Kujikosoa ni msingi imara wa taasisi yoyote ile. Maana mnapojikosoa ndio hapo mnajiweka sawa na kujirekebisha.
Kwa muda mfupi tangu hayati JPM atutoke watanzania kwa macho yao wameshuhudia mabadiliko makubwa.
kuna dalili mradi mkubwa kama JNHP hautakamilika kama ilivyopangwa, kuna dalili za rushwa kama za Escrow kurudi kupitia mgao wa umeme, harufu za ufisadi kila kona mbaya zaidi ni hata mwaka haujaisha tokea hayati JPM afariki.
Je kwa mwanaCCM kama Polepole kuhoji na kukosoa haya mabaya yanahochafua serikali na chama cha CCM ni kosa?