Silaa, Polepole na Gwajima waitwa Kamati Kuu ya CCM kujieleza

Ni kawaida hata Membe bila shaka aliitwa then akafurushwa ndani ya Chama.....sio jambo la kushangaza ni utaratibu wa CCM kwa wanachama wake....

Bila shaka hata vyama vingine vina taratibu zake, tuheshimu taratibu za vyama vyetu....Ndio demokrasia, ukikosea unaitwa unasikilizwa then hukumu inatoka...
 
Kujikosoa ni msingi imara wa taasisi yoyote ile. Maana mnapojikosoa ndio hapo mnajiweka sawa na kujirekebisha.

Kwa muda mfupi tangu hayati JPM atutoke watanzania kwa macho yao wameshuhudia mabadiliko makubwa.

kuna dalili mradi mkubwa kama JNHP hautakamilika kama ilivyopangwa, kuna dalili za rushwa kama za Escrow kurudi kupitia mgao wa umeme, harufu za ufisadi kila kona mbaya zaidi ni hata mwaka haujaisha tokea hayati JPM afariki.

Je kwa mwanaCCM kama Polepole kuhoji na kukosoa haya mabaya yanahochafua serikali na chama cha CCM ni kosa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…