Sikubaliani na Profesa Janabi

Sikubaliani na Profesa Janabi

Kama vile ilivyo kwenye haja kubwa kuwa unapobanwa na haja halafu ukajibanabana madhara hutokea mwilini, ndivyo hivyo hivyo hata kwenye njaa. Usipkula unaposikia njaa, mwili utakula baadhi ya cells ama tissues zake ambazo zilikuwa zikifanya kazi nyingine hivyo kupelekea madhara kutokea.
Hili mboni amelielezea nilimcheck TBC akasema kuhusu 'auto search' au kitu km hicho
 
Ndio kila ukisikia inabidi ufanye kwanini usifanye mwili unataka unless kuwe na factors zinazokuzuia kwasababu sisi binadamu mbali na hapo fanya.

NB: usiseme zinaa sema tendo la ndoa, neno zinaa litumike pale inapostahili.
Dah !!

Kwa hiyo ukisikia hamu ya kulamba malaya ni bora kuusikiliza tu?

Mwili ukisikia hamu ya kumbaka mtoto wa jirani yako uusikizile tu?

Mwili ukisikia kumsaliti mkeo uusikilize tu?
 
Dah !!

Kwa hiyo ukisikia hamu ya kulamba malaya ni bora kuusikiliza tu?

Mwili ukisikia hamu ya kumbaka mtoto wa jirani yako uusikizile tu?

Mwili ukisikia kumsaliti mkeo uusikilize tu?
Inachosha ku-argue na mtu wa namna hii
 
chapati 3, maharage ya nazi, maji lita moja, juice glass moja, matunda, alafu anaenda kulala.
Tuchapati tutwatu tu na tuharagwe twa nazi tumwaji lita plus tujuice glas mbona kawaida sana hapo
 
Inachosha ku-argue na mtu wa namna hii
Mungu kakupa utashi ( will ) wa kujua zuri na baya. Mwili unaweza kutamani bia lakini utashi wako ukakataa kwa maana bia ni tamu ila ina madhara.
 
Kwa nyumbani Tanzania, ukiondoa hawa kuku wa haraka haraka, vyakula vyetu bado ni organic sana.

Kwahiyo madhara yatokanayo na vyakula kwetu bado.

Hii Dunia kuna maeneo vyakula wanavyokula usiombe!

Ni matakataka tupu
Kwahiyo tuendelee kuwaongeza wagonjwa wawe wengi ndio tuchukue hatua si ndio?
 
Hapa tunaongelea quality. Kuku anayeliwa kwetu uswahilini Ulaya anauzwa kwenye maduka maalum kwa bei maalum. Kwenye grocery stores za kawaida huwezi kumwona.
Kitu kingine ukae ukijua Ulaya ya sasa sio ya zamani useme kuku Kitu cha kawaida, bei ya vyakula imepanda mara dufu mpaka kuku unamwona luxury, usikie tu hivyo hivyo
Kuku anayeliwa kwetu Uswahilini hawezi kupata kibali cha kuuzwa hata katika duka la chakula cha makapuku Ulaya, hawezi kukidhi vigezo vyao vya usafi na afya.
 
Kufupisha tu kauli za Janabi ni kama hivi...

1. Tule kulingana na uhitaji sahihi wa mwili, mwenye njaa ndiye ale. (Kula kwa kiasi)

2. Tule kiwango kinachofaa kuiondoa njaa, usile zaidi ya uhitaji.

3. Tule mlo kamili
Sahihi
 
Google GMO foods...
Google non natural foods
Google organic fertiliser
Google organic food...

Google is your friend...
Kumbe wewe unaandika vitu tu usivyoweza hata kuvielewa na kuvielezea kwa lugha nyepesi ukitegemea Google
 
Mwisho wa siku tujifunze kujua miili yetu inahitaji nn.

Mwili wako sio sawa na wa janabi au sio sawa na wangu. Na ndio maana mm na wewe tunaweza kuumwa ugonjwa mmoja ila tukapewa dawa tofauti kutokana na reactivity ya miili yetu.

Nilishajaribu mambo mengi, hata hio Janabi anayosema pamoja na intermittent fasting, lkn nikaona haifanyi kazi kwangu. Ila nilishakua na boss ambae yeye intermittent fasting ni kama desturi kwake, na huwa anakiri inamsaidia hata kuwa productive.

Hivi hujawah kukutana na watu ambao dakika kadhaa baada ya kupata breakfast wanaanza kupata usingizi na uchovu, vile vile kuna watu bila breakfast siku nzima haiendi.

Kwa hio tujifunze kujua miili yetu inataka nn na kuenenda namna inavyotaka hasahasa kwenye swala la lishe na mazoezi.
✔️✔️✔️✔️✔️✔️✔️
 
Ngoja nikuwekee vizuri hoja ya jamaa kwa maelezo ya darasa la tatu C huenda ukaelewa.

Nchi nyingi za ulaya asilimia kubwa hawali Chakula (Food) bali wanakula biadhaa za chakula (Food Products).

Mfano wa chakula (Food) ni ugari maharagwe, kisamvu, ubwabwa mbaazi, makande, makange, mtori nk watanzania wengi hula hivi.

Mfano wa bidhaa za chakula ni Pizza, Bugger, Cheese, Cheese Bugger, Cheese pizza, Hot dogs, Coca-Cola nk wazungu 80% wanakula vyakula hivi kama mlo kamili wa siku yaani mtu anakula Pizza kama Lunch na Dinner pia daily addiction kubwa hata kwenye movie unaona littoral linasusa mpaka Pizza zake ziletwe zikiletwa linakataa "Oooh Cheese Pizza I need Cheese Burger"

Jamaa haongelei sumu ya kwenye chakula dunia ya sasa chemicals kwenye chakula haiepukiki bali anaongelea Food and Food products hizo food products ndio ulaya zimekuwa addiction na zina madhara sana kwa Tz hakuna madhara ya Junks Food labda kwa wachache na Junk food pekee kwa Tz nk Chips Yai tu 90% wajawahi kula Pizza wala KFC
Cheese ni jibini ambapo hata jamii za wafugaji wa Africa zimekuwa zikutumia kwa karne nyingi, pia ina tofauti kidogo tu na samli ambayo jamii nyingi za wafugaji Tanzania zimekuwa zikutumiza tangu enzi.

Pizza ni chakula cha asili cha wazungu kabla hata ya karne ya 16 na wakati wewe hujaanza hata kula Mahindi yaliyoletwa na Wareno.

Burger ni mkate tu unaoongezwa mboga na nyama kitu ambacho ni kizuri zaidi kuliko Waafrika wengi wanokula mkate au skonsi kavu na chai ya rangi.

Kama ni soda hata hapa bongo wanakunywa sana Pepsi, Coca-Cola na vinywaji vingine vya kiwandani vya kina Mo, Azam n.k
 
Kaka kuku ni mkasi wa nguvu siku hizi,kilo moja inagonga kwenye €10.
Kima cha chini au Wastani wa Mshahara wa Mfanyakazi Ulaya ni kiasi gani na hapa Tanzania ni kiasi gani?
 
Mwili una mifumo imara ya kutambua mapungufu na mahitaji yake.

Kwa hiyo jaribio lolote la kuuelekeza (to dictate) mwili nini cha kufanya ni kuharibu miitikio ya kimaumbile.

Mwili hutoa viashiria mbalimbali unapokuwa na mahitaji ama mapungufu;

1. Kiu.........maji.
2. Njaa....chakula.
3. Miayo....uchovu.
4. Usingizi... Mapumziko.
N.k.

Kwahiyo kula unaposikia njaa, kunywa maji unaposikia kiu, nenda haja kubwa unapobanwa na haja..

Kama vile ilivyo kwenye haja kubwa kuwa unapobanwa na haja halafu ukajibanabana madhara hutokea mwilini, ndivyo hivyo hivyo hata kwenye njaa. Usipkula unaposikia njaa, mwili utakula baadhi ya cells ama tissues zake ambazo zilikuwa zikifanya kazi nyingine hivyo kupelekea madhara kutokea.

Hujawahi kusikia madaktari wakishauri watoto walale masaa 8+, watu wazima masaa 6+, watu wasibane mkojo muda mrefu, watu wapumzike vya ktosha kupunguza uchovu, n.k?

Sasa kwanini unapokuwa na uhitaji wa chakula iwe nongwa?

Sikubaliani na Prof. Janabi kuhusu nadharia yake ya mahusiano ya kisukari na vyakula. Ninachokiona ni kwamba wazungu wanataka kutuhamishia kwenye mfumo mpya wa maisha. Ni hao hao wazungu ndiyo walikuja na nadharia ya milo 4 kwa siku, sasa wanaipiga vita. What a contradiction!

Ni wao walioleta nadharia ya jogging, sasa wanasema jogging inaharibu mifupa ya miguu na inaleta matatizo uzeeni
profesa janabi anasumbuliwa na mzimu wa MAGUFULI,kwa ivo ana kiwewe!!
 
Mimi juzi nilimsikiliza..naanza kumuelewa kidogo kidogo Prof..hasa hii statement yake anayosema itunze afya yako sasa ili ukifik 60's ukae kwa amani sio tena sfr za hospitali..maana uzeeni sumu na magonjwa tulobeba kwa miaka mingi ndo yanalipuka sasa..
 
Mungu kakupa utashi ( will ) wa kujua zuri na baya. Mwili unaweza kutamani bia lakini utashi wako ukakataa kwa maana bia ni tamu ila ina madhara.
Tuwe tunajitahidi kusoma hoja in details basi kabla ya kukimbilia kujibu haraka haraka....Anyway wewe upo sawa na hoja yangu tu tatizo ni lipo kwako na una luck baadhi ya vitu.

Mimi nimesema ukisikia hamu fanya mwili ndio unahitaji hivyo na ni Biological Things and human being is Biological things UNLESS KIWE NA FACTORS MAANA SISI BINADAMU kama religious, social, culture, Biological kwenye hizo factors kilamoja tunaweza pata factors zaidi ya 100 ndizo baadhi ulizotaja hapo juu.

So hoja ni kuwa kama hizi factors hakuna kama mimi ni muislam umeoa ulisikia hamu hata kilasiku wewe fanya mwili umetaka kibailojia na hakuna factors inayokuzuia kidini na zingine kama zipo.

Mwisho, nakumbusha kufanya mapenzi ni "TENDO LA NDOA" sshemu yeyote pale linapotajwa kufanya mapenzi jua ni tendo la ndoa liite Zinaa, kubaka na Uzinzi mpaka pale limekuja au kutajwa kinyume chake, tujifunze kufahamu kuwa hili tendo ni zuri, halal na linampendeza Mungu na la kulitaja kwa uzuri na tulitaje kwa ubaya mpkaa pale litapokuja kiutofaiti, kama hapa hoja ilizuka kama Tendo ila wadau kama wewe mumeweka msamiati wa Zinaa pale juu si sahihi.
 
Janabi anazungumza kulingana na uzoefu WA wagonjwa anaowatibu.

Overweight na obese based disease ni vitu serious.

Vyakula tunavyokula ni salama?
Ni natural?

Au mbegu za maabara zenye side effects tele.

Mbolea je ni natural?

Hakuna side effects za madawa?

Unasemaje ukisikia njaa Tu ule kumbe tunakula vyakula vyenye sumu nyingi?
Na ukija kula unakula kipi? Na nini madhara ya kukaa na njaa muda mrefu? Za kuambiwa inatakiwa uchanganye na za kwako. Miezi michache tu walikuwepo wataalam wanasisitiza watu wale vyakula ambavyo havijakobolewa.
 
The guy Prof janabi is specialist mambo anayo ongea yapo sahihi Kwa 100%
 
Wapi huko?Bei ya kuku ipo juu hivyo?

1000017980.jpg
 
Back
Top Bottom