Zirconium
Senior Member
- Feb 1, 2025
- 196
- 254
Jana usiku nilikuwa namsindikiza rafiki yangu Tabata Segerea, nikitokea Kijitonyama .
Binafsi, ni miezi sita tangu nifike Tabata, na njia zangu za kawaida zilikuwa hazinipeleki upande huo.
Lakini kila tulipokuwa tukikata kona, nilikuwa nashangaa kuona jinsi mji ulivyobadilika. Si ule mji niliouzoea tena.
Maduka mengi yamevunjwa na kujengwa upya kwa mtindo wa kisasa, liquor stores zimeongezeka sana, eneo limechangamka. Watu hawalali.
Na haya yote yametokea ndani ya miezi sita tu.
Kuna kasi ya mabadiliko ambayo wengi wetu tunashindwa kuikubali kwa sababu tunapenda ile hali ya faraja tunayopata pale vitu vinapobaki vilevile.
Lakini ukweli ni kwamba, dunia haijali kuhusu faraja yako. Dunia itabadilika, ukiwa tayari au la.
Na ndio maana kwenye mitaala yetu, ikiwa tutaendelea kufundisha na kuwafanyisha mitihani wanafunzi kwenye vitu kama Vita vya Majimaji, huku tukikwepa ukweli kwamba:
na teknolojia nyingine zitakuja kubadilisha au kuchukua baadhi ya kazi ambazo mtu anasomea leo, basi tuna tatizo kubwa.
Dunia itashindwa kukufundisha mambo mengi muhimu, lakini ni muhimu uwe na uwezo wa kujifunza mwenyewe.
Na kama hujui pa kuanzia, angalau jifunze kuhusu:
Rekebisha chochote ambacho bado hakijavunjika kabisa ndani yako.

- AI
- Kazi za mbali (remote work)
- Freelancing
na teknolojia nyingine zitakuja kubadilisha au kuchukua baadhi ya kazi ambazo mtu anasomea leo, basi tuna tatizo kubwa.
Dunia itashindwa kukufundisha mambo mengi muhimu, lakini ni muhimu uwe na uwezo wa kujifunza mwenyewe.
Na kama hujui pa kuanzia, angalau jifunze kuhusu:
- Nidhamu — ya kifedha na ya kibinafsi
- Afya njema
- Kujiamini
- Falsafa na misingi yako ya maisha
- Uadilifu na uaminifu
- Maadili ya kazi (work ethic)
- Mwongozo wa kiroho
- Misingi ya biashara
- Uwezo wa kubadilika na kuendana na mazingira (flexibility)