Ni kweli kama hakuzingatii maana yake hakupendi
Sasa binadamu wapo wa aina tofauti
Kuna ambaye mara zote huwa anaongea straight kwamba hiki na hiki sipendi,napenda hiki
Wapo ambao huwa wanakuonesha hawapendi kwa vitendo,nafikiri ndo aina ya wa kwako...yeye anaona akifanya drama kadhaa ndo utajiongeza kufanya ama kutofanya jambo fulani
Kimsingi mimi navyofikiria mahusiano ya mapenzi ni kuelekezana tu,wa kwako pia unaweza kumwambia kwamba hivyo alivyo hupendi....kama anakupenda na ana-value mahusiano yenu utamuona anabadilika hata kama sio kwa haraka
Ongea nae,ukiona huwezi kuendelea na drama zake unajitoa...navyojua mapenzi hayatakiwi kuongozwa na maumivu sana kuliko amani
Dunia hii ina lots of choices,kuamua kuvurugwa na huyo mmoja ni choice yako pia
Kila la heri