Silaha 3 Zifuatazo Zitakusaidia Kutoboza Maishani (Ya Mwisho ni Muhimu Kweli)

Silaha 3 Zifuatazo Zitakusaidia Kutoboza Maishani (Ya Mwisho ni Muhimu Kweli)

Amba Samedi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2024
Posts
207
Reaction score
346
Habari mwanaJF,

Natumaini kuwa unaendelea vizuri. Hatujaonana siku nyingi. Nilikuwa nafanya "reset". Na Mungu amekuwa mwaminifu. "Ameninyeshea mvua" za baraka katika maisha yangu. Sikuwa na kitu January, lakini maghala yangu yanafurika sasa. Mungu ni mwaminifu!

Leo unapowaangalia watu wanaopiga hatua haraka maishani, utagundua kitu kimoja: wanajenga msingi wao juu ya vitu vitatu muhimu:
  • Mwelekeo sahihi (Mindset),
  • ujuzi sahihi (Skillset),
  • na nyenzo sahihi (Toolset).

Hebu tujifunze zaidi.

1. Mindset: Wewe ni Matokeo ya Fikra Zako​

Huwezi kufika mbali kama akili yako imefungwa.
Kuna mitazamo ya aina mbili:
  • Mtazamo Usiobadilika (Fixed Mindset): Mabadiliko kwako yanakuwa kama adui. Unaogopa kufeli.
  • Mtazamo wa Ukuaji (Growth Mindset): Unaona kushindwa si mwisho bali daraja la mafanikio. Unajifunza kila wakati, unakua kila siku. Kwako, ama unashinda, au unajifunza. Yote mema.
“Ukishindwa, jifunze. Ukishinda, shukuru. Vyote viwili ni kwa faida yako.”

Jifunze kwa Kuokota Vipengele Muhimu (Role Modelling)​

Acha kusubiri. Tafuta watu wa kuiga. Si lazima wakufundishe moja kwa moja. Na usichukue kila kitu. Chunguza vitu vifuatavyo:
  • Wanachokiamini: Mtazamo wao ni upi kuhusu mafanikio, pesa, au juhudi?
  • Wanavyofikiri: Wanatarajia mema au mabaya? Wanafikiri kwa tafakari au hawaeleweki eleweki?
  • Muonekano: Je, Wanatembea kwa kujiamini? Wanaongea kwa uthabiti? Je, mwili wao unaakisi mtu anayeamini kuwa ana thamani?
Mwili ni kama redio ya ndani kwa ndani: unavyoushughulisha, ndivyo unavyotuma ujumbe nje.
“Jinsi unavyosimama huamua jinsi unavyopokelewa.”
Kumbuka: Kipaji pekee hakitoshi—kinahitaji mazoezi, nidhamu, na maarifa ili kuwaka kama moto.

2. Skillset: Soko Huwalipa Wanaojua Kujielezea​

Walisema wahenga "biashara ni matangazo". Sasa, dunia ya leo inathamini skills 3 zifuatazo:

a) Mauzo (Sales)
Watu wengi hawapendi kuuza, lakini kila mtu anapenda kununua.
Ukijifunza kuuza chochote kilicho halali, utakuwa ushakamilisha nusu ya safari.
Uuzaji utakupa uwezo wa kuwashawishi watu kuona faida ya suluhisho fulani kwa matatizo yao.
“Soko la watu wanaopenda kununua ina ukubwa ya mara 19 ikilinganishwa na lile la wanaopenda kuuza.”

b) Masoko (Marketing)​

Soko linalokukabili ni kubwa mno. Ili kufanikiwa, jifunze kuuliza maswali sahihi.
  • Ni nani anahitaji kile unachotoa?
  • Wanapenda nini?
  • Wako wapi?
  • Unawezaje kuwasiliana nao kwa lugha yao?
Daima jifunze kuelewa kabla ya kueleweka.

c) Utambulisho (Branding)​

Jina lako ni sehemu muhimu katika kuisimulia hadithi yako. Ukilijenga vizuri, watu watakulipa hata kabla hujazungumza.

Jenga utambulisho binafsi (personal brand) kabla ya kujaribu kukuza biashara yako (business brand).
Watu hununua kwa watu kabla ya kununua kwa kampuni. Ukijenga jina lako, biashara yako itakushukuru.

“Chapa bora huanzia na mtu, si bidhaa.”

3. Mindset: Kasi Ni Faida Mpya Kwako​

Leo, kila kitu kinaenda kwa "kasi" Tanzania.
  • Mtandao wa 5G: Kasi
  • Mwendo kasi ya Dar
  • Treni ya Mwendo Kasi
  • Chaja ya Kasi (fast charger)

Enzi hizi, lazima uwe na nyenzo za kwenda haraka. Kuna zana tatu za msingi ambazo kila mshindi anapaswa kuwa nazo:

a) Kifaa unganishi (Connected Device)​

Simu janja au kompyuta ni silaha yako ya kazi. Inaweza kukupeleka popote ukiwa ungali nyumbani.
Unaweza kutuma barua pepe, ujumbe wa WhatsApp, kuandika pendekezo, au kuendesha biashara nzima mfukoni.

b) Mtandao wa Intaneti (The Internet)
Mtandao unakufungulia milango.
Unaweza kujifunza ujuzi wowote YouTube, kuingia kwenye masoko ya kimataifa, au kushirikiana na watu wa nchi nyingine bila visa.

c) Akili Mnemba (AI)​

AI haiji kuchukua nafasi yako—inakuja kukuongezea nguvu.
Jifunze kuitumia. Iwe ni kuandika, kupanga kazi, kutafuta taarifa au kubuni maudhui—AI ni msaidizi wako mpya.

Na siku hizi kuna kitu kinaitwa Agentic AI (AI inayoweza kurahisisha kazi za kujirudia rudia).
  • Ukiiweka kwenye inbox ya email yako, inaweza kukusaidia kusoma na kujibu
  • Unaweza kuiweka kwenye WhatsApp yako na ikawasiliana na wateja wako.
  • Kama una biashara, inaweza kukusaidia kukumbushia madeni, na kupokea simu za wateja.
  • Unaweza kupata ripoti za biashara na kufanya summary muhimu bila kuchukua muda mrefu.
  • Na, kwa wakulima na wafugaji, unaweza kutambua kasoro katika mimea au ugonjwa katika kinyesi cha mifugo ili kuleta tiba mapema (na kupata pendekezo la tiba).
“AI haitakuondolea kazi/ajira, lakini mtu anayeitumia AI anaweza kukushinda.”

Jenga, Ongeza, Tumia​

Ili kufaulu leo, si lazima uwe na pesa nyingi au nafasi kubwa. Unachohitaji ni:
  • Mtazamo sahihi
  • Ujuzi unaokua
  • Zana za kiteknolojia
Anza pale ulipo. Tumia ulicho nacho.

Signed,
Amba Jnr.
 
Natumia nyenzo zote hizo. Vinginevyo ningesharudi kwa mama kule Mwanza.
 
Haa yote ukisha fika miaka 30 unayaona sawa na hadithi za abunuasi,haya mambo ni muhimu mtu akiwa na miaka 14-24
 
Wewe hujatoboa......
Nakupa hii, Mimi niliwahi kufanya biashara nikamiliki around 60,000,000 zikakata zote na nikawa na madeni

Nimehangaika sana ikagoma.....baadae nikasoma mchezo na jibu likawa APPROACH EVERY SITUATION FROM SPIRITUAL ANGLE.

Weka usomi pembeni, tafuta jibu la kiroho la Hali yako, kwa sasa naona mshale unaanza kupanda japo taratibu ila kwa uhakika sana
 
Mimi mwaka juzi nilipoteza 80,000,000 ($30,000). Kwa hiyo huo mchezo unaouzungumza najua sana.
Spiritual angle informs the mindset. Inamaanisha unamwamini Mungu. Pili, add methodology to it. Tumia mbinu mbadala. Halafu adopt growth mindset, expand skillset, and adopt/adapt toolset. Huwezi kufeli.

Tatizo itatokea utakapoweka amount ya hela kwenye argument, na kuargue kuwa the more money you lose/make, the bigger umetoboa/kupata hasara.

Kuna wadogo zetu wako hapa. Tuwafundishe hili:
1. Fail first, fail fast, and fail forward. Utatoboa tu.
2. Failure is part of the process. Feedback comes there. You fail, you learn. You pass, you earn. Either way, you learn.
 
Barikiwa mkuu
 
Wewe umeshatoboa ? Kwa sababu ni hatari mno kuchukua ushauri kwa mtu ambae nae ni mganga njaa tu🤔
Waliotoboa huwezi kuwakuta wanaandika nyuzi ndeefu JF. Waliofanikiwa kuna ukuta huujenga wa namna ya kutoboa kama share mambo yao na watu, sio roho mbaya, ni ugumu waliokutana nao umewatengenezea fance flani. Wengi wanaoandika social media ni kusoma, kufikiru au practice kidogo. Hutamkuta aliyetoboa anatoboa siri
 
Tumaubiri akuekue ataelewa tu kuwa mtaa una elimu tofauti kabisa
 
Waliotoboa huwezi kuwakuta wanaandika nyuzi ndeefu JF. Waliofanikiwa kuna ukuta huujenga wa namna ya kutoboa kama share mambo yao na watu, sio roho mbaya, ni ugumu waliokutana nao umewatengenezea fance flani. Wengi wanaoandika social media ni kusoma, kufikiru au practice kidogo. Hutamkuta aliyetoboa anatoboa siri
100%
 
Inategemea uelewa wako wa neno "toboa".

Kama nililala njaa Jana leo nikapata namna ya kujilisha, sijatoboa tu?

Kama mwaka Jana niliishi kwa mshahara na leo biashara yangu ikanilisha na wafanyakazi wangu 15, sijatoboa tu?

Kama mwaka juzi kipato changu kilikuwa 15m mwaka mzima, na mwaka Jana na huu nikapiga 100m+ twice in a row, nimefeli?

Ukiangalia nlichoandika, ni principles tupu. Kama ni uongo, si useme ipi sio ya kweli?

Na nazifata zote, na they serve me well. Sasa nikiandika kwa ajili ya kusaidia wengine nimekosea wapi?

Ningeleta hoja ya umbea au utapeli, ungesemaje sasa?

Maana sijatoboa siri yoyote hapo ya maisha binafsi. Na kama nimesema kuwa nilipoteza 80m mwaka juzi, kuna shida gani. Kwa tajiri fulani hiyo ni hela ya mafuta ya Gari kwa mwezi, and that's OK. Mimi kwangu ambaye nlikuwa sijawahi kuvuka 20m kwa mwaka. That was a BIG lesson...

Kwa taarifa yako, nipo kwenye mastermind groups ya waliotoboa kweli kweli. 7 figure ya USD standards. And those guys follow principles. Wana share na watu. Sasa huu uchoyo wa vitu sijui ni ya hapa bongo tu. No wonder we live kwenye narrow mindset. Tunalea watu wenye akili hafifu, halafu siri zetu sisi "tuliotoboa" tunapeleka kaburini, ndo imsaidie nani huko?

Mentors wangu wanashare hizi principles. Na nimezijaribu zinafanya kazi. Kwani nikishare na wengine ni dhambi gani?

Uzi huu sio kwa ajili ya watu self important/sufficient wanaotunza siri (nashangaa ni siri ipi hiyo isiyojulikana) na "waliotoboa" tayari.

Ni kwa ajili ya wale wanaotamani kupiga hatua kutumia kanuni za mafanikio. Sio kuguess tu.
 
Back
Top Bottom