Sikujua kichaa anayelala nje ya jengo langu ni mpelelezi anayemtafuta gaidi wa Kizungu niliyemuoa bila mimi kujua ni gaidi

Shusha nondo
 
Hahahaa
 
ALI NACHA
 
Title tu umemaliza utamu wote, ungepaswa kuiweka kinamna yake labda "kichaa" Kichaa mpelelezi au Mpelelezi tu ama nyingine ili kuvutia msomaji


Sasa hapo kila naposoma kuhusu kichaa nishajua ni mpelelezi
 
26---28
SIKUJUA KICHAA ANAELALA NJE YA JENGO LANGU NI MPELELEZI ANAEMTAFUTA GAIDI WA KIZUNGU NILIYEMUOA BILA MIMI KUJUA NI GAIDI[emoji15][emoji24] 26&27

Wakati yule mwanajeshi niliyebaki naye anataka kuchukua bunduki kwa mwanajeshi mwenzie aliyelala chini ili amkabili yule mwanajeshi aliyetugeuka ghafla nikashanga[emoji15] yule mwanajeshi msaliti akijirusha na kutua kwenye mbavu za yule mwanajeshi ambaye niliamini ndiye mtetezi aliyebaki baada ya wenzaie kupigwa risasi, kwa namba alivyotua kwenye mbavu za mwanajshj yule na mabuti yake yenye kitu kama chuma mbele nilihisi amemvunja mbavu[emoji20] kwani ulisikika mlio wa mvunjiko wa kitu kutoka mwenye mbavu zile, "kwaa!" kisha wakadondoka wote chini, lakini kabla mwanajeshi yule hajanyanyuka chini, mimi tayari nilishachukua mtutu wa bunduki kutoka kwa Captain wa jeshi ambaye alikuwa amelala chini kwa kujeruhiwa vibaya na risasi maeneo ya mguu, haraka nikamuweka kwenye tageti yule mwanajeshi msaliti kwa kumuelekezea ule mtutu wa bunduki. Alinyoosha mikono juu ishara ya kusarenda[emoji119] huku akinisogelea, nikaona kitendo kile cha kuanza kunisogelea huku akiwa anasarenda ni ishara ya kunipoteza maboya ili nipumbazike anikabili, haraka bila kumremba nilimmiminia risasi za kichwa[emoji15] kwa macho yangu nilishuhudia ubongo pamoja na damu vikifumuka kwenye kicha chake na kuruka huku na kule kwa presha kubwa sana kisha akaanguka chini kama mzigo wa kuni na kupoteza maisha yake palepale.

Sikuwa nimewahi kuua kwa bunduki hapo kabla lakini kwa kipindi nilipokuwa natembea na wale manjemba pamoja na Clara, niliiga namna wanavyoshika bunduki na namna ya kushuti hatimaye nikafanikiwa kumwaga ubongo yule mwanajeshi msaliti.[emoji3] Nilipata furaha moyoni mwangu pamoja na nguvu [emoji123]mpya ya kuendelea na mapambano kwani tayari nilishaanza kukata tamaa, nilipomuangalia Mr.Michael ambaye alikuwa amelala chini baada ya kupigwa risasi ya bega, alikuwa anatabasamu[emoji3] nikamgeukia captain naye alikuwa anatabasamu pamoja na wanajeshi wengine waliokuwa wanananiangalia kwa furaha [emoji2] huku nikiwa nimesimama nimevalia gwanda na mkononi bado nikiwa nimeshikilia mtutu wa bunduki naangaza macho yangu huku na kule utadhani ni mwanajeshi mzoefu kumbe ushuzi tu[emoji3] kwa jinsi walivyokuwa wananiangalia huku wanatabasamu nikazidi kupata bichwa maana nilijua furaha yao inatokana na kazi kubwa niliyoifanya.

Nikaenda kuongea na Captain akiwa bado amelala chini, akaniambia nitoe simu yake mfukoni kwake nipige namba fulani ya marekani kwa whatsapp video Call aongee na namba hiyo ambayo ilikuwa ni namba ya mkuu wa vikosi vya jeshi Marekani, akamuomba aongeze nguvu ya wanajeshi maana tumezidiwa, basi mkuu wa vikosi vya jeshi aliahidi kwamba atatoa msaada kwa haraka sana iwezekanavyo, basi wakati tunasubiri jeshi la ziada kutoka Marekani kwaajili ya kutoa msaada mimi niliendelea kuwatibu wanajeshi ambao walikuwa ni majeruhi wa risasi na kuwatoa risasi kwenye miili yao, kazi hiyo niliifanya kwa weledi wa hali ya juu kwani kipindi nipo Tanzania kazi yangu halisi ilikuwa ni udaktari, basi Captain aliwatumia location ya sehemu tulipo wanajeshi wanaokuja kutoa misaada, masaa mawili yakipita ghafla nikashangaa kuona helcopter mbili za kijeshi zikizunguka angani na kutaka kutua pale uwanjani, hapo nikafarijika[emoji2] moyoni nikasema " Sasa ni ule wasaa wa kwenda kuchukua maokoto yangu[emoji385][emoji389] maana ukombozi umefika"

Helcopter za jeshi zilitua nikasaidiana nao kuwaingiza wanajeshi majeruhi ndani ya helcopter [emoji576] zile tatu kisha Helcopter yetu alipo gaidi Clara ikaanza kupaa huku nyingine zikifuatia nyuma, wakati tupo angani kabla tayari tushavuka Oman ghafla [emoji15] tukakutana na helcopter 6 nyeusi nikashangaa tunaanza kushambuliwa angani kwa kumiminiwa risasi na helcopter zetu kurushiwa makombora. Ghafla helcopter yetu ilipigiwa kombora lililotua kwenye mkia wa helcopter kwa macho yangu nilishuhudia machuma yakidondoka chini wakati huo rubani akijitahidi kuimiliki ili itue chini na ilikuwa inatua kwenye msitu mnene sana sikujua ni nchi gani hiyo maana hakukuwa na makazi ya watu, rubani alijitahidi kucontrol mara ghafla....[emoji15].....

Nini kimetokea? Hebu ninywe chai kwanza kuwahi ofisini ili nikakupe next episode au unasemaje[emoji137]?

USIPITE BILA KULIKE AMA KUCOMENT MAANA NEXT EPISODE NI BALAAA[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]

SIKUJUA KICHAA ANAELALA NJE YA JENGO LANGU NI MPELELEZI ANAEMTAFUTA GAIDI WA KIZUNGU NILIYEMUOA BILA MIMI KUJUA NI GAIDI[emoji15][emoji24] 28

Rubani alijitahidi kuimiliki ille Helcopter ya kijeshi ili itue chini salama, ghafla[emoji15] akatua kwenye msitu mnene sana, uliofunga funga kwa makamba makamba ya miti ya asili, "Eehuuuu ahsante Mungu[emoji17]" Ilibidi kwanza nishushe pumzi na kumshukuru Mungu baada ya Helcopter ile kutua salama bila yeyote kuumia, kwani tayari nilishaona kabisa hatuwezi tena kupona baada ya Helcopter [emoji576] ile kupigwa Combora[emoji95]ikiwa angani na kupoteza muelekeo wake ikawa inayumba yumba nikahisi itaanguka vibaya mno lakini Mungu akawa pamoja nasi, hata hivyo tulipotezana Helcopter za magaidi wa Clara kwani baada ya Helcopter yetu kuangukia msituni, waliachana na sisi na kuendelea kuzifukuzia zile Helcopter zetu mbili ziliobeba majeruhi wa jeshi la Marekani kwani kwa jinsi sisi tulivyoanguka walijua hatutapona. "Jamani hapa tulipodondokea ni sehemu hatari mno kwetu, kwanza hatujui tupo wapi na ni nchi gani maana tumeangukia msituni na msitu kama huu haukosi wanyama wakali hivyo kabla giza halijaingia tufanyeni mawasiliano na wenzetu waje na Helcopter pamoja na kamba watutoe katika msitu huu" alisema mjeda mmoja lakini kila mmoja alipoangalia simu yake ilikuwa inasoma Emergency Call only kwamba eneo lile hakuna mtandao kabisa[emoji30] kila mmoja wetu alianza kuweweseka kwa woga lakini ajabu Clara yeye alikuwa anacheka[emoji23] licha ya kwamba alikuwa na maumivu ya kuvunjika goti lakini hali ile iliyotukuta kwake ilikuwa ni ya furaha. "[emoji1787]Mungu amesikia kilio changu maana kama ningefikishwa Marekani kwa mashtaka yanayomkabili sijui ningepewa mateso gani kabla ya kunyongwa kiekekekeeee[emoji1787] nilikuwa naweza sana kwa bahati nzuri wote tumedondokea msituni na hakuna anayejua tulipo[emoji23][emoji1787] na kizuri zaidi hakuna mawasiliano na hapo mnaumiza vichwa muanzie wapi ili mtoke kwenye msitu huu kiekekekeeee[emoji23] sitakufa peke yangu tutafia wote humuhumu msituni." Aliongea Clara ghafla akakatishwa kauli zake na mwanajeshi mmoja ambaye alimzabua kofi nzito la macho "Kaa kimya mshenzi wa tabia wewe hata tusipofanikiwa kutoka humu tutakuulia humuhumu kifo kibaya sana ndipo na sisi tufe" alisema mwanajeshi yule akimkemea Clara.

" Jamani tusikateni tamaa mapema kwamba hatutaweza kutoka humu tuanzeni safari hata kwa miguu pengine kadri tutakavyizidi kutembea huenda tukafanikiwa kupata mawasiliano, maana tukizidi kubaki hapa tunapoteza muda laiti wenzetu wangelikuwa wanajua tulipodondokea tungekaa hapa kuwasubiri lakini hawajui" Nilitoa wazo, "Ni wazo nzuri kabisa kamanda bora tufanye maamuzi sasa hivi kwasababu hatujui safari yetu ipoje mbeleni" alinisapoti mwanajeshi mwingine wazo nililotoa, kwa bahati nzuri wanajeshi wote walikuwa wazima hawana majereha basi tukaanza safari huku tukipokezana kumbeba Clara kwasababu alikuwa hawezi kutembea. Tulitembea kwa tabu sana [emoji30] kwasababu hapakuwa na njia njia tulitengeneza wenyewe. Hatimaye giza🥹 likatukuta tukiwa bado msituni, hatukuwa na tochi wala nini, hivyo tukashindwa kuendelea na safari , kwa bahati mwanajeshi mmoja alikuwa na kiberiti cha gesi cha kuvuta sigara, hapo tukakoka moto sehemu iliyowazi na kukaa, wanajeshi wa kiume walikuwa sita na wakike wanne pamoja na mimi na Clara, tuliota moto huku tukidisikasi namna ya kutoka mule msituni lakini hatukupata majibu. Mwanajeshi mmoja akatoa wazo "Jamani kwa hapa tulipofikia kwa maarifa yetu tumefika mwisho tuunganeni tumkabidhi Mungu maana anasema hata katika maandiko matakatifu walipo wawili watatu wanaoliita jina langu na mimi nipo katikati yao, naamini tukimuomba Mungu atakuwa na sisi katika safari yetu na ataonyesha njia hata pasipo na njia kama aliweza kuwaokoa Shedrack, Meshark na Abelinego kwenye tanuru la moto basi na sisi tukiomba Mungu atatuokoa na kutuepushia mbali na madhila yote yatakayotokea katika msitu huu, Paulo na slaa walipowekwa gerezani walipiga maombi milango ya gereza ikafunguka, hivyo na sisi tukiwa na imani tutatoka salama katika msitu huu. " Aliongea yule mwanajeshi wa kike nikajisemea moyoni kwamba " binadamu bwama tuna kiburi sana yani Mungu anakumbukwa wakati wa matatizo, je kwanini Helcopter ilipotaka kuanza safari tusingefanya maombi, any way acha tu tuombe.

Tulifanya maombj ya nguvu wakati Huo Clara alikuwa anatucheka [emoji23][emoji1787] tulipomaliza maombi akasema "Mimi hata sijisumbui kuomba maana Mungu akisikia sauti yangu ataziba masikio nimeua watu wengi mno wakubwa kwa watoto tena wengine hawana hatia mimi ni wa moyoni tu" alisema Clara, hakuna aliyemjibu kila mmoja alitafuta sehemu yake ya kulala akajikunyata na kulala, wakati ndo naanza kupata kijiusingizi, ghafla tukasikia mingurumo ya simba wote tukaamka, ile naangalia huku na kule tulikuwa tumezungukwa na simba wengi mno wasio na idadi, "enheee kumekucha sasa "nilijisemea moyoni huku nikitetemeka[emoji30] haraka kila mmoja akashika bunduki naku..[emoji15]..........

Full 1000
0784468229
 
Sema mwanangu Brighton umejipakulia minyama sana [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Uzi mzuri
 

Hivi hii story yako umetunga mwenyeweau umekopi mahali fulani ukatuwekea humu, maana naona sehemu nyingi ukekuwa ukikopi na kupest tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…