Wamemtafutia Polepole sababu ya kumfunga mdomo kwa kuwatumia hao kina Gwajima na Silaa kama chambo.
Hapo kitakachofuata Polepole ataambiwa adhabu yake akae kimya miezi sita yuko chini ya uangalizi, awe makini huko kikaoni kama Gwajima alivyofanya na "mic"
Huu ujinga ndio unafurahiwa na wenye mawazo mgando wenye "chama chao".
Hawajui kufungana midomo kunatengeneza taifa la majuha, na vile elimu yetu iko chini, ndio tunaandaa kizazi cha malofa na adui ujinga ataendelea kututesa miaka yote mpaka mwisho wa dunia, CCM ni wajinga sana.
Nachomshauri Polepole kwanza awaambie hao CCM wenzake hajavunja sheria yoyote ya nchi kutoa mawazo yake, pili, afuate taratibu alizoambiwa na TCRA ili arudi hewani, na nyie TCRA mfanye kazi yenu kiuweledi, msijigeuze wanasiasa.