Sikushauri kununua Impreza subaru

Sikushauri kununua Impreza subaru

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
Mnaonunua hili gari mmeangalia mazingira halisi ya hapa kwetu Tanzania? Gari ipo chini sana pia ni gari ambayo mafuta yanaenda mengi sana sijui kuhusu spare zake kama ni rahisi kuzipata hapa bongo, je mafundi wa magari hapa bongo wanaweza litengeneza ilo gari?

Mafundi wa bongo ni wachache sana wako expert kama unataka nunua hili gari sikushauri utakuja kuuza kwa bei ya hasara.
 
Mnao nunua hili gari mmeangalia mazingira halis ya hapa kwetu tz? Gari ipo chini sana pia ni gari ambayo mafuta yanaenda mengi sana sijui kuhusu spare zake kama ni rahisi kuzipata hapa bongo je mafundi wa magari hapa bongo wanaweza litengeneza ilo gari? Mafundi wa bongo ni wachache sana wako expert kama unataka nunua hili gari sikushauri utakuja kuuza kwa bei ya hasara

kumbe
vipi rav 4 vanguard
 
Taratibu bro.

Moja ya gari pendwa hapa nchini ukiacha IST, Dualis, Harrier ni iyo Subaru Imprezza.

Kwanza bei rafiki, pili mafuta unayosema inakunywa unaongelea hii ya 3rd generation au?

2007_Subaru_Impreza_(GH7_MY08)_R_hatchback_(2015-07-09)_01_(cropped).jpg


Maana iyo ipo ya cc 1500, 4-Speed Auto.

Labda ukichukua WRX na WRX STI ndio unaweza toa ayo malalamiko.

Mafundi na spare kwa Dar es Salaam wapo. Budget yako tu.

Edit: Unavyonunua gari vema ukaangalia inapokaa kwenue issue ya ground clearance. Kweli ipo chini lakini mi nikiwa na gari kuna sehemu siendi. Unapanda boda.
 
Mnaonunua hili gari mmeangalia mazingira halisi ya hapa kwetu Tanzania? Gari ipo chini sana pia ni gari ambayo mafuta yanaenda mengi sana sijui kuhusu spare zake kama ni rahisi kuzipata hapa bongo, je mafundi wa magari hapa bongo wanaweza litengeneza ilo gari?

Mafundi wa bongo ni wachache sana wako expert kama unataka nunua hili gari sikushauri utakuja kuuza kwa bei ya hasara.
Chuma imekaa vizuri tu. Kama unaishi makorongoni ndio utapata tabu kwa kuwa ni kweli iko chini. Kuhusu mafuta na spare mbona zipo za kutosha. Tangu ninunue natembea average ya 12.5km per litre. Mafundi wapo wa kutosha, tena kuna garage special kwa ajili ya subatu tu. Inategemea unaishi wapi.

Mwaka wa tatu huu naitumia nabdalilisha tu engine oil. Service kubwa ambayo nimeshawahi kuifanya ni kubadili bush na tires.
 
kumbe
vipi rav 4 vanguard
nzuri lakini ujue vanguard haina tairi la dharura. ukiwa na safari ndefu hakikisha matairi ni mazuri. ikipiga pacha inarekebishika kwa kuweka dawa lakini ikipiga bust ya maana ujue umeumia

aina ya gari ni utashi na mapenzi ya mtu tu na umenunua gari lenye ubovu wa kiwango gani, kwa sababu hata wanaoyauza japani hawayauzi eti wameamua, wengi wanayauza baada ya kuyaona yana shida na mengine yanakuwa yameshatelekezwa. wahuni wanayaokota wanayapiga polish na kuyaweka sokoni....kuna watu hizo x trail wana uzoefu mbaya nazo.

Ukiamua kununua gari wewe nunua tu kuufurahisha moyo wako usisikilize maoni ya mtu. Hata mafundi ukiwauliza kama kuna gari hawezi kulitengeneza atakwambia hayo magari mabovu sana. Hawezi akakupa positive feedback.
 
Back
Top Bottom