Silent Hero Huyu ni Mzalendo wa Kweli wa Taifa Hili, Ndie Aliyefanya Katiba Ifuatwe Mama Akawa!. Apewe Maua Yake!... Stahiki ni kuwa DGIS in Future!

Silent Hero Huyu ni Mzalendo wa Kweli wa Taifa Hili, Ndie Aliyefanya Katiba Ifuatwe Mama Akawa!. Apewe Maua Yake!... Stahiki ni kuwa DGIS in Future!

Hivi Paskali, nani aliyefanya mambo yaliyotufikisha hapa tulipo? Ni hao hao ambao wanaendelea kugawana majukumu jinsi wanavyotaka.

Halafu tunataka hao hao watutoe tulipo. That is to insult our own intelligence 😂 😂 😂 😂 😂
Kile chetu is the one and only, hivyo watu ni wale wale nchi ile ile na mambo yale yale, tukiwaambia watu ukweli mchungu,kuwa kitatawala milele, hawaamini!。
P
 
Kile chetu is the one and only, hivyo watu ni wale wale nchi ile ile na mambo yale yale, tukiwaambia watu ukweli mchungu,kuwa kitatawala milele, hawaamini!。
P
Nakiri hili kwa sababu nimekuja kujua late kuwa TZ hakuna UPINZANI at all .

Ila Paskali you have to trust , dunia inavyokwenda … kitaibuka chama cha Upinzani chenye Tija and along the way Katiba itabadilishwq hata kwa kumwaga damu and that will be the end of CCM

KUKITOA chama kilichotawala 60 years not so easy , with disaster…. Some days kitatoka

Kuna kizazi fulan lazima KIFE ndio changes zitokee…. Vijana wanazidi kuchanganyikiwa siku baada ya siku and CCM are not smart kukabiliana na hali huko mbeleni…. They still have old version of doing things

It is matter of time
 
Zamani scouting inafanyika shuleni picking the best brains。
P
Ujasusi wa leo ni UMBEA. Paskali kafanya nini nani kafanya nini. Etc kazi za TISS wa sasa hata layperson can do ….. ni kuchunguza maisha ya watu na kuwa mmbea na kubeba uhusika wa ukichaa that is as Fucq

Huku majuu intelligence ya nchi ina focus kwenye :
Technologies and digital transformation, Liquidity na Insolvency issues, economy na inflation, cybersecurity, AI, industrialisation, Monetary, investment and employment, language transformation etc

Like , with technologies Advancement, AI and Digital transformation , data science inayokuwa kwa kasi…. Kuna job nyingi sana zitapotea along the way …..je gvt ina take in place contigency plan gan kukabiliana na hilo wimbi la ukosefu wa ajira in the near vijana…. Vijana waliosoma watakosa ajira wataingia kwenye uhalifu na watachanganyikiwa …. Hatar sana kuwa na msomi kisha hana mishe za maana

; je What strategies serikali ifanye raia wapende investment kuliko kupenda kuajiriwq….. Those are analysis TISS should be able to put in place but hawa wa kwetu hata kutumia PC hawawezi kazi yao kuvaa kaunda suti na ear buds na simu za mkonge na black glasses kama vile tupo miaka ya ujima…..but leverage ya technology hawana…. Shame

Vita ya sasa ipo kwenye technology, infrastructures , industrialisation na Monetary
Vita ya TISS ipo kwenye kuhakikisha fulan anabaki madarakani, ´nani anaongea ukweli akamatwe But Capacity ya kuona unknown risk hamna….
Nchi nzima imejaa matangazo ya Samia, wakati izo ni business places ni sehemu za matangazo zinapaswa kulipiwa na ku collect kodi

Umasikini wa Tanzania unaanzia kwenye brain za viongozi
 
Okay baada ya mchonga kuachia ngazi , si kwa matakwa yake bali organ aliyeianzisha mwenyewe ilimkataa kwa sera zake mbovu za uchumi.
Na ilikuwa kwa lengo zuri , ili kufufua uchumi ulio kufa, ss hawa mabwana wamenogewa hawataki kuachia asali, na Wala hawejengi misingi mizuri kila citizens afaidi keki ya company, wao wanajiangalia wao na kizazi cha 3, imefikia hatua mpaka wanamiliki makundi ya utekaji na uhalifu, so saivi wanapukutishwa ibakie ngome MOJA TU, isiyo kuwa na wahuni na wasaliti

Kusema hakuna majawabu kwenye changamoto zetu sio sahihi. Kusema hakuna watu wenye uwezo wa kuleta mapinduzi chanya nayo sio sahihi.
Kitu ambacho nakishangaa ni kuzungusha wale wale kila siku halafu kutegemea matokeo tofauti. Na ni wajanja sana. Wanajua kupigiana debe na kutuaminisha huyu mtu anafaa maana tunamjua. 😂 😂
 
Wanabodi
Hii ni C&P ya Barua ya wazi kutoka kwa mwana JF huyu Mwandamizi!.
Sababu ya kuileta Barua hii hapa, ni kuwajulisha wanabodi na Watanzania, kuwa tuna Watanzania wengi ndani na nje ya nchi ambao ni wazalendo wa kweli wa Taifa hili, waliofanya vitendo vya kishujaa, bila kutaka kulipwa chochote!.

Kumbe huyu ndie shujaa wa Taifa, aliwezesha Rais Samia kutangazwa. Hayuko peke yake, kuna silent hero kwenye wale vijana wetu wa idara, Baada ya JPM kutwaliwa ile tarehe ile, vijana mashujaa wazalendo wakajua mipango miovu iliyokuwa ikipangwa, wakamtonya Chahali na Chahali bila kupoteza muda, akaipandisha youtube as breaking news.

Huku nyuma, wakakausha kimya as if nothing happened!, wakamtuma Samia Tanga kumzuga ili wafanye yao. Baada ya breaking news ya Chahali, Zanzibar walifuta shughuli zote, huku bara zikiendelea as if nothing happened!.

Usikute ni kitendo cha Chahali kumuacha the cat out of basket ndio kimepelekea CDF kujua, na kuingilia kati!.

Its high time wazalendo hawa wa taifa hili, wawe rewarded accordingly.
Hii ni barua yake kwa Mama ..
C&P

Dear Mama @SuluhuSamia: Mtu Huyu Hana Nia Nzuri Nawe, Anataka Kukufarakanisha Na Baadhi Ya Watu Wanaokusapoti


JAN 9

Dear Mama Samia,

Heri ya mwaka mpya 2025. Na uwe na heri na mafanikio.

Jana nilikutwiti Mama, kuhusiana na video iliyochapishwa juzi na mtu anayeitwa Cyprian Musiba, ambaye alinitaja kuwa miongoni mwa watu wanaokutukana, sambamba na kushirikiana na raia wa kigeni kukuhujumu na kuhamasisha uvunjifu wa amani.

Dear Mama, huyu mtu hajaanza tabia hii leo. Februari 2018, alinitaja kuwa miongoni mwa “Watu Hatari” waliopanga kuipindua serikali ya marehemu John Magufuli.

Na kwa takriban miaka mitatu mfululizo, aliendelea kunichafua kwa nguvu kubwa kupitia magazeti yake ya Tanzanite na Sayari Yetu na chaneli yake ya YouTube.

Dear Mama, sitaki kutumia tukio hili kuwa kama fursa ya mimi “kujisafisha” kwako, kwa sababu sijawahi katika wakati wowote ule kufanya chochote kile dhidi yako, sio tu kwa sababu wewe Mama ni Mkuu wa nchi bali pia kwa sababu bado nina imani na matumaini katika uongozi wako.

Ikumbukwe kwamba mimi ndiye nilikuwa Mtanzania wa kwanza kutangaza kuhusu kifo cha marehemu Magufuli, sio kwa sababu iwe breking news bali kwa sababu kulikuwa na mipango miovu ya kukiuka katiba kukuzuwia Mama usiwe rais.

Kadhalika, mara baada ya kufanikiwa kukwamisha jaribio hilo la ukiukwaji wa katiba na wewe Mama kuapishwa, nilikuwa mmoja wa watu wachache maarufu kujitokeza hadharani kukemea matusi dhidi yako yaliyojificha kwenye kivuli cha uanaharakati.

SIMULIZI ZA JASUSI

[Tahadhari Ya Matusi Ya Nguoni] Huu Sio Unaharakati, Haya Ni Matusi Na Udhalilishaji Dhidi Ya Mama Samia.​


EVARIST CHAHALI

MAY 17, 2021

“Kushindwa kuonya ni dhambi kubwa kabisa katika taaluma ya intelijensia.” Naam, sisi ambao bado tunaendelea kuwa wadau wa taaluma hiyo (hadi tunaingia kaburini) tunawajibika kuepuka dhambi hiyo.[/URL][/TD]

Na pengine mwanao Abdul hajawahi kukufahamisha kwamba niliwahi kuwasiliana nae nilipopata taarifa kuhusu mpango dhalimu wa kukuchafua mtandaoni, mpango uliomhusisha mtu mmoja ambaye sasa anajitanabaisha kama mtetezi wako mtandaoni.

Japo Abdul, hakunijibu, lakini naamini ujumbe husika ulifika na pengine kupelekea kutofanikiwa kwa mpango huu.
Tofauti na anavyojaribu kujinasibu muda huu, huyo mtoa tuhuma amekuwa miongoni mwa watu wanaoneza propaganda kwamba kifo cha marehemu Magufuli kilikuwa sio mapenzi ya Mungu bali “kazi ya watu waliouwa wanaiwinda nafasi yake (marehemu).” Nina hakika vijana wako wa Idara ya Usalama wa Taifa wanaweza kukuthibitishia hilo.

Kadhalika, alichofanya Musiba ni mwendelezo tu wa genge fulani ambalo linaamini kwamba kwa vile sijawahi kukukosoa katika namna nilivyokuwa namkosoa marehemu Magufuli - kwa sababu zilizo wazi - basi labda “unaweza kunikumbuka”.

Lakini kubwa zaidi, katika mwaka huu wa uchaguzi, kuna hofu kwamba labda nikaombwa kushiriki kwenye kampeni zako, kama nilivyoombwa mwaka 2015 kushiriki kwenye kampeni za marehemu Magufuli. Kwahiyo kinachofanyika ni ku- “preempt” uwezekano huo.

Mwisho, Dear Mama, mara kadhaa nimetanabaisha kuwa miongoni mwa sababu zinazonifanya niendelee kukuunga mkono, licha ya wajibu wangu wa kiraia, ni heshima yangu kwa wanawake. Marehemu mama yangu (Mwenyezi Mungu amlaze mahali mema peponi) alinifundisha kuwa “kila mwanamke ni taswira ya mama yako”, na kwangu heshima kwa “mama zangu” ni kama “amri ya Mungu”, sio suala la mjadala bali la lazima.

Kadhalika, Dear Mama, binafsi nina deni kubwa la shukrani kwako. Japo haipendezi kumsema vibaya marehemu, lakini kulifanyika majaribio kadhaa ya kunidhuru wakati wa utawala wa marehemu Magufuli, lakini mara baada ya wewe kuingia madarakani, umefanikisha kukomesha hilo japo watendaji wasio watiifu kwako waliwahi kufanya jaribio moja lililofeli.

Licha ya hilo, hata kijarida hiki na vinginevyo ninavyoandika sasa vinasomwa nchini Tanzania kutokana na wewe Mama kuondoa zuio la TCRA dhidi ya vyombo mbalimbali vya habari rasmi na visivyo rasmi kama kijarida hiki. Japo kuna “wasio na shukrani” wanaoweza kusema “ah si ametekeleza tu wajibu wa kikatiba”, sie tuliolelewa na kufundwa kuhusu umuhimu wa kushukuru, tunafahamu bayana kuwa hili liliwezekana tu kutokana na utashi wako na wala sio wajibu wa kikatiba, kama ambavyo ruhusa yako kwenye mikutano na maandamano ya wapinzani ilivyotokana na utashi wako binafsi na sio shinikizo lakikatiba/kisheria.

Uniwie radhi kwa kukuchukulia muda wako adimu lakini nimeonelea ni vizuri kuweka rekodi sawia, na wala sio kwa kuhofia kwamba unaweza kuamini tuhuma za Musiba - mzushi mzoefu aliyewahi kuwazushia tuhuma nzito za uongo viongozi mbalimbali nchini.

Nimalizie kwa kukutakia tena heri ya mwaka mpya.
Jamhuri ya Muungano, Kazi iendelee 🙏

Mwisho wa kunukuu
My Take.
Everist Chahali anastahili kupewa maua yake, tena kwa viwango vyangu mimi, huyu mtu anastahili kuwa DGIS!.

Uzalendo wake ni kama uzalendo wangu, tofauti yake na mimi, yeye ni Tiss, hivyo ana access na vyombo husika ikiwemo reaching out the core people akiwemo Abdul.

Mimi uzalendo wangu, kwa vile sio mtu wa kule, naufanyia humu JF only.

Hata mimi pia niliwahi kumuandikia barua Dear Mama... Mama, I'm here to support you, to serve our country. I'm here sio tu kuonesha ujuzi wangu kwa nchi yangu, bali pia kuutumia. But...
Kiukweli Erick Kabendera ametusaidia sana watu kufunguka!. Aliyefunguka hapa ni TISS kwenye barua hiyo ni TISS!.

Paskali!.

Duuuh,ila dhana inaweza ikawa sio halisi lakini kwa uhakika kwa asilimia kubwa kwa yanayoendelea wakati mwingine na yanayosemwa na Kabendera kama ni ya kweli basi mchongo wote yule Makamu wa Rais Mabuto alikua anajua mchongo wote .

Mengine yote yalikua ni zuga tu sijui ameenda ziara Kabanga ,sijui wanataka kukiuka katiba ,ni usanii tu . Mchongo ulichezwa na waliocheza mchezo walitaka mtu wanayemtaka amerithi mabutu asiwe kama Mabuto na cheche zake .
Dili lilikua linajua kwa wazi nani atachukua nafasi . Waliojaribu kuhujumu mipango ya uapishwaji ni kwa sababu tu hawakujua dili lilipoanza na hawakushirikishwa hujuma nzima ya kuama ugomvi.
Kifo cha Mabuto kilineemesha wengi kwa namna mbalimbali .Wengi waligawana viroba vya fedha ,wengine dhahabu ,wengine madaraka na kupata fursa ya kuuza rasilimali za Kongo kiholela kuonyesha kuwa walikua wamejipanga kumpoteza Mabutu kwa umoja wao.
 
Pasco unaweka hadi mabandiko ya kuji brand mtu unashindwa kujua unapigia chapuo nini! Sasa mabandiko ya 2015 yanahusika vipi? Unaji brand sana
Nasikitika kuona kuwa umechelewa sana Kuling'amua hili, ila analo Kiasili na ndiyo linamgharimu Kutwa tu kiasi kwamba yupo yupo tu wakati Wenzake 'wanaukata' tu kila Kukicha.
 
Anafaa kuwa nani sasa? Rais au Mwenyekiti wa Chama cha habari au CEO wa kampuni yako?

Huwa siwaamini kabisa spies. Mtu aliye nje ya system sababu ya kukizanzana na maboss wake kwenye kazi anayoipenda sana, unamuaamije anamaanisha anachosema?

Just for your information, the guy is one of those rare local species with the art of disguising the public. He is good at deception
Chahali nadhani yuko huko na bado yuko kazini, ni namna tu aishi vipi huko ughaibuni ila bado anaitumikia serikali ya JMT kwa uaminifu mkubwa.
 
Mkuu Ozon, ni kweli ila ni baadhi tuu,hii thread sio ya watoto!。
P
Mkuu Mayalla vipi nikimwangalia maza ni kama anajiandalia mazungira mazuri kwa kampeni zake hasa kwa hizi tetesi za kumdhamini Mbowe nadhani lengo lake akipita Mbowe kwenye uenyekiti na kwa kuwa atakuwa amewezeshwa na mama atamuwekea mgombea ambaye atakuwa soft au atakayepangiwa yapi ayaseme kwenye kampeni.

Unadhani kwa mazingira hayo anaweza akamwachia mwanaume agombee kama sauti yako ya ndani inavyokutuma, huoni kama mazingira ya fomu moja yanamtengenezea njia ya kupeperusha bendera ya wanakijani bila kikwazo. Unadhani nini kitatokea ili mgombea awe mwanaume maana ni kweli mara nyingi unayoyaandika yamekuwa yakitokea. Na mimi pamoja na kujikataa kuwa wewe ni kipepeo ila kuongea kwako kutembea kwako na mwonekano wako unaonyesha kabisa wewe ni kipepeo ambaye hutaki watu wajue hilo japo si lazima kila mtu ataamini maana hamjitangazi hadharani.
 
Nakiri hili kwa sababu nimekuja kujua late kuwa TZ hakuna UPINZANI at all .
Mkuu Megalo, Megalodon , kwanza nimefarijika sana kwa kauli yako hii, you are a genuine person, watu genuine ni wachache na most times ni wanachukiwa na society, wanachukiwa na wengi kwasababu ni wakweli kupitiliza, Mwalimu Nyerere was one of them, JPM was another, hata TAL akipunguza u ropo ropo!. Thanks for genuity!.
Samia alipoingia, she was very genuine, ni mkweli, mpenda haki na mtenda haki, she was very genuine kutaka kuwatendea haki Watanzania, tatizo lake ni moja tuu, naomba kwa heshima ya kiongozi wetu mkuu, nisilitaje. Kutokana na tatizo hilo, wahafidhina wa CCM, reached her, wamefanikiwa kim brain wash, sasa anawasikiliza, na kiukweli wanamdanganya sana!. Mtandao huu tumeendelea kumsaidia kwa kumweleza ukweli kama huu
Ila Paskali you have to trust , dunia inavyokwenda … kitaibuka chama cha Upinzani chenye Tija and along the way Katiba itabadilishwq hata kwa kumwaga damu and that will be the end of CCM
True
KUKITOA chama kilichotawala 60 years not so easy , with disaster…. Some days kitatoka
True
Kuna kizazi fulan lazima KIFE ndio changes zitokee…. Vijana wanazidi kuchanganyikiwa siku baada ya siku and CCM are not smart kukabiliana na hali huko mbeleni…. They still have old version of doing things
This is very true, na hili la kizazi kife kiibuke kingine, hata mimi nimelisema Uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM! Wajinga karibu wote watakuwa wamemalizika!
It is matter of time
Nakubaliana na wewe, my initial calculatins was 2030, but kumetokea fursa 2025 kupitia TAL!. Japo Lowassa Alikuwa a Liability CCM, Akawa Asset Chadema. Lissu is a Very Bad Liability, but is The Only Asset Chadema Has Kuwangiza Ikulu!. Je... ?
P
 
Kamwa kweli ni mzalendo mwambie aje hadharani kutoboa siri ya kilichomkuta JPM mara tu baada ya kutoka kufungua majengo ya polisi kule Kurasini hapo ndipo urejee kumsifia mtu mwenye kiburi, jeuri , ujuaji nk. TISS safi hajiweki hadharani kama huyu alivyo, huyu anatafuta maslahi tu, ndio maana kipindi cha mwanzo cha utawala wa JPM walikuwa marafiki sana lakini JPM alipombaini ni ndumila kuwili akaghairi kumpandisha cheo kwenye kitengo na wenzie waliokuwa wananyemelea walipogundua uchonganishi ukachochewa hadi huyu mtu wa milimani akatimkia Uskochi huko hadi leo.
Chahali alitimkia Scotland kabla ya utawala wa Magufuli, huko unakosema sijui alitaka kupandishwa cheo na JPM ni uongo uliokubuhu
 
Chahali nadhani yuko huko na bado yuko kazini, ni namna tu aishi vipi huko ughaibuni ila bado anaitumikia serikali ya JMT kwa uaminifu mkubwa.
No, huyu ni mtu wa intelligence ambaye pia ni intelligent,wengi wa huko siku hizi ni majinga tuu, ndio maana yalishindwa kumprotect yule mtu wetu。

Kuna namna ambayo hawa jamaa huwa wanafanya to do away na watu wao ambao they are done with,the ejecting mechanism differ,hivyo alipotonywa he is about to be ejected,akaamua kuwawahi kwa ku deffect kabla! 。Jamaa ukiwawahi, wanakasirika sana,angekuwa within their reach,wange mu imrankombe!。
P
 
Back
Top Bottom