwezo wala matakwa yake.
Wala hajihusishi na maisha yetu ya sasa.

Hawa manabii, wachungaji, masheikh na wengine woooote wanojifanya kujua lolote kuhusu nguvu iitwayo Mungu, ni waongo na wapigaji wakubwa.
 
Ni bora kufuatilia jambo kwa nia ya kujua na si mihemko kinachozngatiwa kwenye uislamu mwanamke kuolewa au mwanaume ni kubaleghe na mwanamke kuvunja ungo na sio miaka ,kwasababu mwanmke akishapevuka tu ashakuwa mkubwa ndio maan anaweza kubeba mimba,

Zinaa allah akakataza ndio maan karuhusu wanaume ambao wanaona kuwa hawawezi kujizuia kuoa,na yule asietosheka na mke mmoja aoe wawili kama bado basi aongeze watu hadi wa 4 kwa kauli yake allah katika suurat al nnisaa aya ya 3

وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا ﴿٣﴾

3. Na mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu kwa mayatima, basi oeni waliokupendezeni katika wanawake (wengine); wawili au watatu au wanne. Lakini mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi mmoja tu au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki.[2] Hivyo ni karibu zaidi kwamba hamtoelemea kudhulumu.[3]
 
Ndivyo nature ilivyo.

Na kila kitu ni part ya nature hiyohiyo.

Kuzaliwa na kufa sio kigezo cha uwepo wa huyo Mungu.
Unazungumza hivyo kwasababu ya afya na uzima ulio nao ila usisahau kuwa walipita watu kabla yako nao walikadhibisha uwepo wa allah kama alivyoeleza katk suurat al qalam

إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ﴿١٥﴾

15. Anaposomewa Aayaat Zetu, anasema: Hekaya za watu wa kale.


Akendelea kusema katika sura hiyo hiyo allah

فَذَرْنِي وَمَن يُكَذِّبُ بِهَـٰذَا الْحَدِيثِ ۖسَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ﴿٤٤﴾

44. Basi Niache (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na anayekadhibisha Qur-aan hii. Tutawavuta pole pole adhabuni kwa namna wasiyoijua.

وَأُمْلِي لَهُمْ ۚ إِنَّ كَيْدِي مَتِينٌ﴿٤٥﴾

45. Nami Ninawapa muhula. Hakika Vitimbi Vyangu ni Thabiti.


Fursa unayo rejea kwa mola wako ewe ndugu yangu mbora kabla allah hajakupa dhahama hapa duniani na kesho akhera kwani ukifa na hali hiyo huna nafasi tena ya kutengeneza rudi kwa allah anasameh madhambi yote
 
Mungu anataka hata kama huna hata mia ushukuru tu kuwa hai na afya. Hata ukiumwa ushukuru tu sabab unaish wengine wamekufa. Hata ukifa ushukuru tu sabab kuna wengine wamekufa kifo kibaya zaidi ya chako. Hata ukifa kifo kibaya ushukuru sabab kuna marehem wenzio hawakuish miaka mingi kama yako...

It's a primitive kind or rationality
 
usimpeleke huko. allah sio Mungu, ni jini tu la kiarabu.
Allah sio jini ni muumba wa hao majin pamoja na binadam na kila kitu kama alivyosema katika Qur an Suurat Al hijir

وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ﴿٢٦﴾

26. Na kwa yakini Tumemuumba binaadam kutokana na udongo wa mfinyanzi mkavu, unaotoa sauti, unaotokana na tope nyeusi iliyotaghayari.

وَالْجَانَّ خَلَقْنَاهُ مِن قَبْلُ مِن نَّارِ السَّمُومِ﴿٢٧﴾

27. Na majini Tuliwaumba kabla kutokana na moto ulio mkali mno.


Kwahiyo hata wewe inakupasa urudi katika dini ya haqqi (uislamu) huyo yesu atakuja kuwakana siku ya qiyama kama ambavyo allah amesema kweny suurat maida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…