Sikujua kichaa anayelala nje ya jengo langu ni mpelelezi anayemtafuta gaidi wa Kizungu niliyemuoa bila mimi kujua ni gaidi

mimi sitohi hata mia kama hutoposti tena baci stohi hata shilingi moja
 
Kumbe nilitema BIG "G" kwa karanga za kuonjeshwa,tu halafu ukatuacha njiani
 
Sikujua kichaa anayelala nje ya jengo langu ni mpelelezi anayemtafuta gaidi wa Kizungu niliyemuoa bila mimi kujua ni gaidi.

Nadhani story yako umeimaliza kwenye hiyo title yako.
 
Tatizo huwa hamumalizii story hadi inatia uvivu kuisoma
 
SIKUJUA KICHAA ANAELALA NJE YA JENGO LANGU NI MPELELEZI ANAEMTAFUTA GAIDI WA KIZUNGU NILIYEMUOA BILA MIMI KUJUA NI GAIDI[emoji15][emoji24] 41&42

Doctor Shedy alikunywa pombe nyingi[emoji898]kupita kiasi na kulewa chakari mithili ya mlevi wa mataputapu, nikiwa sina hili wala lile mara ghafla[emoji32] Doctor Shedy akaanza kuropoka mbele ya Mr Michael na wanajeshi wengine, "Watanzania hasa wapare na wachaga wanapenda hela sana [emoji3] yani mtu yuko radhi akane damu yake ili apate mabilioni ya pesa, hcho ndicho alichokifanya Brighton ila kawaida ya sisi walevi ni wasema kweli acha tu ukweli usemwe, vipimo vya DNA vya mtoto wa Cara vinaonyesha baba wa mtoto ni Mr. Brighton" aliropoka Doctor Sheddy na kumfanya mr. Michael apigwe na butwaa na kutoa macho[emoji15] kama mtu aliyepokea habari mbaya za kuogofya, "Mbona wewe doctor hueleweki, sasa kama mtoto ni wa Brighton kwanini ukanibambikizia mimi ee" aliuliza Michael huku akiwa amekunja uso wake [emoji30]kwa hasira. "Wewe nawe kwahiyo kukuambia ukweli mapema ni kosa, au ulitaka ulee mtoto wa kidume mwenzio kisha huko baadae ushagharamika ndio uje kuujua ukweli[emoji12]?" Doctor Sheddy alimuuliza Mr. Michael kwa sauti ya kilevi wakati huo nilikuwa nimeduwaa sana🫢baada ya doctor Sheddy kuvujisha siri. Haraka Mr. Michael akamkunja tai Doctor Sheddy, "Sema ukweli kwanini uliamua kunidanganya, na ole wako usiseme ukweli nakwambia hizo pombe zitakuisha leo[emoji3525]" aliongea Mr Michael huku akiwa amemkaba Doctor Sheddy shingo yake kwa kumshika tai. "Niachie basi niseme" Doctor Sheddy alijitetea "Haya sema" Mr Michael alimwambia kwa kumkoromea. "Ukweli ni kwamba Mr. Brighton ndiye aliyeniambia kwamba ikitokea vipimo vya DNA vikaonyesha mtoto ni wake basi nisimtaje yeye bali nikutaje wewe kwasababu kama nitamtaja yeye kuna uwezekano wa yeye kukosa hela alizoahidiwa kulipwa kwa kigezo kwamba atahisiwa kwamba kuna njama anazopanga dhidi ya jeshi na pia ataonekana anashirikiana na majambazi mpaka akafikia kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Clara hivyo aliniomba nimfichie siri na pia akaniahidi akilipwa atanikatia fungu kidogo kwa kazi niliyoifanya ya kumfichia siri." Doctor Sheddy alitoboa siri wakati huo mkuu wa vikosi vya jeshi na wanajeshi wengine walikuwa wakisikiliza kwa umakini �sana.

"Lione vile yani kama lizwazwa hapo tayari limeshaunguza picha yani tena halijalewa hili huenda limefanya makusudi maana kawaida ya wabongo hatupendani, wivu na chuki ndio vinatusumbua hapo limeona nimewekewa mabilioni ya pesa kwenye akaunti yangu likajisikia wivu " Niliongea kimoyomoyo huku nikimtazama Doctor Sheddy kwa hasira sana[emoji3064] na machozi yakinilengalenga. Mkuu wa vikosi vya jeshi akamnyamazisha Dr. Sheddy pamoja na Mr. Michael na wanajeshi wengine ambao walikuwa wakiendeleza minong'ono. Baada ya wote kukaa kimya mkuu wa jeshi akaanza kuongea "Nchi yetu inapinga vikali sana kitendo cha mtu kutoa rushwa ili apate cheo au kitu fulani anachokihitaji, kwa hili ni dhahiri kabisa kwamba Mr. Brighton atakuwa anashirikiana na Clara kwa namna moja au nyingine, na huenda kuna mpango anausuka ndio maana akawa anajipendekeza kwetu, kwa maana hiyo aswekwe mahahusu mara moja ili kupisha uchunguzi wa kina dhidi yake[emoji32]" alisema mkuu wa vikosi vya jeshi na kuwaamuru wanajeshi wawili wanikamate na kuniweka ndani ya gari nipelekwe mahabusu. Pale nikaona sasa nisipojitetea kufa na kupona nitaswekwa gerezani hivi hivi naona, na kwa jinsi wazungu wasivyotupenda sisi waafrica naweza kupewa hata kesi ya uhaini kwenye taifa la watu na nisiwekewe dhamana, basi wakati wale wanajeshi wananifuata ili wanikamate, nilinyanyuka mara moja nilopoketi na kuanza kukimbia[emoji2099] walianza kunikimbiza huku wakiniftatulia risasi, nilikimbia kwa kupindapinda nikizikwepa zile risasi zisinipate[emoji16], nilipotoka tu nje ya kambi ya Jeshi kuna jaamaa alikuwa anataka kupaki pikipiki yake nje ya duka moja, kabla hajaizima nilimpiga kikumbo akadondoka pembeni, nikamnyang'anya pikipiki[emoji2509] na kuanza kukimbia nayo , nilivuta mafuta nikiwa kwenye mwendo mkali sana maana nyuma yangu nilikuwa nakimbizwa na gari dogo la kijeshi, hapo nikajiongeza kupita njia za vichochoro ambapo lile gari la kijeshi [emoji601] haliwezi kupita, hapo nikakatiza vichororo kadhaaa na kuwaacha kwenye mataa[emoji3] Nilikimbia na kutoka kabisa maeneo ya makazi ya watu na kwenda kujificha maeneo ya porini chini ya daraja kubwa sana, niliwasha simu yangu haraka, na kumpigia mdogo wangu ambaye yupo Tanzania kwa whatsap call, nikafanya utaratibu wa kuhamisha zile bilioni sabini kutoka kwenye account yangu kwenda kwenye account yake ya benki.

Niliendelea kukagua simu yangu mara nikautana[emoji15] na picha zangu kwenye vyanzo vya habari vya marekani wakiwa wamenipost kila kona wakiambatanisha kichwa cha habari kilichosomeka "JAMBAZI MWENYE ASILI YA KITANZANIA ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUSHIRIKIANA NA MAJAMBAZI WENGINE KWA KOSA LA KUVUNJA MABENKI NA KUSABABISHA MAAFA YA MAMIA YA WATU, yoyote atakaefanikisha kupatiana kwake atapatiwa donge nono kama zawaidi. " nilisoma taarifa hizo huku moyo ukinidunda balaa[emoji15] "Mungu wangu tayari nishabambikiziwa kesi ya mauwaji, hivi wakinipata si nimekwisha mimi[emoji848]" niliwaza, basi usiku uleule nilienda benki za marekani kwasababu zilikuwa zinafanya kazi masaa 24 nikatoa kama milioni saba ambazo nilibakiza kwenye account yangu, baada ya kutoa haraka nikaondoka bila kupoteza muda maana kuna watu walianza kunitizama usoni nahisi walianza kunifananisha na picha zangu zilizopostiwa, baada ya kuondoka pale nikaenda kwenye duka la nguo nikanunua baibui na nikabu ya kuficha uso, nikaenda hotelini na kuchukua chumba , kwenye daflari la kujiandikisha wageni nikaandia jina tofauti lakini la kiume, ila nilipoingia chumbani nikabadilisha mavazi haraka na kuvaa yale ya baibui na nikabu, wakati nipo ndani ya chumba changu mara nikasikia nje polisi wakiongea na muhudumu wa vyumba " Sisi ni jeshi la polisi samahani hapa hotelini kwako una CCTV camera" polisi aliuliza . "hapana ilishaharibika" alijibu muhudumu. "Basi sawa kuna muhalifu tunamtafuta kama kungekuwa na CCTV camera ingekuwa rahisi kumpata ila kwasababu hamna waamshe wateja wako wote tufanye ukaguzi chumba hadi chumba" alisema polisi. Macho yalinitoka[emoji15]moyoni nikasema sasa kimenuka.. .

JE ITAKUWAJE SASA ? BRIGHTON ATAKAMATWA AU? Hakika mambo ni moto si kitoto[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji16] hakikisha unalike na kucoment ili nije chaaaap

Offer malizia kwa 500
0784468229
 
SIKUJUA KICHAA ANAELALA NJE YA JENGO LANGU NI MPELELEZI ANAEMTAFUTA GAIDI WA KIZUNGU NILIYEMUOA BILA MIMI KUJUA NI GAIDI[emoji15][emoji24]

Sehemu ya 43,44&45 MWISHO[emoji3578]

Nikiwa tayari nimekwishavalia baibui langu na nikabu ambayo iliyonifunika uso wote na kuacha sehemu ya macho🥷 nikajilaza kitandani huku nikiwaza ni kwa namna gani nitachomoka marekani nirejee tanzania bila jeshi la polisi la marekani kunitia nguvuni, wakati naendelea kujadiliana na serikali pamoja na bunge la kichwa changu mara ghafla[emoji15] nikasikia huko nje polisi wakiongea na muhudumu wa vyumba, walimueleza kwamba kuna muhalifu wanamtafuta hivyo wakamuomba CCTV camera [emoji327] ambayo ingenasa picha za watu wote waliowasili hotelini hapo, kwa bahati nzuri muhudumu aliwaeleza kwamba CCTV camera iliyokuwa inatumika hotelini hapo imeharibika, basi wakamwambia "basi sawa sio tabu hebu waamshe wateja wako wote tukague chumba hadi chumba" niliposikia kauli hiyo mwili wote ulianza kunitetemeka mpaka utumbo, kwani niljua ni lazima tu nitiwe nguvuni.

Basi nikakaa kimya nikingoja kitakachojiri, niliwasikia wakikagua chumba hadi chumba huku wakiwauliza wateja majina yao na sehemu walipotoka pamoja na kazi zao, waliuliza chumba hadi chumba walipofika kwenye chumba changu wakagonga mlango [emoji15] hapo nikajidai nimelala na ninakoroma kama paka aliye usingizini[emoji3] wakapiga mpaka simu ya mezani[emoji338] iliyokuwa mule chumbani, simu iliita mda mrefu lakini bado nilizidi kujikausha. "Mh huyu mtu vipi ni usingizi gani huo yani pamoja na kubamiza kote mlango kiasi hichi manusura uvunjike lakini bado yupo usingizini hapana huenda ndiye muhalifu mwenyewe kwani kwenye daftari na mteja wa chumba hichi ameandika jina gani" Askari alimuuloza muhudumu wa vyumba. "Ameandika George Nicholus" muhudumu alijibu. "Na ameandika ametoka wapi? Askari alimuuliza tena muhudumu. " Washngton Dc " muhudumu alimjibu askari kwamba natokea jiji la washton Dc lililopo hapohapo marekani, "Ni sawa lakini kama ni mwema kwanini ajikaushe asifungue mlango, je alikuwa ni mzungu au ni mwafrica" askari alizidi kumdodosa muhudumu. Swali hilo likawa mwiba kwangu kwani wakati naingia mpaka napewa chumba nilikuwa bado sijavalia yale mavazi tangu ya kujificha yani baiubui na nikabu🥷. "Ni mwafrica na anadai yeye ni mfanyabiashara wa madini" alijibu muhudumu. "Je ni huyu hapa kwenye picha" askari aliendelea kumuuliza muhudumu huku akimuonyeshea picha yangu. "Sina uhakika maana hapa nahudumia watu wengi na kuna vyumba zaidi ya mia mbili ishirini hivyo ni vigumu kukariri kila sura ya mteja anayeingia na kutoka" alisema muhudumu.

"Sawa kama ni mwafrica tunaomba tuvunje mlango, tutalipa gharama za mlango na ikiwa sio yeye tunayemtafuta pia tutamlipa gharama za usumbufu" alisema askari. Basi sawa" muhudumu alikubaliana nao. Moyoni nikasema "Kishanuka sasa hapa natembeza mkong'oto [emoji109]bila kujali ni nani atapita mbele ya macho yangu" niliongea kimoyomoyo huku nikiwa bado nimejilaza pale kitandani wakati huo mlango wakiendelea kuvunja mlango, mlango ulipofunguka nikajifanya nimekurupuka kitandani mfano wa mtu aliyekuwa anaota ndoto mbaya akashtuka na kupiga kelele. Tena nilipiga kelele kwa kuigiza sauti ya kike[emoji32] "Heee mbona sasa ni mwanamke yupo na kwenye daftari amejiandikisha mwanaume. Aliuliza askari na nilikuwa hodari wa kuigiza sauti ya kike haswa yani Joti wa kutokea Tanzania akasome. "Wewe dada kulikoni umejiandikisha jina la kiume ile hali wewe ni mwanamke" askari alianza na swali hilo. "Mimi nilikuwa na mume wangu tulikuja hapa kuenjoy kama wapenzi ila ameitwa kazini maana yeye ni mfanyabiashara wa madini na yeye ndiye aliyejiandikisha kwenye kitabu" Nilijibu. "Hebu kwanza toa hiyo nikabu yako sisi tunataka tuongee na mtu ambaye tunaona sura yake" alisema askari. "Kaka dini yangu hairuhusu" nilijibu kwa kulegeza sauti. "Dada acha kuleta mambo ya udini kwenye serikali toa nikabu yako haraka sana[emoji17] usituletee udini wako hapa kila mtu ana imani yake lakini tuwapo kwenye mambo ya kiserikali wote tuwamoja na pia wewe unaonekana ni muhalifu tu kwasababu utalalaje na hizo nguo [emoji848]"

Alisema askari. Kabla hajakaa sawa nilimchopu ngumi[emoji109] ya kidevu, alianguka pembeni haraka nikashika kiti kilichokuwa mule chumbani, nikaanza kuwatembezea wenzanzake kwa kuwatwanga nacho vichwani, yani kila aliyejileta aliambulia kiti cha kichwa, nilipopata tu kaupenyo sikutaka kung'oja nnzi wajae[emoji12] nilichomoka mbio na kuanza kukimbia, baadhi walinikimbiza lakini walishindwa kunipata, asubuhi yake nilienda uwanja wa ndege nilikata pasport ya kusafiria ambayo ilikuwa na jina la kike, nilisafiri mpaka uturuki na huko nilobadili sura yangu na kuwa ni ya mwanaume ambaye ni chatara mwenye asili ya kizungu na africa kisha nikakata pasport tena ya kusafiria na kurudi Tanzania, iliniwia vigumu ndugu za kunielewa lakini sauti pamoja na kuwatambua ndugu wote wa ukoo pamoja na kuwatajia majina yao hadi waliokufa viliwafanya waniamini, hata hivyo nilihama nilipokuwa naishi kuhamia kijijini kabisa ambapo kwa sasa nimejiwekeza katika biashara mbalimbali ila kiuhalisia natumia sura ambayo sio yangu. Yote yote pia nimejifunza kutokuwakaribisha watu nisiowafahamu vizuri nyumbani kwangu .

MWISHO SEASON 02!!!

 
Pamokooooooo
 
Title ya story tu inabore. Hakuna ubunifu ni ya kitoto. Haina mvuto.
 
Bado unataka Mwanzi?
Kweli naona umejanjaruka. Wewe ulikuwa huishi kuandika nyuzi za kutusema wapemba.... Na ukasimulia kile kisa cha mpemba kukutunuku gari. Leo unaona kutukana ndo ujanja wa mjini? Hewallah sheikh. Inshallaah... Ila kumbuka bado hujamaliza safari sheikh.... Wewe mjini tumekuingiza sisi, tumekupokea na kukupa hadi gari.... Leo hii umekuwa mjanja wa matusi? Nawe eti unajua kitu.... Umesahau kuwa umekaa home kwa Ami Yusufali ukimhudumia? Na ulisema humu mwenyewe? 😁
 
Nimekuuliza UMEUMISS MWANZI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…