Sikutegemea kama Mtwara ina fursa kiasi hiki

Hayo maghala yangejaaje mizigo au mazao, kwa hayo yaliyosemwa?, unamaana mazao yanajilima yenyewe?
 
Sasa hayo Unayoyasema na uislamu wapi na wapi? Hii nchi ina vijana Wana umasikini wa fikra sijawahi kuona aisee
 
Sijui kwanini watu wanaichukia mikoa ya kusini
Wengi hawajawahi kufika Mtwara na wanachanganya Lindi na Mtwara.
Mji wa Lindi kwa kweli haujachagangamka ila Mtwara nadhani ni Manispaa inayokuwa kwa kasi ulinganisha na baadhi ya Manispaa tena hapo baada ya shughuli za gesi kukimbiziwa Dar.
Kama vile viwanda vilinvyotumia gesi vingejengwa Mtwara nadhani ingekuwa JIji maana kipindi cha gesi viwanja vilifikia sh mil 300 gesi ilivyopelekwa pwani na Dar mji ukadorora ila kwa sasa umeanza kurudi kidogokidogo
 
Usichojua ni kuwa mkoloni hakupotezea mikoa ya kusini. Alijenga hadi reli na alianzisha shule nyingi tu za maana. Aliyepotezea kusini ni Nyerere na ccm yake
Nimesoma history ni kweli alijenga reli kwenda nachingwea kwenye mradi wa karanga ila aliing'oa kwa nini
 
Kweli watu wanai Chukia mtwara Sana!gesi ingebakizwa mtwara aisee ingekuwa ni cape town nyingine
 
Ccm oyeer
 
Qa
Tufanye hakuna,hela wanazopata huko zinaenda wapi?siulizi kwa ubaya mimi nahisi wenyeji wanesinzia kuna wageni wameigeuza mtwara kama chimbo lao la kupiga hela na kuwekeza makwao
Watu gani hao?
 
🙏marhaba
 
Huwa nawashangaa sana watu wa bara sisi huku mtwara tunalima mazao maarufu nchini kuanzia korosho,mbaazi na ufuta sasa huwa nashangaa mno tunapoitwa sisi ni wavivu...au kipimo cha uvivu ni kutokuwa wachukuzi wa magunia kama wasukuma?
Korosho, mbaazi na ufuta ni mazao ya kivivu
Sehemu yenye wavaa kobazi wengi hawana maendeleo angalia Singida, Shinyanga mjini, Pwani, Lindi, Tanga na Mtwara.
Mikorosho imepandwa miaka 15 iliyopita kama maembe halafu anajiita mchapakazi😀😀😀😀
Nilienda Masasi kijiji cha Kinamatunu. Kutoka kijiji mpaka masasi kwa mguu unatumia dk 45 mpk 50 kufika lkn hakina mabomba ya maji wala umeme. Nenda Karatu (Mang'ola, umeme na maji ya bomba ni uhakika). Wairaq wanaendesha Land cruiser na Defender (TDI) ambapo huko kwenu ukiona ni magari ya serikali tena taasisi, jeshi au polisi. Ni miti ya mikorosho tu imepandwa ili apate muda mwingi wa kupumzika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…