Sikujua kama presha ikipanda kuishusha Ni kazi tofauti Na kupandisha presha iliyoshuka

Ngoja niongezee uzito kwenye hoja yako kwa kuweka madini zaidi. View attachment 2987527
 
Kahawa ina addiction. The more unatumia the more utaongeza kikombe cha ziada. Mimi nilikuwa nanunu ile chupa ya kioo ya Nescafe kubwa kabisa lile na maziwa ya unga. Aisee nilikuwa natandika mugs za kahawa kwa siku naweza piga hata tatu. Nilikuwa na moto balaa, ukipiga kahawa unakuwa kama Newton, akili inakwenda fasta kuprocess mambo, yaani unakuwa umechangamka balaa.

Sasa balaa likaanza kwenye kukosa usingizi. Halafu nikawa napata episodes za kukosa pumzi muda mwingine sababu ya kuwa hyperactive muda wote. Nikaanza kudetoxify mwili haraka sana.

Nilikuwa sili vitu vya dukani kwa siku maji ni lita nne, nakunywa juice za kutengeneza tu.

Hadi sasa niko poa nikilala ni kama mwanafunzi wa darasa la kwanza siku ya ijumaa anavyouchapa usingizi mtamu akijua jumamosi haendi popote.
 
Wakuu ningeomba mtueleweshe kidogo back benchers,
Hivi hiyo ratio eg 140 kwa 89 inamaanisha nini,
Na normally pressure inapaswa kuwa kwenye ratio ipi kwa kuzingatia nini?
Umri au uzito ?
Hiyo namba ya juu mfano 140 ina maanisha kiwango cha pressure kwenye mishipa yako ya altery (mishipa inayochukua damu kutoka moyoni kuelekea mwilini) wakati moyo unakaza kusukuma damu mwilini.

Hiyo namba ya chini mfano 80 ni pressure ya msukumo wa damu katikati ya kila pigo la moyo linapostrike. Yaani ukisikia "bubpup" "bubpup" "bubpup" moyo unapokita then yale mapigo yake msukumo unasomwa kwa namba ya chini hiyo.

Sijui kama nimekufafanulia vizuri.
 
Hapo anasema wazee wale wavijiweni wanaokunywa majivu ya buni ya kahawa iliyounguzwa hadi ikawa mkaa. Sasa si bora wanywe majivu ya mkaa ule wa kupikia
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

By the way me natumiaga hii ya Nescafe.
 
Kwanza wewe unaonyesha ni mjuaji hufuati ushauri wa daktari, naamini ungemuona daktari angekupa ushauri mzuri sana kuliko huku jf
Hadi utumie dawa daktari anakuwa ameshachunguza frequency ya upandaji wako wa pressure, siyo kwamba ikifika 140/80 ina maanisha ni tatizo ,pressure haiwezi kuwa 120/ 80 saa zote kutokana na factors nyingi ,age, chakula/ mazoezi/ stress etc
 
Inapatikana maduka ya dawa au...? Na inauzwa shilingi ngapi...?
 
E
Endelea kuwa karibu naye mno ipo siku atakuamini zaidi na mengi atakuambia Ila kwasqsa jua yapo mazito anapitia pole sana
 
Unagida vingapi?

Nmezungumzia Africafe zile nyepesi si zile za vijiweni.
 
Wakuu nashukuru Mungu now nimekaa Sawa....nimeponea kwenye grandmalta chupa mbili nilikunywa Kwa pamoja nikakaa Sawa till today my life has back to normal mana kila kitu kilisimama nlikua nna mitihani lakini nlishindwa kufanya sababu ya kuumwa
 
140/89 ndio inakufanya ufungue na uzi? Watu tunazurura na mzigo wa 180/100.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…